PreGE2025 Kiria Ormemei aandika barua kutia nia jimbo la Simanjiro

PreGE2025 Kiria Ormemei aandika barua kutia nia jimbo la Simanjiro

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
472
Reaction score
581
Katika video aliyopakia mtandao wa TikTok tarehe 1 Juni 2025, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Kiria Ormemei Laizer, ameonekana akizungumza katika ibada ya Jumapili, akitangaza rasmi nia yake ya kuwania ubunge wa Jimbo la Simanjiro kupitia chama hicho cha Mapinduzi.

Kiria Ormemei amefafanua kuwa anaandika barua rasmi ya kuomba nafasi hiyo, jambo linaloashiria kuachia ngazi ya uenyekiti wa wilaya na kuingia rasmi katika mchakato wa kugombea ubunge.

Hatua hii ni utekelezaji wa maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye alitoa onyo kwa viongozi wote wa chama wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali kuwasilisha majina yao kabla ya Juni 1, ili kuharakisha mchakato wa wazi na huru wa kuchagua wagombea.
 
Back
Top Bottom