Video: Makonda sasa amgeukia na kumshambulia Lowassa

Video: Makonda sasa amgeukia na kumshambulia Lowassa

Tahadhari.. Mods sitaki mhamishe uzi wangu.. Nimeurudisha tena

Habari za asubuhi wana jamvi? Ni matumaini yangu mmeamka salama ili kulijenga taifa.. Ngoja niende moja kwa moja kwenye lililonifanya niandike uzi huu.

Moja kati ya mambo yaliyotushtua wengi ni hili la uteuzi wa wakuu wa wilaya uliofanywa wiki kadhaa zilizopita. Hii ni kutokana na watu walioteuliwa kushika nyadhifa hizo. Mmoja kati ya watu wanaofanya watu waendelee kuhoji uteuzi wake ni pamoja na Mh. Paul Makonda, mkuu mpya wa wilaya ya Kinondoni. Nadhani kila mmoja ana sababu zake kwanini ashtuke juu ya uteuzi wake lakini hilo nawaachia wenyewe.. Mimi niko na hili;

Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia Mh. Mkuu huyu wa wilaya ( Makonda) akimponda na kumuelezea kwa kina ndugu Edward Ngoyae Lowa;sa kuwa ni mtu mwenye nia ya kukivuruga chama huku akiwataja vibaraka wanaotumwa na Lowasa. Aliendelea mbele zaidi na kutaja kuwa Lowasa hana sifa ya kuwa Rais wa nchi, amiri jeshi mkuu wa nchi wala mwenyekiti wa CCM kwakuwa ni mtoaji na mpokeaji RUSHWA..

Sasa nikajiuliza, kwa mfano yaani sasa imetokea Lowasa kawa Rais wa nchi....je Mh. Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda atakimbia nchi? Au Lowasa akipita kura ya maoni atamsafisha? Lakini nikajiuliza tena.. Au ndo kapewa ukuu wa wilaya angalau atengeneze CV na ajipoze kwa kazi aliyofanya maana hatopewa hata uenyekiti wa mtaa baada ya 2015? Nimewaza tu kwa sauti...
 
Kwanini akimbie?katiba inamlinda kila mwananchi,kuwa raisi hakumfanyi huyo raisi afanye anavyotaka,au awafunge watu Tanzania ni nchi ya kidemokrasia,udikteta hauna nafasi katika dunia ya sasa,kama kumpinga raisi ni kosa sijaona sheria inayosema hivyo.
 
Atakimbia nchi kwan lowasa atakuwa ameuziwa nchi ,acha uzembe ,lowasa hatakama atakuwa kiranja ila nchi ni yetu
 
Lowassa atakuwa rais wa wapenda fitina na siyo rais ambaye watanzania wanamtaka.

Tutakuwa taifa la ajabu kuongozwa na mtu kama Lowasa wakati kila mtu anajua kuwa mzee huyu mwizi na fisadi.
 
Kunamawazo ya kijinga sana wakati mwingine hapa tanzania na jf some time.
 
Atakimbia nchi kwan lowasa atakuwa ameuziwa nchi ,acha uzembe ,lowasa hatakama atakuwa kiranja ila nchi ni yetu
Huyu mleta mada anafikiri nchi inaendeshwa kama ambavyo SACCOSS ya CHADEMA inavyoendeshwa. Huyu atakaeingia Ikulu kwa lengo la kuwqnyonga watu atakuwa wa kwanza kukimbia nchi.
 
Back
Top Bottom