Je kuna kitu ambacho serikali ya Tanzania inaweza kufanya vizuri? Je vitambulisho viko wapi wakati wananchi waliambiwa pesa imeshategwa na zoezi limeongelewa kwa miaka karibu kumi sasa. Pesa ilikuwa imeshategwa kwanani? Kwasababu ya vitambulisho au kwa mafisadi!. Ndiyo maana wengi tunasema kusubiri serikali kufanya vitu hatutaendelea ina bidi tupunguze kazi za serikali na mambo mengine yafanywe na serikali za mitaa au hata kampuni binafsi. Serikali imetumia pesa kujilipa mishahara ya watu wengi kwenye mradi lakini vitambulisho hakuna watasema hile pesa walioweka haipo na wanataka pesa nyingine!!