Viatambulisho Vya Taifa viko wapi tena!! Pesa ilikuwepo vipii!


K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,372
Points
2,000
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,372 2,000
Je kuna kitu ambacho serikali ya Tanzania inaweza kufanya vizuri? Je vitambulisho viko wapi wakati wananchi waliambiwa pesa imeshategwa na zoezi limeongelewa kwa miaka karibu kumi sasa. Pesa ilikuwa imeshategwa kwanani? Kwasababu ya vitambulisho au kwa mafisadi!. Ndiyo maana wengi tunasema kusubiri serikali kufanya vitu hatutaendelea ina bidi tupunguze kazi za serikali na mambo mengine yafanywe na serikali za mitaa au hata kampuni binafsi. Serikali imetumia pesa kujilipa mishahara ya watu wengi kwenye mradi lakini vitambulisho hakuna watasema hile pesa walioweka haipo na wanataka pesa nyingine!!
 
R

raymg

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2012
Messages
844
Points
195
R

raymg

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2012
844 195
Mkuu una hoja....but mchakato wa vitambulisho uliingiwa na uchaguzi wa chama kwa hiyo baadhi ya pesa tuliielekeza huku ili kumnuthru mwenyekiti!
 
M

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
4,944
Points
1,500
M

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
4,944 1,500
Kamundu,

This Tnz"!! mhnnn ...I tell u. kwanza wengi walishasahau kuna ilo Jambo. I lastly heard about it waliposema kuna wapiganaji walikutwa na certificate fake. Since then sijasikia limefikia wapi Wabunge wetu wapo hope they will peak it up. kwanza hongera kulikunbuka hilo.
 
Lokissa

Lokissa

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Messages
7,308
Points
1,500
Lokissa

Lokissa

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2010
7,308 1,500
kamundu hela zilitengwa lakini NIDA hawajapewa kama ilivokusudiwa
tuseme the fund was allocated but never issued
pili tanzania haina infrastructure ya kutumia hivo vitambulisho vyao vya smartcard
ni technolojia ngumu na ngeni, Marekani na Uingereza waliamua kuachana nayo
waliona ni garama sana kuimplement.sasa mataifa tajiri wanasema ni technolojia ngumu na garama
sisi nchi maskini tutaweza wapi?

NIDA wanategemea mkonga waTaifa ukamilike wakati haiujulikani utakamilika lini
Garama za mradi ni kubwa sana kulingana na idadi ya watu.
NIDA washatoa ahadi kem kem za kutoa vitambulisho mwezi wa 4 mwaka huu
hatukuviona
wakasem ni kwa sababu ya ongezeko la vyeti kuwa feki hasa vya wanajeshi
lakini walikiri ukosefu wa fedha

mwitikio wa watu Dar,na Moro haukuwa mkubwa
na pia hata wakusanyaji taarifa nao hawana utaalamu wa data wanazokusanya kutoka kwa watu.
wananchi walishindwa kutofautisha data za sensa na data za vitambulisho

kazi bado kubwa sidhani kama mradi huu utafanikiwa kwa sasa
labda watumie technolojia ingine rahisi
 
M

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
4,944
Points
1,500
M

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
4,944 1,500
Lokisa,

then why there were too much noises from our bunge? watatwambia nini tena juu ya zoezi ili. Ile kamati ya bunge ikiingozwa na ajuza mmoja hivi haikuona mambo hayo uliyoainisha hapo juu? amakweli Tzn inaliwa na wenye akili ndogo huku wenye nazo kubwa wakitazama!
 
gobore

gobore

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2009
Messages
729
Points
195
gobore

gobore

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2009
729 195
Wakuu heshima mbele

Nilikua napita tu ila nimeona si vibaya tukawekana sawa kwenye hili swala na sio kulaumu tu. Tatizo sio mkongo wa taifa wala infrastructure ya smartcard, unayesema hivyo nadhani hujui hivyo vitambulisho vinafanyaje kazi. Kimsingi ni kuwa huo utaratibu ulishaanza katika hatua ya awali ambayo ni ya kutengeneza database kwanza na mikoa ya Dar na Moro(Nadhani Kilombero peke yake) walishaanza kuandikisha na uandikishaji unafuata utraratibu huu

1.Unaandikishwa makazi(Daftari la makazi la mataa limerudishwa kama miaka ile yetu)
2.Baada ya hapo wanachukua taarifa zako nyingine pamoja na supporting information kwa ajili ya verification
3.Then after verification kwenye database nyingine zilizopo tayari wanarudi kuchukua fingerprints
4.Inatengenezwa database ya taifa zima
5.Ndio unapewa kitambulisho(Kikadi) kwahiyo ishu ya muhimu sio kile kikadi bali ni taarifa za ujumla za muombaji na hii inachukua muda kuthibitisha

Kwa mkoa wa Dsm watu waliandikishwa kwa hatua ya kwanza walikua 7m kwa kupita kwenye makazi ila katika hatua ya pili kwasababbu ya mapuuza ya waTanzania kama kawaida yetu walikwenda watu millioni 2 tu mpaka muda ulipokwisha.

Muda utaongezwa tena ila kwa sasa walisimamisha kupisha zoezi la sensa kwakua NIDA nao ni washiriki na baadhi ya data zitatumika.

Muda sio mrefu uandikishaji utaendelea Dar kwa wale waliokosa
Lokissa nimejaribu kuelezea kwa kifupi hapo na teknolojia ya smartcard inayoongelewa sio complicated ni kama lesseni mpya za magari tu zilivyo. Ishu ni registration yani kwenye jina pamoja na fingerprints.Nadhani kama ni mfanyabiashara utakua umegundua lesseni mpya za biashara kuandikisha ni mpaka uweke fingerprints pia hiyo ni sehemu ya huu mradi wa NIDA pia. Logic ni kuwa na uwezo wa kuonganisha idara hizi kwa pamoja..TRA,,NEC,NECTA,NACTE,Immigration, Bureau of Statistics pamoja na wale wazee wa mitaa/wanaitwa wenyeviti nadhani na hiyo database ndio itakua controled na NIDA kwahiyo ni mradi mkubwa kuliko watu wengi wanavyofikiri na wanakomaa na Dar wakifanikiwa hapo wanajua watafanikiwa Tz nzima
 
Last edited by a moderator:
washa

washa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2007
Messages
619
Points
500
washa

washa

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2007
619 500
Wakuu, mimi ninahisi kunakitu chanya kinaendelea kwa sasa baada ya ukimya wa muda mrefu hawa jamaa wa RITA wamekuja na mitambo yao ya teknolojia ya juu, wametupiga picha, kuchukua alama za vidole na kuhakiki taarifa binafsi.
Hata kama kulikuwa na matatizo hapo awali, lakini sasa mambo yanaonekana
 
B

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
9,744
Points
0
B

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
9,744 0
Je kuna kitu ambacho serikali ya Tanzania inaweza kufanya vizuri? Je vitambulisho viko wapi wakati wananchi waliambiwa pesa imeshategwa na zoezi limeongelewa kwa miaka karibu kumi sasa. Pesa ilikuwa imeshategwa kwanani? Kwasababu ya vitambulisho au kwa mafisadi!. Ndiyo maana wengi tunasema kusubiri serikali kufanya vitu hatutaendelea ina bidi tupunguze kazi za serikali na mambo mengine yafanywe na serikali za mitaa au hata kampuni binafsi. Serikali imetumia pesa kujilipa mishahara ya watu wengi kwenye mradi lakini vitambulisho hakuna watasema hile pesa walioweka haipo na wanataka pesa nyingine!!

Kamundu me naulizia abt VAZI LA TAIFA
 
Last edited by a moderator:
B

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
9,744
Points
0
B

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
9,744 0
Wakuu, mimi ninahisi kunakitu chanya kinaendelea kwa sasa baada ya ukimya wa muda mrefu hawa jamaa wa RITA wamekuja na mitambo yao ya teknolojia ya juu, wametupiga picha, kuchukua alama za vidole na kuhakiki taarifa binafsi.
Hata kama kulikuwa na matatizo hapo awali, lakini sasa mambo yanaonekana
rita ni usajili,ufilis uzaz na vifo,vitambulisho NIDA,wanahusianaje hapa?
 
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Messages
5,600
Points
1,195
B

Bangoo

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2011
5,600 1,195
vitambulisho havitakiwi kuwa kama vile vyakupigia kura ambavyo hata wafuasi wauamsho na all shaabab wanavyo na siyo raia
 
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,372
Points
2,000
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,372 2,000
Mimi kama nakumbuka tuliambiwa pesa imeshategwa, research zote zimeshafanywa na zoezi limeanza baada ya maandalizi ya muda mrefu sana. Sasa haya matatizo tunayosema yanatoka wapi wakati mikakati yote ilishamalizika? Sasa jamani tukisema tunachukizwa na serikali hapa tutaambiwa mambo ya siasa. Mimi naona swala kama hili ni muhimu sana kwa taifa lakini nashangaa serikali haijali kabisa na inawezekana zile pesa walizosema wamezitenga hazipo kwani Watanzania wengi viongozi hawana uzalendo kabisa.
 
Ebebe

Ebebe

Member
Joined
Nov 20, 2012
Messages
12
Points
0
Ebebe

Ebebe

Member
Joined Nov 20, 2012
12 0
mh bora umelionge mdau make mimi nilienda na kichanga cha wiki naambiwa nisipojiandikisha mda unaisha hawaandikishi tena!ila sishangai hiyo ndo serikali yetu.
 
commited

commited

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,617
Points
1,195
Age
28
commited

commited

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,617 1,195
mada ngumu na makini kwa faida ya watanzania woote kama hii huwezi waona vijana wa lumumba au mashabiki wa ponda wanaweka neno hapa, wanachungulia kwa mbali kutafuta thread za cdm tu na udini full stop.
 
Lokissa

Lokissa

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2010
Messages
7,308
Points
1,500
Lokissa

Lokissa

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2010
7,308 1,500
well said Gobore
elewa tu au unajua kabisa electronic ID lazima iendane na infrastructure
ambayo kwa sasa inategemea mkonga wa Taifa, na ofisi zote za serikali
zitaunganishwa baada huo mradi kukamilika,kwa sasa haiko hivo

ukisema vitambulisho havitegemi infrasture labda kama ni barcode technology na sio smartcard.
data base haiwezi kufanya kazi kama network infrastructure haijakamilika,
tunaambiwa vitambulisho hivo vitakuwa na biometric information kama fingerprint

ili polisi aweze kujua we ni mgeni au mzawa lazima atumie
biometric reader ambacho kina link na central registry database
sasa bila network monitoring system watasomaje au kujua legal data ID holder?

jiulize kwanini suala la kuwa na vitambulisho lilianza
tangu mwaka 1968 lakini serikali imeshindwa mara zote kutoa
Jiulize kwanini serikali ilikataa kutoa tender kwa National Printer wakaipa
"Iris Corporation Berhad") YA MALAYSIA?

Mradi wa NIDA unahitaji USD Mil 124 kwa sasa serikali ishawapa NIDA sh ngapi kati ya hizo?
kwanini NIDA wameshindwa kutoa vitambulisho hadi leo licha ya kuahidi mara nyingi?
ndugu mradi huu wamekurupuka

Labda
waige ya UK au marekani kuwa lesseni ya gari au kadi ya bima au afya ni kitambulisho halali
cha msingi kila mtanzania apewe number maalumu ya utambulisho ambayo itakuwa inahifadhi data za mtu
mtu akiwa na KADi ya bank au lesseni ya kuendesha gari inatosha cha msingi iwe na number yake maalumu ya usajli
mtoto akizaliwa apewe number maalumu na iwe unique tanzania nzima

hii itasaidia kupunguza garama na fedha.
swali linabaki hiyo data base iko safe kiasi gani?
KAZI NI NDEFU BADO TUONE KAMA MWAKA HUU WATAOA VITAMBULISHO AU MWAKA KESHO
 
B

Bob G

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2011
Messages
2,354
Points
1,195
B

Bob G

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2011
2,354 1,195
naona ilipogundulika maofsa wamechukua majina ya watu wakaona wakiendelea na zoezi watoto wa vigogo wangeumbuka na vyeti bandia
Je kuna kitu ambacho
serikali ya Tanzania inaweza kufanya vizuri? Je vitambulisho viko wapi
wakati wananchi waliambiwa pesa imeshategwa na zoezi limeongelewa kwa
miaka karibu kumi sasa. Pesa ilikuwa imeshategwa kwanani? Kwasababu ya
vitambulisho au kwa mafisadi!. Ndiyo maana wengi tunasema kusubiri
serikali kufanya vitu hatutaendelea ina bidi tupunguze kazi za serikali
na mambo mengine yafanywe na serikali za mitaa au hata kampuni binafsi.
Serikali imetumia pesa kujilipa mishahara ya watu wengi kwenye mradi
lakini vitambulisho hakuna watasema hile pesa walioweka haipo na
wanataka pesa nyingine!!
 
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,372
Points
2,000
K

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,372 2,000
Bado nauliza mara ya mweisho serikali ilifanya mradi gani ukafanikiwa bila matatizo. Pesa imeenda wapi tena!!! je wale wanaoshabikia CCM mnasemaje kwenye hili au imekuwa mnachojali ni kuwazuia Chadema wakati issue kama hizi hamsemi chochote.
 
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,478
Points
1,195
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,478 1,195
tanzania ya leo sio kama ile ya zamani.
Labda zoezi hili linasubiri lisainiwe na jk na kuzinduliwa na bilali na kutekelezwa na pinda.
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
13,992
Points
2,000
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2012
13,992 2,000
tanzania ya leo sio kama ile ya zamani.
Labda zoezi hili linasubiri lisainiwe na jk na kuzinduliwa na bilali na kutekelezwa na pinda.

unamaanisha bilali a.k.a mr mkasi??

Wadau wanasema yule jamaa huwa anatembea na mkasi kwenye mfuko wa koti lake maalum kabisa kwa ajili ya kukata kata tepe mbali mbali za ufunguzi na uzinduzi

lokisa,hoja yake imekaa vyema sana
 
tanga kwetu

tanga kwetu

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2010
Messages
2,182
Points
2,000
tanga kwetu

tanga kwetu

JF-Expert Member
Joined May 12, 2010
2,182 2,000
ukichukua baseline data June,2012...ukaendelea na 'mchakato' wako kimyakiya.....utengeneze na ku-issue hizo ID June,2016.....data zako zitakuwa reliable kiasi gani? wangapi watakuwa washakufa? washahama? washahamia? washazaliwa? iwe mvua au jua, serikali imekurupuka??? haijui ifanye nini iache nini??? ili wazee mfisadi lazima m'buni mradi, ndio kama huu!!! mwisho wenu utakuwa m'baya, endeleeni kutetea wizi!!!
 

Forum statistics

Threads 1,284,775
Members 494,236
Posts 30,839,360
Top