Victoria Mwanziva: Karibuni banda la Wilaya ya Ludewa kwenye maonesho ya nane nane Mbeya katika viwanja vya Mwakangale

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
NANE NANE MBEYA 2023

KARIBUNI BANDA LA WILAYA YA LUDEWA

Maonyesho ya Kilimo - Nane Nane 2023 yafunguliwa leo tarehe 01.08.2023 katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya ambapo mgeni rasmi wa sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Sunday Deogratias, wamewasili Jijini Mbeya kwaaajili ya kushiriki zoezi la ufunguzi wa maonyesho hayo.

Wamefanya ukaguzi wa mwisho wa Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa- ambalo limekamilika tayari kuwapokea viongozi, wadau wa kilimo na wananchi wote kiujumla kulitembelea banda hili ambalo limejipambanua kwenye;

Maonesho ya bidhaa za Kilimo kwa mifano ya mazao mbalimbali yanayozalishwa Ludewa (Shamba Darasa na Bidhaa zake).
Bustani ya kisasa ya mbogamboga.

Bwawa la Samaki la Kisasa lenye aina mbalimbali ya Samaki wanaofugwa kupitia programu za Ufugaji wa Samaki Wilayani Ludewa- ambapo yupo mfugaji wa Mfano kutokea Wilayani Ludewa.

Kuku ambao wanafugwa Wilayani Ludewa na mfugaji wa Mfano kutokea Wilayani Ludewa.
Bidhaa mbalimbali za Kilimo; Ufugaji, Ujasiriamali kutoka Ludewa.
Muongozo wa Fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Ludewa.

Maonyesho hayo kwa mwaka 2023 yameambatana na kauli mbiu isemayo "Vijana na Wanawake ni msingi imara wa mfumo endelevu wa chakula”.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa anawakaribisha sana kwenye maonyesho haya adhimu ya Nanenane; na zaidi anawakaribisha sana kutembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ili kukutana na wataalam wa Kilimo, Ma-Afisa ugani, wadau wa Kilimo na wajasiriamali kutoka Wilayani Ludewa ili kupata Elimu ya Kilimo, Kuona Shamba Darasa la mazao mbalimbali ya Ludewa, Kuona kizimba cha Samaki- kuona Ufugaji wa Kuku, Ufugaji wa Nyuki na kupata bidhaa mbalimbali za ujasiriamali kutoka Ludewa.
Karibuni kuwekeza Wilayani Ludewa kwenye Sekta ya Kilimo.

#LudewaYetu
 
Huyu DC namuelewa sana.
 
Back
Top Bottom