Uchawi,uchawi,uchawi,uchawi,kila kona .
Hirizi yasitisha kwa muda mwenendo wa kesi Dar
Na Elizabeth Suleyman
HIRIZI iliyorushwa mezani kwa waendesha mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni, jana ilizua mshangao na gumzo huku Hakimu akiwapiga mkwara waliofanya hivyo kwamba hatishwi hata kama wakitupa 10.
Hirizi hiyo iligundika juu ya meza wakati kesi ya kutekwa nyara kwa mtoto wa Kisomali (2) ilipokuwa ikisikilizwa mahakamani hapo jana.
Pamoja na waendesha mashikata mahakamani, meza hiyo pia hutumiwa na mawakili na tukio hilo lilitokea chumba namba tano cha mahakama.
Kitendo cha kukutwa hizi hiyo katika meza ya wakili na waaendesha mashitaka kilionyesha kuwashangaza watu waliokuwa wakisikiliza kesi na wengine kujiuliza mahali ilipotoka hirizi hiyo ambayo ilikuwa imesokotwa kwa kitambaa cheupe na kuzungushiwa kamba nyeupe.
Mara baada ya kuona hirizi hiyo, Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Eliminius Mchauru, alisema kwamba anashangaa katika dunia ya sasa kama kuna watu ambao wanaamini hirizi.
"Wale wote wanaoamini mambo ya hirizi mpaka sasa hivi, haya ni mambo ya kizamani, kama hali hii itaendelea wanao uwezo wa kurusha hata hirizi kumi kwa jinsi wanavyotaka. Hirizi haziwezi kututisha sisi tutaendelea na kazi," alisema.
Naye mwendesha mashitaka katika kesi hiyo, Isaya Mwanga, alisema kwamba kitendo cha watu kurusha hirizi bila kujulikana ilikotokea inasikitisha.
"Wakati nikimuhoji mshitakiwa nikaona hirizi ikiwa mezani, sijui ilitokea wapi, mimi nilishangaa kuona hirizi ikidondoka mezani bila kujua aliyetupa ni nani," alisema.
Hata hivyo, kesi hiyo iliendelea kusikilizwa huku hirizi ikiwa mezani hadi mahakama ilipofungwa jana.
Kesi ya kutekwa nyara kwa mtoto wa Kisomali inayoendeshwa na Hakimu Mchauru, iliendelea kusikilizwa jana katika mahakama hiyo, ambapo shahidi wa sita alitoa ushahidi wake.
Kesi hiyo, inayowakabili washtakiwa wa tano katika utekeji nyara wa mtoto huyo, ina mashahidi 15.
Tuma maoni kwa Mhariri
source.mwananchi.