Vifo na Vipigo JKT intake June 2014 vichunguzwe

Vifo na Vipigo JKT intake June 2014 vichunguzwe

Nilipita jeshini intake ya kwanza OP "miaka 50 ya JKT", Kanembwa jkt 821 KJ...!!!

Kwanza mleta mada usilete upotoshaji, ni kinyume kisheria hata kwa sheria za hapa JF.
Unaposema vifo you explicitly mean ni zaidi ya kifo ki1, mpaka sasa ni kifo ki1 tu ambacho kimeharifiwa. RIP...

Hakuna mtu anayeweza kuzuia kifo anywise....
Mazoezi ya jeshini ni ya kawaida sana, in such a way that, kila mtu anaeza kushiriki kama afya yake ipo sawa.
Accidents happens bhana, who knows even the next second??? So ukisema mtu alivunjwa mbavu kwa kupigwa teke bado hainiingilii akilini, kwani ameenga kuuwawa, amaa???

Acha vijana wale cozy bana, wapate ukakamavu, uhodari, uvumilivu, nidhamu, mafunzo ya kijeshi, uzalendo nk nk...


Unapo sema kifo kimoja unaonaje kikiwa cha mwanao wa pekee?.
vijana wapelekwa taratibu ukizingatia mfumo wa maisha umebadilika,watoto wame legea toka majumbani. wamekulia soseg na kazi lainii.
kwa taarifa yako ata wa vijijini sikuhiz sio wakakamavu kwahiyo transformation ina takiwa taratibu.
 
ni kweli inauma kwa wazazi, walezi, jamii na hata taifa kwa ujumla tunaposikia nguvukazi imepotea, lakini tukumbuke kuwa pia vifo si jeshini pekee, ni kila mahali hata ulipokaa chaweza kutokea pia, sasa tumeambiwa vifo vimeripotiwa halafu tunaambiwa aliefariki ni mmoja, tuwe wakweli kwenye issue nzito kama hizi pia hakufariki kutokana na mazoezi au mafunzo ni ugonjwa ambao unaweza mpata yeyote mahali popote, kupona au kufariki ni matokeo ya ugonjwa, pia jamii kuna mahali tunakosea tunapoambiwa tujaze medical sheets kwenye hospital zinazotambulika kabla ya kuhudhuria mafunzo yoyote wengi wetu hudharau huchukua na kwenda kujaza popote bila vipimo husika kufanyawa nimeshuhudia haya ili mradi hilo zoezi liopite sasa madhara yake utahudhuria mafunzo bila kufanyiwa vipimo kama ulikuwa na ugonjwa awali unategemea nini, pili malezi ya vijana wa sasa ni shida mashuleni wanaendekeza migomo na vurugu unategemea wakienda jkt watakuaje si ni viburi tu kwa maafande? sasa kuepusha haya tujaribu kuzingatia taratibu zote za afya, utii na nidhamu, wao si wa kwanza wengi wetu tumepita jkt tunajua, na tunaona vurugu za hawa vijana wetu na baadhi ya wazazi tunashiriki kwenye vurugu hizo pengine kutokana na ukubwa wa vipato kuwa hata mtoto akifukuzwa shule ya serikali atakwenda private ambalo zamani halikuwepo ndio mana nidhamu ilikuwa juu, nawakilisha.
 
Kwani ni lazima mzazi kumpeleka mwanae huko?

Unaweza kwenda kumchukua ukiwa na wasiwasi wa afya yake?
 
Huyo tuachane naye
Inawezekana atakuwa hapo ruvu kwani wao ndo wanakimbilia hapo;

Hilo la kunyimwa vyeti ni kwa wote watakaokwepa kwenda jkt.
Huyu huyu uliyemuulizia au Watanzania????!!!
 
Kule jkt hata uende na cheti cha daktari mkuu wa muhimbili ni lazima ukapimwe upya;
Kwani ni lazima mzazi kumpeleka mwanae huko?

Unaweza kwenda kumchukua ukiwa na wasiwasi wa afya yake?
 
Maboresho kweli ni muhimu sana tena yafanyike haraka sana;
Naamini Serkali yetu sikivu italifanyia kazi
Kwa kuwa mimi ni sawa pia na niko kambini kipindi hiki as
my dota yuko pale siwezi kusema kitu zaidi;
Ritz pitia huku pia.

Bora..kuna vitu vya kuangaliwa upya kwa dhumuni la maboresho!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Namshukuru Mungu ujumbe huu umewafikia siyo serikali tu bali JWTZ.

Hivi leo JWTZ wametoa tamko kukanusha habari hizi ingawaje ni za kweli. Naomba wasiishie kukanusha lakini wabadilike na wawatreat watoto wetu kama watu na si kana kwamba wanapambana na adui katika uwanja wa mapambano. Waelewe wako na watu tena watoto wadogo wengine hata miaka 18 hawajafika.


Waache tabia ya kuwanyoa hadi waone damu kana kwamba wao ni vampire. Naomba kusisitiza kuwa ujumbe huu si uvumi wala uzushi na hakuna siri ya jeshi iliyovujishwa hapa kwani aliyefariki hakuzikwa kambini bali nyumbani kwao na jamii ilihudhuria mazishi. aliyevunjwa mbavu hakufichwa kambini bali alipelekwa hospitali na ndugu jamaa na marafiki walienda kumjulia hali.

Kama JKT itashindikana kuendeshwa kisayansi na kuyafanya mazingira friendly kufanikisha mafunzo husika ni bora ifutwe la sivyo kambi hizi zitageuka kuwa chimbuko kubwa la makaburi ya vijana wadogo ambao taifa linawateg emea.
 
JKT SALAMA: JWTZ yatoa tamko leo kukanusha ujumbe unaosambaa kwenye simu ukidai watoto wanakufa kambini JKT shauri ya mazoezi magumu, wasema mafunzo ni salama.
 
JKT SALAMA: JWTZ yatoa tamko leo kukanusha ujumbe unaosambaa kwenye simu ukidai watoto wanakufa kambini JKT shauri ya mazoezi magumu, wasema mafunzo ni salama.

Hao wanajeshi wenyewe joto hasira na wanamalizia kwa watoto.WABADILIKE waache kutoa matamko.
 
Huko watoto watarudi watukutu sana, magaidi watatokea huko kwani wanajua kushika bunduki na kazi hakuna mtaani mtakomaje.
Magonjwa mengi yatapatikana huko pia
 
Kamchukue mwanao/nduguyo umfundishe nyumbani
Kwani lazima apitie mafunzo ya JKT? Hv waliomaliza forma six tangu 1995 hadi 2012 bila kupita JKT wamepungua nini ? JKT is and will never be one of the basic needs of life. Hii ni aina ya passage tu
 
JKT SALAMA: JWTZ yatoa tamko leo kukanusha ujumbe unaosambaa kwenye simu ukidai watoto wanakufa kambini JKT shauri ya mazoezi magumu, wasema mafunzo ni salama.

Wamezoea ku politisize kila kitu.
 
Namshukuru Mungu ujumbe huu umewafikia siyo serikali tu bali JWTZ.

Hivi leo JWTZ wametoa tamko kukanusha habari hizi ingawaje ni za kweli. Naomba wasiishie kukanusha lakini wabadilike na wawatreat watoto wetu kama watu na si kana kwamba wanapambana na adui katika uwanja wa mapambano. Waelewe wako na watu tena watoto wadogo wengine hata miaka 18 hawajafika.


Waache tabia ya kuwanyoa hadi waone damu kana kwamba wao ni vampire. Naomba kusisitiza kuwa ujumbe huu si uvumi wala uzushi na hakuna siri ya jeshi iliyovujishwa hapa kwani aliyefariki hakuzikwa kambini bali nyumbani kwao na jamii ilihudhuria mazishi. aliyevunjwa mbavu hakufichwa kambini bali alipelekwa hospitali na ndugu jamaa na marafiki walienda kumjulia hali.

Kama JKT itashindikana kuendeshwa kisayansi na kuyafanya mazingira friendly kufanikisha mafunzo husika ni bora ifutwe la sivyo kambi hizi zitageuka kuwa chimbuko kubwa la makaburi ya vijana wadogo ambao taifa linawateg emea.

Ni kweli mkuu hata mimi nimesikia hili tamko. Ila tamko liambatane na kuwachukulia hatua waliowavunja watoto mbavu na kusababisha vifo
 
JWTZ msitoe makanusho blind bali yaambatane na reformation ya the entire Jeshi ili kuepuka matatizo kwani naamini mtoa mada ana hoja na hana kisasi na JKT.
 
JKT SALAMA: JWTZ yatoa tamko leo kukanusha ujumbe unaosambaa kwenye simu ukidai watoto wanakufa kambini JKT shauri ya mazoezi magumu, wasema mafunzo ni salama.

taarifa ya jkt imejaa vitisho wakati ni kweli kuna mtoto amefariki jkt oljoro..wanaposema hatua kali zitachukuliwa kwa yoyote aliesambaza habari za kifo wanamaanisha nini? wanataka kutisha watu wasiripoti madudu yao?
 
jkt badilikeni, wachukulieni hatua kali wanaotesa vijana kwenye makambi, kumbukeni.kuna ndugu zetu na watoto wetu huko wanaotupa taarifa ya kila kitu kinachoendelea huko
 
Back
Top Bottom