Video: Azimia jukwaani baada ya kutumbuliwa na Makonda

Video: Azimia jukwaani baada ya kutumbuliwa na Makonda

Jamani kwa kweli inaumiza sana ,maana huyu mtu ni baba wa family sijui utajisikiaje kama ndiyo baba yako
 
Mmmmh. Nimejisikia vibaya. Unaweza kuvuta taswira kwamba huyu ni kiongozi, je ana "utu"?
Mtu amezimia halafu unachombeza "Dar oyeeee".
Jamaniiii!!!! Tusijisahau hakuna atakae dumu milele.
Na ni MUNGU gani Makonda unamwabudu? Wewe sio Mkristo.
Dah...hapana kwa kweli.
Na hao wanaoshangilia bila shaka ni misukule.
 
Huu ulevi wa madaraka sasa umepitiliza jamani. Makonda anajisahau kua yeye pia ni binadamu sio mungu. Karma karma karma kwanini humuoni huyu mtu tumechoka kukusubiri[emoji26][emoji26]

Hata kama kuna makosa sio kudhalilishana huku. Kisa cheo tu
 
Utu wa mtu unadhalilishwa kabisa. Binadamu nwenzako amezirai, wewe unashangilia Dar Es Salaam, Magufuli hoyee!! Tupisheni tuchape kazi!!
Na watu wanashangilia k uona mwenzao amebebwa hana fahamu!
 
Hv bashite harogeki
hv uchawi unarogeka
Disturbed.jpg
 
Imeniumiza zaidi ya kuumia kwenyewe, halafu Mzee wa watu amejibu vyema maswali yote, takwimu alizonazo yeye inawezekana hata huyo mkuu wa idara hazijamfikia, niseme tu nimeuzika sana ktk hili. Hekima na busara zituongoze.
 
Aliponichosha jamaa ni pale anapohitaji takwimu za migogoro iliyopo kwa ofisa ardhi kubalance na ile aliyopokea yeye ofisini.

Bila kujiuliza kuwa kwake akialika wenye malalamiko wanaenda hata wale waliowahi kusikilizwa na kupewa maamuzi, na huenda tu Mtu anajaribu tena bahati yake kwa jambo lililowahi kutatuliwa.
 
We unajua hao wakuu wa idara kwa kusababisha migogoro mfano ya ardhi, wameua watu wangap!?
Huyu ana miaka miwili tu ya ukuu wa idara, na kwa taarifa yake, jinsi alivyojipanga, anaonesha alikuwa anaenda sawa na kasi ya Mh. Rais. Kwa miaka miwili hii, watumishi wengi wamejitoa kwa uadilifu ktk kuwatumikia watu ndugu, makosa ya kale yasiwahukumu wengine.
 
Huyu jamaa kweli ni empty kabisa..huku kutafuta sifa kwa watu kutamfanya aue watu...hajui watu wengine wana mapresha,visukari etc....yeye anaona hapo anafanyakazi..
Kama makonda anajiamini anapiga kazi...aruhusu siku moja aende kituo cha tv..then watu waanze kupiga simu kumuuliza maswali yoyote kuhusu DSM tuone kama atachomoa....
 
Safi sana, huwezi kazi, tumbuliwa, zimia, juu yako...
 
Tofautisha kati ya Takwimu na statistics, Takwimu na namba, fani za wengine usiwe unaparamia mkuu
Cheki hili taahira la lumumba linashindwa kuficha aibu ya umbumbumbu wake hadharani....sasa kati ya mimi na wewe nani anaparamia fani za watu...hakuna tofauti kati ya statistics na takwimu...tofauti ni lugha tu statistics kwa kiingereza na takwimu kwa kiswahili but statistics na takwimu vyote vinamaana moja...kwa taarifa yako tu umeparamia vitu usivyovijua kijana bahati mbaya umeingia kwenye mikono ya mtaalamu wa statistics...ki degree changu cha kwanza na cha pili vilikuwa kwenye hiyo field...unajingine jipya????
 
Back
Top Bottom