DC Mwanziva Atembelea Vijana wa Jeshi la AKiba Ludewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa; Victoria Mwanziva; aunga mkono mafunzo ya Vijana wa Jeshi la Akiba Wilayani Ludewa kwa kuwatembelea Kambini na kuwapatia “TrackSuit” sambamba na kuwachangia sare zao za kuhitimu mafunzo.

Matunzo ya Vijana wa Jeshi la Akiba-Wilayani Ludewa kwa mwaka 2023 yanafanyika katika Kata ya Mavanga- na vijana wa Kata ya Mavanga wamepata fursa ya kupata mafunzo ya Jeshi la Akiba.

DC Mwanziva alipozungumza nao; alisisitiza kuwa “Vijana hawa ni wazalendo, wakakamavu na wenye ari na morali ya kujitolea na kuhudumia jamii yao- sisi kama Serikali tunapaswa kuendelea kuwalea, kuwapa morali na motisha katika kipindi chote cha mafunzo yao”
“Tunawashukuru Wakufunzi, wasimamizi na uongozi mzima wa Kata kwa uratibu mzuri wa mafunzo haya”

DC Mwanziva aliambatana na DAS Ludewa Mhe. Sandagila, Sambamba na Kaimu Msimamizi wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Ludewa; Afande Shamte Mkwahe- waliungana na viongozi wa Kata ya Mavanga na wakufunzi katika zoezi hili.

#LudewaYetu #Ludewa

WhatsApp Image 2023-10-19 at 09.14.16.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-19 at 09.14.16(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-19 at 09.14.17.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-19 at 09.14.17(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-19 at 09.14.17(2).jpeg
 
Back
Top Bottom