Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali

Vichwa 15 vya treni kununuliwa na Serikali

Mwenye vichwa anajulkana,vichwa vina nembo ya TRL.aliyeletewa hvyo vichwa hapa bongo hajulkani.serekali inafanya tathmini ya vichwa hvyo na baada ya kujirithisha tutakaa pamoja na yule aliyeleta vichwa vile tupate win-win situation..am confused..
 
Wanakataa kutupa posho wanatengeneza kamati za kutafuta mwenye mali iliyookotwa.
 
Serikali zote zilizotangulia zilikuwa zinatambua na kuthamini mchango wa wafanyabiashara kwenye kukuza uchumi wa Taifa hili...
Leo hii mfanyabiashara amegeuka kitega uchumi cha serikali, mfanyabiashara amekuwa sio wakala tena wa ukusanyaji kodi bali amekuwa mdaiwa...

Serikali imeua mitaji ya wafanyabiashara kwa kudhani wanawakomoa kumbe wanahatarisha uchumi wa nchi.

LEO hii tunasikia serikali inataka kununua vichwa vya treni vilivyotelekezwa bandarini bila aibu, kodi imekuwa juu, mfanyabiashara anafanya kazi ya kuinufaisha serikali huku yeye akizidi kufilisika.

Mfanyabiashara huyu si Kweli kwamba hajulikani maana kabla havijapakiliwa yalikuwepo makubaliano baina na mwenye Mali na Meli iliyopakia, anajulikana ila serikali inataka kumfilisi makusudi
 
walisema mwenyewe hajulikani leo wanataka kuvinunua kwa mwenyenavyo kiki mpaka 2020
 
Na Tume Mkuu bajeti yake ni bilioni. Boti uozo na vichwa vya treni uozo kwa hisani ya watu wasiojulikana! Only in Tanzania.

Sawa kabisa tusubiri sasa
Muda wote viko hapo mbona mmiliki hajajitokeza
Na sasa tume inaunndwa kumchunguza mtu asiyejulikana ili alipwe
 
Hivi si kwamba vililipiwa awamu iliyopita?,tena wavilipie?,

mzigo hauwezi kuwa delivered bila kuwa umelipiwa
 
Najuta kuzaliwa tz ,hivi vichwa hivina mwenyewe,halafu wataka kununua sasa hapo mazingaombwe au wanataka kipiga hela timu ya nini,nchi gani hii
 
vichwa-jpg.608394



Hebu wataalamu tuelezeni inakuwaje vichwa vikubwa na vizito namna hiyo vinaelea kwenye chombo chenye surface area ndogo hivyo?
 
Ahh amekosea serekali itatoa sadaka kwa mungu aliyevishusha vichwa bandarini utawala huu umebarikiwa
 
hongereniiii kwa kusahau kauli zenu. ...ccm ni jangaaaaaa
 


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunda tume ya watu 11 kuchunguza vichwa 15 vya treni ambavyo Rais Magufuli alivikuta bandarini vikiwa havina mwenyewe mwanzoni mwezi Julai, 2017 ili kama vitathibitika kuwa ni vizima serikali ivinunue.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema kuwa serikali imekusudia kuvinunua vichwa hivyo vya treni kwa matumizi endapo vitakuwa ni vizima na kama havitakuwa na matatizo yoyote.

Prof. Makame amesema endapo vichwa hivyo vikionekana ni vizima kwa mujibu wa uchunguzi ukaofanywa na tume hiyo ya watu 11 iliyoundwa na serikali hivyo serikali itakaa chini na mmiliki wa vichwa hivyo 15 vya treni na kuzungumza naye biashara.

Mwezi Julai Rais Magufuli alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam alisema ameviona vichwa vya treni zaidi ya 15 ambavyo kwa muda huo vilikuwa vinaonekana havina mmiliki, na kudai kuwa vichwa hivyo vya treni ni vibovu. Rais aliagiza Wizara husika kulifanyia kazi jambo hilo ili ukweli ufahamike kuhusu vichwa hivcyo 15 vya treni.

Chanzo: EATV

Tukumbuke TAKUKURU waliwahi kumtaja mmiliki wa vichwa hivi, pitia hapa=>
TAKUKURU imemtaja mmiliki wa vichwa vya treni vilivyokutwa Bandarini na rais Magufuli kuwa ni Electro-Motive Diesel


1) Watavinunua kwa nani na huku walisema havina/hawamjui mmiliki wake??

2) Kama hatukua tumeviagiza means hakukua na uhitaji wake, je watavinunua wavipeleke wapi??

3) Gharama au thamani ya hivyo vichwa ni kubwa, je kuna bajeti yoyote iliyotengwa kwa kazi hiyo??

4) Manunuzi ya serikali ya Ukubwa huo hua yanapitiaga kwanza Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), je huu mchakato umepitia lini huko??
 
Ina bidi wabadili bogie zake kama sio za standard gauge

Mkuu bogi zake ni za metre gauge, na hakuna uwezekano kabisa wa kuzibadili kwenda Standard gauge.

Cha kushangaza ni kwa nini tuvinunue wakati tumeshaanza mradi wa kujenga standard gauge?!

Kama vililetwa kienyeji si wamwagize aliyevileta avirudishe?!
 
Kupanga ni kuchagua, Cha kuokota si chakuiba..

Asiyejulikana atanunua..
 
1- Aliviona vichwa 15 vya treni...[emoji15] [emoji15]
2- Vichwa 15 vya treni havina mwenyewe...[emoji47] [emoji47]
3- Serikali inataka kukaa na mmiliki wa vichwa 15 vya treni kufanya mazungumzo ya biashara....[emoji2] [emoji2]
4- Serikali yaunda tume ili kuchunguza vichwa 15 vya treni....[emoji13] [emoji13]
5- Vichwa 15 vya treni vilivyo kamatwa bandarini ni vibovu...[emoji23] [emoji23]
 
Hahahahahahah lol! Mkuu ni kichekesho hiki tena kikubwa sana. Mali haina mwenyewe halafu wanataka kuinunua! Hizo pesa atalipwa nani? Mniache nainyoosha nchi napambana na ufisadi LOL!
Kipindi cha kampeni alisema kwamba, akipewa ridhaa na watanzania katika kipindi chake hatokua na mambo ya tume
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom