tanaznia ipo vitani siku nyingi sema mpaka vita vikikaribia ikulu ndio watawala wanashituka, hata wale wa sadam hussein walikuwa wakiimba bado wako salama wakati adui alikuwa sebuleni.
Asiyeamini kwamba vita vimeanza siku nyingi angojee kitanda alicholalia kikichomwa.
Kila mtanzania anamaumivu yake.
Albino wanatolewa sadaka,
wanafunzi wanafukuzwa shule.
Waalimu hawalipwi.
Wagonjwa mahospitali wanakufa kwa kukosa huduma.
Mafisadi wanatia kichefuchefu kila mtu.
Viongozi wako likizo huku wakituzomea na shida zetu.
Kazi hakuna.
Wasomi wanadharauliwa.
Wafanya biashara wazawa wanaoonekana nuksi.
Machinga kilio cha samaki.
Kila kona inahuzunika.
Kikwete kakumbatia washikaji na waliompeleka ikulu na fedha zao.
Wananchi tumekua wasindikizaji na macho ya huruma.
Vita gani tena tunasubiri, tupo vitani, kazi iliyobakia ni kupindua kitanda kila mtu alale chini.