forest zone
JF-Expert Member
- Jun 10, 2017
- 253
- 228
Natamani mwisho wa ccm ufike nikiwa hai maana najua kabisa hata wao wanajua hawatendi haki.
tena ya pale uhuru na msimbazi!FaizaFoxy hapa lazima abaki njia panda!
Mimi sioni kasoro yoyote katika kauli yake, bado ukweli upo pale pale mashehe waachiwe, haki za binadamu zinakiukwa
kwa Kosa gani? Lugha ambayo huwa serikali inaielewa ni ipi? Unajua alimaanisha nini? Ukisema lugha ambayo mbunge ataielewa ni ipi ? Mtu anaweza kusema 2020 tutatumia lugha ambayo ccm watatuelewa kuwa hatufurahishwi na wao ( akiwa na maana 2020 tutawachagua wabunge wa upinzani)Kama kweli Lowassa aliongea hivyo mbona walichelewa sana kumkamata huyu mtu!
Kulitokea nini wakati wa mwinyi ambacho ni kosa Ktk katiba yetu ya sasa?Tatizo haliko kwenye matumizi ya lugha peke yake, msikilize vizuri anawa mfano jinsi waislam 'walivyoongea' wakati wa Mzee Mwinyi. Sijui una umri gani lakini kwa watu waliokula chumvi kidogo wanakumbuka nini kilitokea kipindi hicho. Mungu apitishe mbali.
Mabwege yanajionaga maungwana halafu madhalimu ya haki za watu yanaishi kwa khofu kama makunguru ya mjini kwa sabab yanajua wazi juu ya maovu yao kwa watuKwahiyo ktk akili yako lugha nyengine ni kujilipua tu.? Hivi nyie watu wa CCM mbona hamna busara! Mbona mmekaa ki shali shali tu. Hivi kauli ya kuzungumza lugha nyengine na kauli ya tutawashulikia ipi ya uchochezi? Huu ubaguzi mnaoupalilia huu, ohooo! Kumbukeni kwa kauli yenu wenyewe kuna kura milioni 6 !! Msije mkalaumu upnzani kumbe nyie ndiyo mna fujo.
Ni kweli kitendo cha kuwatia kizuizini miaka na miaka bila mashitaka mashehe wa Zanzibar wasiotaka Muungano ni kitendo cha kionevu na kifashisti. Wengine tunakubaliana kabisa na Edward Lowassa, tunalaani na kukemea uwepo wa political prisoners ambao walishatoka magerezani toka JKN anatoka madarakani miaka ya 80.
Lakini katika kutetea mashehe hao, Lowassa amevuka mipaka kwa kiasi cha kutisha. Lowassa ameongelea vurugu na taharuki za siasa za kidini zilizokuwepo enzi za Ally Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, mpaka ikafikia kulazimika kudhibiti hali ile kwa kutumia watu wa usalama na askari wenye mbwa kuingia misikitini kusikiliza mawaidha na kukamata watu. Lowassa anataka misikiti na mashehe radical and firebrand wa enzi zile warudi kwa sababu misikiti siku hizi imekuwa baridi.
Lakini uchochezi wa kijahili na mbaya kuliko wote ambao usingeutegemea kutoka kwa Edward Lowassa ni pale aliposema WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA.
Lugha ya Waislamu ambayo serikali itailewa ni ipi, kujilipua? Muhimu tukumbuke hapa pakiwaka hapa kwa milipuko ya kidini sio wewe wala mimi wala Lowassa wala Magufuli wala polisi wala majeshi yeyote atakaekuwa na hakika ya kubaki salama.
Kwahiyo ktk akili yako lugha nyengine ni kujilipua tu.? Hivi nyie watu wa CCM mbona hamna busara! Mbona mmekaa ki shali shali tu. Hivi kauli ya kuzungumza lugha nyengine na kauli ya tutawashulikia ipi ya uchochezi? Huu ubaguzi mnaoupalilia huu, ohooo! Kumbukeni kwa kauli yenu wenyewe kuna kura milioni 6 !! Msije mkalaumu upnzani kumbe nyie ndiyo mna fujo.
Si Waislamu tu, ningependa Watanzania wote wanaojitambua tuongee lugha ambayo Serikali inaitambua. Maana kwa sasa Majuha yote ya CCM yanaongea lugha ya kumtukuza mtukufu. Hiyo si lugha inayoweza kutuletea maendeleo, maana tumeiongea kwa zaidi ya miaka hamsini, tulichoambulia ni ufukara na udikteta uchwara. Sasa tuseme imetosha.Kuna mambo yanaleta ukakasi.
Mashehe wa Zanzibar walikamatwa wakati wa Rais Kikwete, Lowassa hakusema chochote, na kipindi hicho Tanzania haikuwa na tatizo la Kibiti. Watu zaidi ya 30 wameuwawa katika mazingira ya kutatanisha, halafu anaibuka Lowassa ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu anawakusanya Waislam nyumbani kwake na kuwaambia "WAISLAMU SASA WAANZE KUONGEA LUGHA AMBAYO SERIKALI INAIELEWA". Lowassa anakwenda mbele zaidi na kuwakumbusha namna 'watu walivyotumia dini kuleta machafuko wakati wa Rais Mwinyi.
Maswali ya kujiuliza,
1. Mbali na maagizo aliyotoa hadharani, Lowassa amekuwa anafanya nini nyuma ya pazia?
2. Lowassa anajua nini kuhusu Kibiti?
3. Lowassa ana maana gani anapoagiza waislam waongee 'lugha ambayo serikali inaielewa? Hiyo lugha ikoje?
4. Ni kwanini ametolea mfano wa mchafuko ya kidini wakati wa Mzee Mwinyi?
5. 'Shehe' ambaye amekuwa anafuatana na Lowassa kila mahali (hata leo alikuwa naye) ni kwa ajili ya maombi au ndiye msimamizi mkuu wa 'lugha' ambayo Lowassa anataka waislam waitumie.
Kuna tatizo kubwa.