Vehicle Tracking System (VTS) ni nini na inafanyaje kazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
1666696418567.png

VTS ni mfumo wa kisatelaiti wa ufuatiliaji mwenendo wa magari barabarani. Mfumo huu unafanana sana na ile mifumo ambayo wengi wameizoea kama Car track au U-truck.

Mfumo huu kwa sasa unatumika hapa Tanzania chini ya usimamizi wa LATRA. Kwa kuanzia mabasi 100 ya njia ya kati Dar-Mwanza, Kahama, Musoma, Kagera yamefungwa mfumo huu.

Jinsi mfumo unavyofanya kazi

Mfumo umepangwa (set) kurekodi spidi kuanzia hadi speed ya mwisho atakayotembea dereva husika. Isipokuwa alarm inalia akifika 85kph.

Hii ina maana kwamba iwapo dereva ataendesha gari kwa mwendo wowote ule kengele(alarm) ya mfumo haitalia, ila atakapozidisha speed 85kph, basi kengele italia kumtahadharisha kuwa sasa anavuka spidi inayokubalika na hivyo ni hatari kwake na kwa maisha ya abiria.

Kwa kutumia mfumo huu mpya Mamlaka ya Usafirishaji (LATRA), Mmiliki, pamoja na Jeshi la Polisi wanaweza kufuatilia mwenendo wa mabasi mchana na usiku.

Iwapo mamlaka inataka kujua dereva wa gari kwa mfano T 000 XXY alikuwa anaendesha spidi gani jana usiku, kinachofanyika ni kwenda kwenye mfumo na kuomba taarifa ya gari hilo.

Mfumo utatoa (retrieve) mwenendo mzima wa gari hilo na speed aliyokuwa anatembea kila mahali huko barabarani ikiwemo wapi alisiamama na kwa muda gani. Taarifa hiyo itatumika kumuadhibu dereva husika.

Aidha, mfumo huu unaruhusu ufuatiliaji wa basi wakati huo huo likiwa safarini (instant tracking). Kwa maana ya kwamba afisa wa LATRA, mmiliki au Jeshi la polisi anaweza kukaa ofisni na kufuatilia kila basi mwenendo wake na hivyo kuweza kuchukua hatua kwa wakati.

IKUMBUKWE

kuwa mfumo haulizuii gari kuvuka speed iliyosetiwa kwenye mfumo, mfano 100 lakini mfumo unahifadhi rekodi ya kila speed dereva aliyotembea njiani.

Hivyo chaguo ni lake dereva, akimbie speed afanye ujanja asikamatwe na tochi mchana, lakini akifika mwisho wa safari au popote pale ataadhibiwa tu kwa taarifa iliyopo kwenye mfumo.

Hivyo, ni jukumu la dereva na kumchunga dereva wake na pia dereva kujichunga yeye mwenyewe ili asikumbane na adhabu za mara kwa mara.
 
View attachment 2397451

Umeeleza vizuri sana vfs sio speed governor
 
Hivyo chaguo ni lake dereva, akimbie speed afanye ujanja asikamatwe na tochi mchana, lakini akifika mwisho wa safari au popote pale ataadhibiwa tu kwa taarifa iliyopo kwenye mfumo.
Wangekuwa wanaadhibiwa Ally's ya Dar - Mwanza na Sauli ta Dar - Mbeys zingeingia Morogoro saa 2:00 asubuhi?
 
Back
Top Bottom