VIDEO: Josephine Mushumbusi akihutubia Singida Mjini

VIDEO: Josephine Mushumbusi akihutubia Singida Mjini

Mwanamke anaepita kumkomboa Mtanzania akiwemo mwanamke anashangaza sana anaposema "mwanamme na akili zako timamu huwezi kuvaa T-shirt imeandikwa ari mpya, nguvu mpya na kasi zaidi" kwa sababu itamaanisha kuwa anaona sawa kwa mwanamke na akili timamu kufanya hivyo.

Mwanamke mwenye akili hizi hawezi kuwa mtetezi wala mkombozi wa wanawake wengine, amegubikwa na mfumo dume

Hii ni kweli kabisa. Kama mwanamke anayetaka kuonekana kioo cha jamii anapaswa kuwa makini na matamshi yake. TGNP wakimsikia atakuwa na "kesi ya kujibu".
 
Sehemu ya Waraka wa Juliana Shonza kupinga kitendo cha John Heche kutangaza kumvua uanachama kinyume na taratibu inasoma hivi:

"MADAI YAALIYODAI MH. MBOWE KUWA NI YA KITOTO

Niseme wazi kwamba nimesikitishwamno na madai aliyoyatoa Mwenyekiti wangu wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe kupitiagazeti la Mtanzamia la tarehe 12/01/2013 kwamba madai yangu ni ya kitoto .

Kwanza niweke wazi kabisa kwambanamuheshimu sana Kiongozi wangu huyu mkuu ambaye ndiye alipaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwambahaligawi baraza la Vijana na chama kwa ujumla, ahakikishe kuna utawala borandani ya chama, na utendaji haki, lakini cha kushangaza ameibuka kumtetea Hechekwa hoja za mwegemeo wa upande mmojabila kuangalia maelezo ya upande wa pili.

Niweke wazi kabisa kwamba kaulialiyoitoa dhidi yangu ni yakiushabiki maana kama ni madai yangu kuhusu namna ninavyohujumiwakupitia kwa Katibu Mkuu yeye anayo nakala ya malalamiko [ushahidi upo], lakinihakuna hatua ambayo ameichukua.

Namshangaa Mwenyekiti kudai madaiyangu ni ya kitoto sasa sijui ni madaiyapi anayazungumzia? madai ya kitoto ni yapi? na madai ya kikubwa ni yapi? naje madai ya kitoto ni haya mimi kuhoji kwanini hatuweki akiba kwenye akauntikwa ajili ya uchaguzi 2015 kama tulivyokubaliana kwenye baraza kuu mara baadaya uchaguzi wa 2010.Naombaniwajulishe wanachadema kuwa, nimejitahidi sana kushauri juu ya

1; Uanzishwaji wa chuo chamafunzo ya uongozi kwa makada wa CHADEMA , badala yake ni matumizi mabaya yafedha za ufadhili wa wadau tofauti na hasa mfadhili mkuu ndugu SABODO. Hiiingesaidia pia kulea ki-mfumo wa maadili ya uongozi kwa vijana wa umoja wawanafunzi wa CHADEMA wa vyuo vikuu yani "CHASO" ambapo mimi ni mwasisi wamkakati huu nchini.

2; Chama kwa ujumla kutokuwa na jengo letu na hasa makao makuu yetu. Niaibu kwa chama kikubwa kama CHADEMA kuwa na ofisi tulizopanga na kulipa mamilioni ya fedha za ruzuku na misaada kwa manufaa ya Mwenyekiti Freeman Mbowena Mkurugenzi wa fedha wanaomjua mmiliki wa jengo la makao makuu. Kimsingi mimi natambua chama kina uwezo mkubwa wa kuwa na majengo yetu.

3; Kupunguza mshahara wa katibumkuu Ndugu Dk. Slaa ambao ni zaidi ya milioni saba kwa mwezi na marupurupu kibao ili pesa hizo na mamilioni zielekezwe kujenga chama mikoani kama kweli tunataka2015 tuingie Ikulu.

4; Kuhakikisha pesa zilizochangishwa kwenye M4C zinatumika ipasavyo na si kama zitumikavyo kipindihiki ambapo ni kama tumelewa wingi wa watu kwenye mikutano ya hadhara.

5; Kitendo cha Mwenyekiti wa chama kufumbia macho hatua ya ndugu Slaa (katibu mkuu) kujikopesha pesa ya ruzuku ya watanzania zaidi ya shilingi milioni mia na arobaini.

6; Hatua ya mwenyekiti ndugu Heche kulipwa mshahara na marupurupu hali kanuni za chama haziruhusu huku Mbowe akifumbia macho wakati viongozi wa mikoa na wilaya hawapewi pesa na vifaa vya uenezi.

7; Kitendo cha mchumba wa Dk.Slaa, Josephine Mushumbusi kuzunguka mikoani na kulazimisha kupokelewa kama mke wa mfalme na kuendesha vikao vya ndani na mikutano ya hadhara yenye kulenga kuwajenga wagombea ubunge anaowataka yeye na katibu mkuu kwa mwaka 2015.

Ndugu wanahabari, je hizi ndo hojaza kitoto anazodai Mh. Mbowe? Hivyo basi namtaka Mh. Mbowe sasa asikimbiliekujibu hoja kiushabiki. Ajitahidi kuwa na fikra na Busara ili kukisaidia chama kuvuka kwenye daraja la sasa la pepo kufukuzana. Atambue Baraka anazozitoa wanachama wafukuzwe hovyo na kunyanyaswa ni hatari kwa kuwa anaandaa kundi kubwa nje ambalo litageuka mwiba siku za usoni. "
 
Wanakoelekea CDM ni pagumu sana ukizingatia CCM wamejirekebisha sana kiasi cha kuwaaminisha wananchi kwamba wako makini kuliko CDM. kwa kweli kama CCM wataendelea kuwa wasikivu na wachapakazi hivi sijui CDM watatumia turufu gani 2015.

JUST IMAGINE MAGUFULI AU MWAKYEMBE NDIO MGOMBEA WA CCM 2015 unafikiri watu wengi watampigia nani?

CCM kujirekebisha? This will never happen unless they are out of power !!!!!!
 
hivi jamani huyo mnaemuita babu si alimkuta huyu bibie akiwa kwenye harakati za kulikomboa hili taifa?? mlitaka alivyoolewa na Dr. aache harakati au?
 
Tatizo siyo kuhutubia mkuu. Ugomvi wetu ni mambo mawili. Kwanza kutumia pesa za chama kwa maslahi binafsi kwa sababu anachokifanya siyo kazi ya chama ila ni kazi ya kujenga mtandao wake, pili ni kuabuse power kwa kupokelewa kama kiongozi wa kitaifa bila kuheshimu protocol.

umekazana mitandao mitandao, hivi huwezi kufikiri zaidi ya hapo?
 
hivi jamani huyo mnaemuita babu si alimkuta huyu bibie akiwa kwenye harakati za kulikomboa hili taifa?? mlitaka alivyoolewa na Dr. aache harakati au?

Acha kupotosha makusudi Dr Slaa ajamuoa...alikuwa chama gani zamani.
 
Kwa hiyo mnaiga yale ccm wanayofanya.Halafu mama salma mke halali wa rais
wapi mkuu imeandikwa kwamba mke halali wa rais apigiwe saluti na kusomewa taarifa za maendeleo ya mikoa na wilaya na wakuu wa mikoa na wilaya? Haya ni matumizi hovyo ya raslimali na cheo cha urais!
 
Tunajadili mustakabali wa taifa hili nyie magamba kwa kukosa kazi mnatuletea humu mambo ya kipuuzi
 
kwani Salma Kikwete ana madaraka gan katika nchi....

mary mary, Kwa hiyo ndio J.Mushumbusi nae anaiga sio? Basi msikimbilie kulalama na kuwaka bango humu mnapomuona mama First Lady akipigiwa saluti airport na nyie subiri Mushumbusi aje!
 
Last edited by a moderator:
Wivu tuu mwambieni yule wa bosi wenu athubutu kusimama jukwaani kama anaweza ongea bila karatasi ya kuandikiwa na kuhesabu herufi. Ndani ya CHADEMA kila mmoja ni jembe.
 
Back
Top Bottom