Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali

Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali

Hapo mtu kategwa aseme vyakwangu ili ukabanwe vzr mtego wa panya sijui kma utamnasa simba
 
Ni vya kwangu aisee nipo hapa. Fanyeni fasta mnipe huo mkwanja. Bei ni maelewano.
 
Takukuru kama walishamtaja ni gharama kuunda tume hao wataleta mkanganyiko tu mimi nawaamini sana hawa takukuru wapo vzr
 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda tume ya watu 11 kuchunguza vichwa 15 vya treni ambavyo Rais Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe mwanzoni mwezi Julai, 2017 ili kama vitathibitika kuwa ni vizima serikali ivinunue.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa serikali imekusudia kuvinunua vichwa hivyo vya treni kwa matumizi endapo vitakuwa ni vizima na kama havitakuwa na matatizo yoyote.

Prof. Makame amesema endapo vichwa hivyo vikionekana ni vizima kwa mujibu wa uchunguzi ukaofanywa na tume hiyo ya watu 11 iliyoundwa na serikali hivyo serikali itakaa chini na mmiliki wa vichwa hivyo 15 vya treni na kuzungumza naye biashara.

Mwezi Julai Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam alisema ameviona vichwa vya treni zaidi ya 15 ambavyo kwa muda huo vilikuwa vinaonekana havina mmiliki, na kudai kuwa vichwa hivyo vya treni ni vibovu. Rais aliagiza Wizara husika kulifanyia kazi jambo hilo ili ukweli ufahamike kuhusu vichwa hivcyo 15 vya treni.

Chanzo: EATV

Tukumbuke TAKUKURU waliwahi kumtaja mmiliki wa vichwa hivi, pitia hapa=>
TAKUKURU imemtaja mmiliki wa vichwa vya treni vilivyokutwa Bandarini na rais Magufuli kuwa ni Electro-Motive Diesel


Sasa kama mwenyewe anajulikana inakuwa je wanasema vimetelekezwa?? Nakama havina mwenyewe wanavinunua kutoka kwa nani? Mbona haya ni maajabu ya karne ya 22??
 
Yaan mambo yanayofanya na viongozi wa nchi hii tena wengi wao ambao ni wasomi wakubwa. Wanatufanya wengine tusione hata umuhimu wa kusoma sana kufikia level zao kama upeo wao wa kufikiria ndiyo upo hivi
 
Kama mmiliki hajulikani, biashara itafanyika vipi?

Hapa anavutiwa speed mmiliki akijitokeza tu, akione cha moto...


Cc: mahondaw
 
Ni vema Rais wetu ajifunze utulivu kabla ya kutoa matamko...
 
soku hizi bongo movie wamepitwa kwa mbali sana na politiks movies!maana hizo plot zake very interesting a lot of twist in their story narrations.
politiks movies ina real characters potraying themselves!a power house of characters no movie critic can err them!
 
Back
Top Bottom