Vifo na Vipigo JKT intake June 2014 vichunguzwe

Vifo na Vipigo JKT intake June 2014 vichunguzwe

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
652
Reaction score
607
Kuna taarifa kuwa mwezi mmoja tu baada ya wanafunzi wa kidato cha sita kuanza mafunzo ya JKT tayari vifo vimeripotiwa.

Kifo cha wiki mbili zilizopita ni tukio lililotokea katika kambi ya JKT Oljoro iliyopo Arusha ambapo inasemekana binti kutoka Rombo mkoani Kilimanjaro alifariki dunia kwa Pneumonia baada ya kukataliwa matibabu.

Hapo hapo Oljoro kijana mwingine amepigwa na afande na kuvunjwa mbavu na amelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC.

Matukio haya yanatufadhaisha sana wazazi na kutujengea hofu kuhusu aina ya treatment wanazopewa watoto wetu kwani tulishuhudia awamu iliyopita ikighubikwa pia na wimbi la vifo vya watoto wetu waliojiunga JKT baada ya mafunzo haya kuanzishwa tena.

Sina uhakika kama askari wanaopokea watoto hawa wamepewa mafunzo maalum ya kuwa treat watoto ambao ndio kwanza wanatoka mazingira ya shule na kwenda jeshini.

Inawezekana kabisa maaskari walioko kambini na jeshini kwa zaidi ya miaka 5-20 kutaka kuwa transform wanafunzi hawa kuna wanajeshi kama wao katika kipindi kifupi hiki cha miezi 3.

Siamini hata iweje kuwa kipindi cha miezi mitatu mwanafunzi anayokaa JKT kitatosha kumfanya afikie calibre ya Uanajeshi mkakamavu.

Hii ni sawa na kulazimisha mimba ya mtu kutungwa na mtoto kuzaliwa katika kipindi cha miezi mitatu, jambo ambalo haliwezekani.

Ni lazima wajue wao walikuwa wanajeshi kamili baada ya mafunzo ya muda mrefu wakipitia hatua moja baada ya nyingine na huu ni utaratibu ambao naweza kusema ni natural phenomenal.

Kitendo cha kuwataka wanafunz hawa wawe wanajeshi kamili kwa muda mfupi kinawafanya askari hawa kuwa subject katika harsh environment kwa ghafla.

Ikumbukwe hata mche wa mmea unapohamishiwa kwenye shamba kubwa kutoka kwenye kitalu huhitaji uangalizi wa karibu kikiwemo kivuli, maji na bada ya muda unashika chini na kuanza kupambana kustahimili mazingira magumu wenyewe.

Wanafunzi hawa ni kama miche iliyotolewa katika kitalu na hivyo wanahitaji mafunzo yawachukue hatua kwa hatua hadi watakavvozoea na si ku wa induce kuwa full wanajeshi overnight.

Hapa mtawaua wengi!!!. na hiki ndicho chanzo cha vifo na vipigo. Tofauti na huko nyuma, wanafunzi wanaoingia JKT sasa wana umri mdogo ukilinganisha na sisi tulivyoingia kipindi cha miaka ya nyuma hadi JKT kwa mujibu wa sheria iliposimamishwa miaka ya 1996/97.

Mzazi anategemea mtoto akitoka JKT arudi kujiunga University lakini badala yake wanapokea maiti na walemavu na hivyo kukatiza juhudi zote za kumsomesha mtoto yule.

Hiki sicho mzazi alichotarajia hata kidogo. Wazazi wamekuwa na hofu kubwa hususani kutokana na aina ya mafunzo yanayotolewa na kugharimu maisha ya watoto wap. Inakuwa kama mtoto amekwenda vitani mstari wa mbele!!!.

Tunawasihi maafande wawaone watoto hawa kama watoto wao, watangulize utu mbele badala ya ukatili na kama kweli wana facilities za afya mtoto akiumwa basi wasiwa tease na kuona wana deka.

Kama hatua hazitachukuliwa tutakuwa tukishuhudia vifo vya watoto wetu miaka nenda rudi na JKT zitachukuliwa kama kambi za mateso na vifo kama zile za Adolph Hitler (concentration camps) na si kambi za mafunzo.

Mimi kama mzazi naiomba serikali ifanye uchunguzi wa sababu ya vifo na vipigo katika kambi za JKT ili wanaohusika au kuzembea wakibainika wachukuliwe hatua kali ikiwamo kufukuzwa kazi.

Lakini pia watoe mafunzo maalum kwa askari watakao kuwa wakiwafundisha wanafunzi kutoka mashuleni.
 
Jamani imeanza tena mbona inatisha hii jambo. Are we taking it simplly
 
daah mdogo wangu wa kike yuko kambi ya tabora,mdogo wangu wa kiume yuko morogoro kambi ua cheater,mjomba wangu wa kike nae yuko kambi ya mafinga......nikionaga habari kama hizi nakosa amani kweli kweli "mungu waepushie mabalaa yote yenye makusudi ya wanadamu".
 
kaa ukijua ya kwamba intake moja ikiingia adi kuja kumalizika kwa mafunzo lazima mtu afe, ilo siyo geni kiongozi
 
kaa ukijua ya kwamba intake moja ikiingia adi kuja kumalizika kwa mafunzo lazima mtu afe, ilo siyo geni kiongozi

Kujua ni jambo moja na kuchukua hatua kudhibiti ndio sehemu ya maendeleo ya vikosi husika na nchi kwa ujumla!!!!!

1. Kupima afya
2. Kutunza afya husika
3. Kuingiza mafunzo katika afya hiyo ili kupata "matunda"

Sio zaid ya hapo wala pungufu yake!!!!
 
Hata mimi najua lengo la JKT kwa watoto wetu ni kuwajenga kikakamavu na kuwajengea uzalendo na siyo kuwaonyesha kuwa jeshi ni gumu. Lakini najua maafande wengi wanataka watoto waone jeshi ni gumu . Mbaya zaidi unaonyesha ugumu kwa kuwanyima matibabu jambo ambalo hata kwa mwanajeshi mwenyewe akikosa atakufa sembuse mtoto wa shule.
 
vyombo husika ni vema wakasaidia kujua ukweli wa jambo hili linaukweli kiasi gani.
 
Hao wajeda wa jkt wanapenda masifa sana ka duly sykes vile..r.i.p kwa walioaga dunia na pole kwa walio umizwa na hao wajeda
 
Kujua ni jambo moja na kuchukua hatua kudhibiti ndio sehemu ya maendeleo ya vikosi husika na nchi kwa ujumla!!!!!

1. Kupima afya
2. Kutunza afya husika
3. Kuingiza mafunzo katika afya hiyo ili kupata "matunda"

Sio zaid ya hapo wala pungufu yake!!!!

Mimi nilipitia JKT Makutopora.Kwa wakati huu JKT imerudishwa lakini inahitaji maandalizi,akili na maarifa.Ikumbukwe kwamba vijana wanakwenda huko kwa lazima.Hawajapitia serious medical test.Na wengi hawana nia ya kuwa askari.Ni muhimu haya yazingatiwe
1)wapewe huduma nzuri za afya
2)WAPATE CHAKULA KIZURI.kwa wakati na cha kutosha
3)wapate sehemu nzuzi za kulala.pamoja na mosquoto net +blankets
4)wafanye kazi kiasi na kwa akili

KAMA SEREKALI HAIJAJIAANDAA NI VEMA KUYASITISHA
Wapewe mavazi maalum na viatu
 
kujua ni jambo moja na kuchukua hatua kudhibiti ndio sehemu ya maendeleo ya vikosi husika na nchi kwa ujumla!!!!!

1. Kupima afya
2. Kutunza afya husika
3. Kuingiza mafunzo katika afya hiyo ili kupata "matunda"

sio zaid ya hapo wala pungufu yake!!!!
practice and procedure hata ukipinga siye tulipita huko vijana kadhaa tuliwazika
 
kuna mmoja aliripoti jkt siku hiyo hiyo akavunjwa mguu
 
Nilipita jeshini intake ya kwanza OP "miaka 50 ya JKT", Kanembwa jkt 821 KJ...!!!

Kwanza mleta mada usilete upotoshaji, ni kinyume kisheria hata kwa sheria za hapa JF.
Unaposema vifo you explicitly mean ni zaidi ya kifo ki1, mpaka sasa ni kifo ki1 tu ambacho kimeharifiwa. RIP...

Hakuna mtu anayeweza kuzuia kifo anywise....
Mazoezi ya jeshini ni ya kawaida sana, in such a way that, kila mtu anaeza kushiriki kama afya yake ipo sawa.
Accidents happens bhana, who knows even the next second??? So ukisema mtu alivunjwa mbavu kwa kupigwa teke bado hainiingilii akilini, kwani ameenga kuuwawa, amaa???

Acha vijana wale cozy bana, wapate ukakamavu, uhodari, uvumilivu, nidhamu, mafunzo ya kijeshi, uzalendo nk nk...
 
hivi wewe ni mzima kweli..watoto wamekwenda jkt juzi tu kifo kimeripotiwa unaona sawa tu. wewe utakuwa mwehu
 
Back
Top Bottom