VIDEO: CCM wananitishia maisha - Rev. Munishi

VIDEO: CCM wananitishia maisha - Rev. Munishi

Status
Not open for further replies.
MCHUNGAJI ...acha kuchanganya dini na siasa...
Si umeona UAMSHO walivyochanganya dini na siasa
 
Hahaha...
Nimeangalia Clip nimcheka mpaka basi...

Katika Jina la yesu Kikwete ondoa usalama wa Taifa...
Katika jina la yesu Kikwete shetani shindwa....

Katika jina la yesu mungu....(Mungu mwenyewe baba yake wa kambo fundi seremala)
 
Munishi alikuwa anafanya siasa za kutumiwa badala ya kuhubiri injili akaanza kuhubiri siasa za chuki
 
Anatakiwa akamatwe na kuswekwa ndani kwa kosa la kudanganya umma
 
watu wengine bwana kwa kupenda sifa??? yaaani tulikua tushamsahau kabisa kama huyu jamaa yupo, pastor wewe hubiri neno la Mungu tu sidhani kama kutakua na wa kukufuata, ila publicity mbaya wakuu
 
Hii ni Mbaya sana Kwani Kiongozi wa dini hapaswi kuwaeleza watu ukweli. Maandiko matakatifu yanasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa; Maana yake ni kwamba kama una waumini wasiokuwa na maarifa basi wataangamia kwa umasikini unaosababishwa na watawala . Dini ufundisha upendo , haki na usawa ktk jamii, sasa, inakuwaje kosa pale mchungaji anapowaambia watu wake kwamba Watawala wanawaibia na wanawafarakanisha kwa kuwafanya wawe masikini. Nchi iliyobobea kwenye dhuluma, uonevu na umasikini ni Vigumu sana kulieneza neno la Mungu,kwani watu wake wana ugojwa unaohitwa "akrasia" means the weakness of will.Sasa basi mtu wa Mungu mch,MNISI alichokuwa anafanya ni sahihi kwani kuwahubiria neno la Mungu na kuwaaminisha watu wenye njaa si kazi rahisi, hivyo ni vema kuanza kuwapa mwanga/dozi ya kujitambua ni kwa nini wananjaa zisizokoma wakati wamo kwenye taifa linalojinasibu kuwa na Viongozi na serikali Sikivu, taifa lenye utajiri wa kutisha ( dhahabu, Almasi,Tanzaniate... the list goes on and now Mafuta na gesi).
Note: Mungu kwa mtizamo wangu uchukia Masikini na Umasikini, kwa tafasiri ya kawaida ni kwamba Mtu aliye na njaa awapo ibadani iwe ni Msikini au kanisani inaaminika kwamba umwimidi Mungu kwa wasiwasi na inaaminika kwamba mawazo na fikira zake kipindi cha ibada uwa zinawaza mambo tofauti na yazungumzwayo Ibadani.
 
Nata, nahisi hilo jicho lako halioni sawa sawa.... Mchungaji haruhusiwi kuwa mwananchama wa chama cha siasa? Au mchungaji haruhusiwi kuwa mpinzani wa chama cha siasa?

Kwa akili ya NATA ya kimaccm mtumishi wa Mungu hapaswi kuwa mpinzani anapaswa kuwa kwa maccm
 
Last edited by a moderator:
NAdhani limeona hatari ya yeye kushindqna na serikali, kwa kupitia Kelele aende mahakamani Kama anaushahidi wa kutosha. Maana amekaa kihubiri hubiri hapo kukemea ni kidini zaidi aende mahakamani. Hili liko kikalisali zaidi!

Mahakama gani!? hizihizi za ccm!??? thubutu yake,,, Mi mwenzenu baada ya kukosa imani na serikali,polisi na mahakama niliamua kununua uchawi mzito, saivi mambo kwenye mstari, hiyo ndo imekuwa polisi yangu na mahakama yangu, labda mpaka hapo nchi hii itakapopata serikali...
 
Anglia sana maneno yako utakuja kutekwa, kuteswa, kunyofolewa kucha, kuhasiwa na kutolewa jicho na meno.
 
Hivi Munishi kesi yake ya ujambazi iliishaje?
 
Mtumishi wa Mungu Mch Munishi tuko nyuma yako,tuko wengi tumechoka na hawa wauaji,majambazi Kwa jina la Yesu haya mapepo Maccm yameshashindwa na yamelegea na mwisho wa kuyachoma ni 2015 tatuwa huru.Endelea kuwaambia ukweli kwani ukweli na Mungu yu pamoja nawe
 
watu wengine bwana kwa kupenda sifa??? yaaani tulikua tushamsahau kabisa kama huyu jamaa yupo, pastor wewe hubiri neno la Mungu tu sidhani kama kutakua na wa kukufuata, ila publicity mbaya wakuu
Kwa hiyo kama anafuatwa fuatwa akae kimya tu?
 
Kikwete ana maelfu ya majini yanayomlinda aliyorushiwa na Sheikh Yahya. Inabidi mchungaji Munishi ayakemee yote; asibakize hata moja!!
 
Huyu Mchungaji na mwimbaji mashughuri wa nyimbo za injili ni miongoni mwa waliolalamika sana kutishiwa maisha na CCM. Alilalamika sana jinsi CCM itumiavyo dola kumtishia na kuitishia familia yake huko Arusha na Moshi. Kwa sasa huyu mchungaji yuko nchini Kenya akifanya shughuli zake za kidini na uimbaji.

Endelea tu kama hawajakutoa macho!
 
Last edited by a moderator:
watu wengine bwana kwa kupenda sifa??? yaaani tulikua tushamsahau kabisa kama huyu jamaa yupo, pastor wewe hubiri neno la Mungu tu sidhani kama kutakua na wa kukufuata, ila publicity mbaya wakuu
Ulikuwa umemsahau wewe na nani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom