Video: Makonda sasa amgeukia na kumshambulia Lowassa

Video: Makonda sasa amgeukia na kumshambulia Lowassa

Wadau video hii kwa ambaye hajaiona....kijana Makonda anaonesha confidence ya ajabu...sioni mwisho mzuri wa hawa wawili. Mzee akiamua kujibu itakuwa shida.

[/QUOTEUkiua kwa Upang utakufa kwa upanga, Team Lowasa ndiyo ilitumia magazeti ya Rostam na baadhi ya Redio kumaliza Sumaye eti ana Trioni 9 kwenye mabenki yetu na amechukua ardhi ya wananchi wa dodoma
 
Last edited by a moderator:
Kwa maneno hayo ya Makonda,Lowassa alipaswa afikishwe mahakamani kwa kutoa rushwa,makonda akiwa shahidi namba moja.TAKUKURU ingepaswa ianze taratibu za kumchukulia hatua Lowassa kutokana na tuhumwa zilizosomwa na kiongozi wa siasa kwenye vyombo vya habari.Kukaa kwao kimya ni udhaifu mkubwa katika chama na serikali kwa maana ya takukuru.
 
Jamani wana forum hebu nisaidieni huyu makonda haya maneno kayasema lini ni mwaka huh huu WA Joto LA uchaguzi
 
Makonda ni mhuni lkn wote na lowasa na ni wawakilishi wa magenge ya uhalifu na ujambazi na ufisadi wa kutisha nchini
 
Kwa maneno hayo ya Makonda,Lowassa alipaswa afikishwe mahakamani kwa kutoa rushwa,makonda akiwa shahidi namba moja.TAKUKURU ingepaswa ianze taratibu za kumchukulia hatua Lowassa kutokana na tuhumwa zilizosomwa na kiongozi wa siasa kwenye vyombo vya habari.Kukaa kwao kimya ni udhaifu mkubwa katika chama na serikali kwa maana ya takukuru.


Nakubaliana nawewe 100%. Hakuna nguvu kubwa ya kutafuta ushahidi, kama nikweli kesi ikafunguliwe mahakamani.

Hii kutupa vijembe ni upungufu wa fikra pevu. (UFIPE)
 
Kijana kajikata miguu mwenyewe ktk tasnia ya siasa hawez kusonga mbele...asubir tu amalize kpind hich kidogo kilichobaki
 
Cheki sehemu ya video hii ambayo huyu jamaa Makonda akianza kurusha makombora kwa Lowassa. Inavyoonekana huyu Makonda ni kama midomo ya watu(attack dog) wa watu fulani ambao ndio wanampa kiburi na ubavu hata wa kupambana kwa kiwango cha kutaka kumdhuru mzee wetu Warioba.



Namskitikia makonda kwa sababu wanaomtumia ndani ya ccm hawana ubavu wa kupambana na edo na je ikitokea edo akachukua nchi itakuaje kwa makonda?
 
Last edited by a moderator:
Hebu ngoja niwaite faster hapa wapwa wanhu wasikoswe na jambo hili masikioni mwao
MANI itika tafadhali kama upo zumbemkuu Juzi hukuepo, tafadhali nijibu everlenk hii video inaumiza masikio, watu wanaumizana huku BAK nimekuona asubuhi hata hivyo ulikuwa mpweke sana, sijui kwanini, Yule kijnana wa JKT hajapatikana bado ila Chakaza akiiona hii clip nadhani atapata pa kuanzia

Mpwa asante sana kwa kunistua dah!! inaumiza sana kwa kijana kumshughulikia mzee hii ni laana kwa kweli!!!..... wameamua kulana na kutafunana wao kwa wao hakika machozi ya wengi si bure......Mpwa ila vita vya kunguru......
 
Last edited by a moderator:
Huyo kijana bado hajielewi kwani hayo mambo ni ya ndani ya chama na wote ni wanaccm!!!au ndio mpasuko wa hicho chama?
 
Mpwa jana niliuona uzi kuhusiana na yule kijana wa JKT, baadhi walidai uzi ule ni uzushi na sasa imethibitika kwamba uzi ule ulikuwa kweli tupu. Imenikumbusha sakata la Dr Ulimboka alivyotekwa na hadi kusababisha gazeti la Mwana.Halisi kufungiwa kwa kuandika ushahidi wote kabla na baada ya kutekwa.

Kiongozi wa vijana JKT atekwa, aokotwa - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Hebu ngoja niwaite faster hapa wapwa wanhu wasikoswe na jambo hili masikioni mwao
MANI itika tafadhali kama upo zumbemkuu Juzi hukuepo, tafadhali nijibu everlenk hii video inaumiza masikio, watu wanaumizana huku BAK nimekuona asubuhi hata hivyo ulikuwa mpweke sana, sijui kwanini, Yule kijnana wa JKT hajapatikana bado ila Chakaza akiiona hii clip nadhani atapata pa kuanzia
 
Duuh huyu dogo sijui anajiamini vipi.
 
Back
Top Bottom