Video: Uchochezi wa Lowassa huu hapa

Video: Uchochezi wa Lowassa huu hapa

Lugha ambayo serikali itaielewa ni ile isiyokuwa ya kichochezi.
Lugha ya kichochezi na vurugu serikali haielewi na inapambana na wewe.
 
Mkuu unataka tufe kikondoo?

Jifunzeni kuwa mnaweza kuuua mwili lakini hamtaweza kuua mawazo ya watu. Mnapoona mmewaza sana mjue kuna wengine wamewaza zaidi yenu.

Mnapoona mnatumia mbinu za kudhibiti kuna walio na mbinu na kujinasua na kuwapa changamoto.

Kama hamjui Magu ni mchafu kiakili na kimwili si wa kumtetea kwa mabaya anayoyafanya. Msisahau mlimpeleka Ujerumani kwa matibabu ya akili.

Mwisho kumbukeni ujumbe wa inzi "Mkijua medani na mbele wenzenu wamebobea medani za nyuma"
 
Unataka kutwambia kuwa wewe ndiyo unajua makosa kuliko serikali na wataalam wake wa mambo ya kiusalama?naona unajisikia uchungu kwa serikali kumwachia leo

kwani kuachiwa leo maana yake hana kosa?

wakili wake amesema "shitaka ni uchochezi."

maana yake ana face shitaka la uchochezi.

Mkurugenzi wa upelelezi yeyote yule lazima amemuuliza, Mheshimiwa una maana gani kusema WAISLAM WAANZE KUONGEA LUGHA SERIKALI INAYOILEWA, UNATAKA WAFANYEJE, WATUNGUE RISASI ASKARI KAMA KIBITI?

Kati ya wanasiasa wote usingetegemea Lowassa ambae huwa anajiweka kama soft-spoken elder statesman anaependa maridhiano leo aseme Waislam siku hizi wamekuwa baridi.

Kasema anataka Waislam warudishe zile siku za misikiti kufuatiliwa na serikali. Mheshimiwa umejichafulia hadhi yako.
 
Lugha ya waislam inayoeleweka wewe kwako ni kujilipua! kumbe wewe ndiye unatakiwa ukaripoti polisi!
 
Alikosea. Na hii ni Mara pili nakumbuka kwenye uzinduzi as kampeni uchaguzi mkuu uliopita alisema akichaguliwa kuwa raid atawaachia wale mashehe waliofungwa.
 
Alikosea. Na hii ni Mara pili nakumbuka kwenye uzinduzi as kampeni uchaguzi mkuu uliopita alisema akichaguliwa kuwa raid atawaachia wale mashehe waliofungwa.
Kuna mwingine alisema tukichagua upinzani ataingia msituni,hakuitwa kuhojiwa!
 
Matatizo ya Waislam ni pamoja na MOU Kati ya Makanisa na Serikali inayolazimisha Serikali kutoa ruzuku kuendesha Shughuli za Makanisa na aliesaini huo Mkataba upande wa Serkal ni Prof Mahalu na Edward Lowassa 1992, alitolee ufafanuzi badala ya kutafuta Kick za Kwmy Futari
 
Kuna mambo yanaleta ukakasi.

Mashehe wa Zanzibar walikamatwa wakati wa Rais Kikwete, Lowassa hakusema chochote, na kipindi hicho Tanzania haikuwa na tatizo la Kibiti. Watu zaidi ya 30 wameuwawa katika mazingira ya kutatanisha, halafu anaibuka Lowassa ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu anawakusanya Waislam nyumbani kwake na kuwaambia "WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA". Lowassa anakwenda mbele zaidi na kuwakumbusha namna 'watu walivyotumia dini kuleta machafuko wakati wa Rais Mwinyi.

Maswali ya kujiuliza,

1. Mbali na maagizo aliyotoa hadharani, Lowassa amekuwa anafanya nini nyuma ya pazia?
2. Lowassa anajua nini kuhusu Kibiti?
3. Lowassa ana maana gani anapoagiza waislam waongee 'lugha ambayo serikali inaielewa? Hiyo lugha ikoje?
4. Ni kwanini ametolea mfano wa mchafuko ya kidini wakati wa Mzee Mwinyi?
5. 'Shehe' ambaye amekuwa anafuatana na Lowassa kila mahali (hata leo alikuwa naye) ni kwa ajili ya maombi au ndiye msimamizi mkuu wa 'lugha' ambayo Lowassa anataka waislam waitumie.

Kuna tatizo kubwa.
Kwenye maisha ya kawaida kumdhania mtu ni dhambi haisameheki na Mungu. Sema mnajidhania kuwa watu wanawaona mnavyo ropoka, mnakurupuka hamna maono. Msijidhanie ni ukweli hamna maono mnaropoka sana mnakurupuka mna kauli za kupishana utadhani ni genge la walevi.

Kauli ya waziri mkuu makamu wa rais mawaziri kwenye suala la mimba za watotowa shule kila mtu kivyake.

Utawala wa sheria ulikwisha zikwa kwa hiyo lazima makelele yapigwe ili msikie. Watu gani mmekufa ganzi kwa wanayowapata masheikh tena wa uamsho ili mradi nyinyi mpo kwenye utawala?
 
Mkuu unataka tufe kikondoo?

Jifunzeni kuwa mnaweza kuuua mwili lakini hamtaweza kuua mawazo ya watu. Mnapoona mmewaza sana mjue kuna wengine wamewaza zaidi yenu.

Mnapoona mnatumia mbinu za kudhibiti kuna walio na mbinu na kujinasua na kuwapa changamoto.

Kama hamjui Magu ni mchafu kiakili na kimwili si wa kumtetea kwa mabaya anayoyafanya. Msisahau mlimpeleka Ujerumani kwa matibabu ya akili.

Mwisho kumbukeni ujumbe wa inzi "Mkijua medani na mbele wenzenu wamebobea medani za nyuma"
Matibabu ya akili tena? Hapo tunahitaji utupatie ufafanuzi kidogo
 
Kimsingi lazima watanzania wote tuongee lugha ambayo serikali itatuelewa, haiwezekani maisha magumu halafu wao wanakenua tu meno.
 
Kwanza ukamatwe wewe kwa kumjengea Lowassa maana ambayo hakumaanisha. Lugha ambayo serikali inaielewa ni nini? Unajua ENL alimaanisha vipi?

Je, kama alimaanisha waache kutumia Lugha za Kiarabu na badala yake Kutumia Kiswahili ama Kingereza kama ambavyo zimekuwa lugha rasmi za Kiserikali?
Na hapo ndiyo Lissu atakapomburuza wakili wa serikali kwenye hii kesi.
 
KAMISHINA MLOLOWA BABA ,KAMILISHA HARAKA UCHUNGUZI WA RICHMOND, HUYU JAMAA AENDE SEGEREA HARAKA
 
Siku zote ukisoma hali ya hewa ilivyo, toa tungo zinazoendana na hali halisi ilyopo, ili kila mtu atafsiri kwa kadri ya uwezo wake, hiyo ni mbinu shirikishi ambayo inatusaidia sisi raia kuibia majimbu ambayo yeye hana na atsyapata kwa raia, yamkini yeye alimaanisha jambo dogo ila wafasili wakaleta makubwa kutokana nauelewa wao mpana hivyo kuzidi kumnufaisha mtoa mada,
 
Uislam hautaki kudhulumu, na kutodhulumiwa haki.ENL amekumbusha tu!
 
"....msiwe baridi........."-E.L.
sikiliza kuanzia 1.44 na shirikisha kidogo akili utamuelewa!
Ndiyo wasiwe baridi wapaze sauti zao ili kilio chao kisikike.

Hivi haya maneno ya mafumbo mtaanzia wapi kuyajengea shtaka au ndiyo mnataka Lissu awanyooshe tena mahakamani muanze kumtukana?
 
Back
Top Bottom