Uzuri wa Mwanamke huwezi kuuona siku ya kwanza, Macho hudanganya.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
UZURI WA MWANAMKE HUWEZI KUUONA SIKU YA KWANZA, MACHO HUDANGANYA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Sisi wanaume kisaikolojia tunapomuona Mwanamke Kwa mara ya Kwanza, macho yetu hutuonyesha kama tumeona kiumbe kizuri. Hii ni Kwa sababu wanaume kiasili katika Akili zetu tumezaliwa tukijua Wanawake ni Wazuri.

Hali hiyo ya uzuri huduma Kwa Siku 90 mpaka 120. Ikiwa unamuona Mwanamke ni mzuri Kwa kiwango kilekile ulichokuona nacho tangu siku ya Kwanza na imezidi miezi mitatu au minne. Basi hapo kuna mambo mawili ambayo ni hakika;

1. Mwanamke huyo ni mzuri Kweli kama unavyomuona.
Zikizidi siku 90 mpaka siku 120 na ukawa bado unamuona huyo Mwanamke ni mzuri basi jua huyo Mwanamke ni mzuri Kweli. Na dalili moja wapo ya uzuri wake utausikia Kwa Ndugu, Rafiki na jamaa. Wakikuambia Mchumba au Mkeo mzuri Sana.

2. Unampenda Sana huyo Mwanamke.
Ukimpenda Sana Mwanamke na hisia zikawa juu Kabisa, basi macho na Akili huwa havifanyi kazi vizuri.
Hisia zikiwa juu Akili huwa Chini. Na Akili ikiwa juu basi hisia huwa Chini.
Mapenzi hupofusha macho kwani Akili inakuwa haifanyi Kazi.
Ukiona Mwanamke unamuona mzuri alafu muda huohuo unasikia Watu wakikuambia sio mzuri basi jua Mwanamke huyo sio mzuri. Hiyo ni dalili namba moja.

Dalili ya pili, ni kuuona ubaya wa Mwanamke wako pale unapokuwa katika uhalisia hasa ukiwa umekasirika au kuchukizwa.
Hata hivyo kuna Ile unamwanamke mzuri alafu hapohapo unampenda. Hapo ni kama upo na Malaika angelica.

Uzuri WA Mwanamke utauona Baada ya mambo yafuatayo;
1. Mazoea naye.
2. Kumjua( kulala naye)
3. Attention ya Watu pindi akipita au akiwa Mbele za Watu.

Kikawaida Sisi wanaume huwaona Wanawake Wazuri wale tusio na mazoea nao. Ndio maana huwaga Taikon nashauri Binti za Tibeli kuwa namna Bora ya kujithamini na kulinda muonekano wao ni kutokuwa na mazoea mazoea na wanaume, Kwa Lugha nyepesi Mwanamke anatakiwa aringe, ajishaue, awe na madoido. Hiyo ndio salama na ulinzi wake ikiwa anataka kuonekana mzuri.

Mwanaume kama Hana mazoea na wewe ni ngumu ku-note ubaya wako ukilinganisha na ukiwa na mazoea naye. Ukiringa kikawaida Watu wataangalia unaringia nini, hivyo wataangalia Yale Majaliwa uliyopewa mathalani, labda Sauti, rangi, Elimu, Pesa, au shepu n.k. Kwa nje wanaume tutajifanya tunakuchukia na kukutukana au kukukejeli lakini bado Kwa ndani utakuwa umetuweza na tutakuwa na heshima na kubaki na swali, Kwa nini anajishaua.
Jambo moja la hakika ni kuwa kila Mwanadamu kuna Jambo kajaliwa. Hata kama ni moja hilohilo litakufanya uheshimiwe ikiwa utajua kulitumia.

Lakini ukiwa na mazoea Zoea, Vijana watakusifia huringi lakini wataangalia zaidi negative side ya Kwa nini huringi, hivyo wataona mabaya yako kuliko mazuri yako.

Wanawake wengi wamekuwa wakijiuliza, ni kwanini Baada ya kuwa karibu na Mwanaume Fulani mambo yamebadilika, "mbona hanipi Ile attention aliyokuwa akinipa?" Au ukishampa namba ya simu unakuta akutafuti, au ukishamvulia chupi, hataki kujibu tena SMS wala kukupigia simu.
Kisaikolojia Mwanamke anapokubali mahusiano Baina yake na Mwanaume haya atayataka;
1. Attention, kama ishara ya upendo, kupagawa, kujali, kupepeswa pepeswa.
Wanawake wanapenda kuona na kusikia wanaume wakipagawa na uwepo wao. Na kama wapo mbali basi kuwajulia Hali.

2. Kumsifia.
Yaliyomo yamo yamejaa Hadi pomoni.
Wanawake hawaamini wao NI Wazuri mpaka waambiwe Hilo weka kichwani, pili, wanathibitisha wao ni Wazuri Baada ya kukuvulia nguo na bado ukawasifia yakuwa wao ni Wazuri.
Kwa Mwanamke Sifa ni kitu kikubwa na huwezi mtenga Mwanamke na kumsifu.

Wanawake wanapenda Sifa ya mwisho kuliko Ile ya Kwanza. Ndio maana Kwa Mwanamke wa mwisho ndio anaweza kuwa mshindi.

3. Uhakika, Security.
Ulinzi na uhakika Kwa Mwanamke atautaka Kutoka kwako. Uhakika wa mapenzi yake, furaha yake, Amani yake, na mahitaji yake.
Utamfikisha? utampendezesha? Utamlisha? Utamfanya aishi vizuri?

4. Sanaa
Wanawake watahitaji Sanaa. Hapa nazungumzia Ufundi, ujuzi ulio katika uzuri na wenye kufurahisha.
Je unajua kuongea Lugha Tamu zenye ucheshi?
Je unajua Michezo ya michombezo, kucheza muziki(Wanawake wote 99.9% Duniani wanapenda Muziki. Sanaa ni nguzo muhimu Kwa Mwanamke.

Ukitaka usimchukie Mwanamke basi subiri mpaka jicho lako limzoee. Hapo utajua ni mzuri au sio mzuri. Kisha ndio uamue umuoe.
Lakini ni kosa kubwa kuoa Mwanamke unayemuona ni mzuri ilhali sio mzuri alafu baadaye jicho lako likitoka tongotongo unaanza kuleta shida.

Taikon kama mwanasaikolojia mbobevu, ninapendekeza mambo haya Kwa Vijana Kwa habari za uzuri wa Wanawake;

1. Usimtongoze Mwanamke Kwa mara ya Kwanza uliyekutana naye Jioni au Usiku, Bar, au Kanksani au kwenye sherehe. Kikawaida hapo utamuona Mwanamke huyo ni mzuri.
Tongoza Mwanamke au tafuta Mwanamke katika mazingira yatakayomuweka katika uhalisia wake zaidi. Hasa majina ya Mchana au akiwa kwenye shughuli za kumtoa jasho, labda kufua, au kupika, au anatembea Mchana kwenye jua.
Au ametoka kulala.

2. Usitafute Mwanamke ukiwa unamhitaji.
Andaa Mpango na upe muda. Mfano, 7YE Plan (Seven Years Eternity Plan), Mpango WA kutafuta MKE mzuri wa kuoa utakaofanyika Kwa miaka Saba. Hii inafaa zaidi Kwa Vijana wadogo ambao wapo chuoni au kidato cha sita, na ambao hawajafika huko basi Vijana walio na miaka 18-27.
Hapo utafuta Kwa utulivu. Lakini sio unatafuta MKE ukiwa unamhitaji, utakwama.
Siku zote, tafuta kitu Wakati hauna uhitaji nacho Kwa Sana(yaani papo hapo). Hii itakupa utulivu.
Na hautakuwa under pressure.

Ukitafuta MKE ukiwa unamhitaji ni rahisi Kupata MKE asiye Sahihi. Ni aidha uone hakuna MKE wa kuoa au uone wake wengi WA kuoa. Aidha uone Wanawake wote ni Wazuri au hakuna Mwanamke hata mmoja aliyemzuri. Hii itakuweka katika mazingira ya kuchagua yeyote.

Ukitafuta ukiwa hauna uhitaji naye WA haraka utawachuja wengi na atajitokeza mmoja ambaye ndiye best choice kwako ambaye hafanani na yeyote na halinganishwi. Ukiwa na muda huwezi chagua yeyote.

Na huwezi kuwa kwenye Ile state ambayo upo kwenye harusi yako alafu muda huohuo unaona ukumbini kuna Wanawake Wazuri mpaka unajuta Kwa nini umewahi kuoa. Hali hiyo huwajia Watu ambao hawakuwa na muda wa kutosha kuchagua na kufanya maamuzi.

Huwezi OA Mwanamke ambaye sio mzuri. Lakini sio kila Mwanamke aliyeolewa ni mzuri. Hapo factors mbili nilizozitaja kule juu zitakuwa constant.

Taikon Acha nipumzike SASA.

Ninawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
UZURI WA MWANAMKE HUWEZI KUUONA SIKU YA KWANZA, MACHO HUDANGANYA.

2. Unampenda Sana huyo Mwanamke.
Ukimpenda Sana Mwanamke na hisia zikawa juu Kabisa, basi macho na Akili huwa havifanyi kazi vizuri.
Hisia zikiwa juu Akili huwa Chini. Na Akili ikiwa juu basi hisia huwa Chini.
Mapenzi hupofusha macho kwani Akili inakuwa haifanyi Kazi.
Ukiona Mwanamke unamuona mzuri alafu muda huohuo unasikia Watu wakikuambia sio mzuri basi jua Mwanamke huyo sio mzuri. Hiyo ni dalili namba moja.
Kwanini usitumie akili kutamani.. ???

I can feel a beauty
I can feel a stupidity
I can smell beauty

Guess what nataka kusema nini...

sometimes kwa uhakika zaidi kutofautisha sukari na chumvi kwa macho ni ngumu, You suppose to taste it.

I Love to Love.
 
FIRST SIGHT NDIO INAKUPA UZURI AU UBAYA WA MWANAMKE

BAADA YA HAPO NI KUTAFUTA VIUNGANISHI TU UMUONE MTU NI MZURI AU MBAYA

First sight haiwezi kukupa uzuri au ubaya wa Mwanamke au MTU. Bali ukaribu na mazoea ndio yatakupa uzuri na Ubaya aa mtu.

Kuna Wanawake wanaonekana ni Wazuri Kabla hujawazoea, lakini siku ukiwazoea unashangaa kuwaona ni wakawaida au Chini ya kawaida.

Na kuna Wanawake wanaonekana ni wakawaida au Chini ya kawaida lakini siku ukizoeeana NAO ndio unakuja kuona uzuri wao.

Haya mambo mwanaume yeyote ambaye ametembea na Wanawake tofauti tofauti mpaka wa kimataifa atakuambia vivihivi.
 
Kwanini usitumie akili kutamani.. ???

I can feel a beauty
I can feel a stupidity
I can smell beauty

Guess what nataka kusema nini...

sometimes kwa uhakika zaidi kutofautisha sukari na chumvi kwa macho ni ngumu, You suppose to test it.

I Love to Love.

Hiyo ya Kutumia akili katika mapenzi wengi inawashinda ndio maana inahitaji maelezo marefu kufafanua mambo haya.

Watu wengi wanajua uzuri upo machoni ilhali uzuri upo akilini(ubongoni), macho yanaweza kuona kitu ni kizuri lakini Akili ikaona tofauti
 
Binafsi mwanamke namwona mzuri pale ninapozungumza nae , kauli zake tu na jinsi anavyo itikia mazungumzo yetu naweza mwona mzuri hata kama kwenye macho ya wengi kisura na kiumbo anaonekana mbaya , pia naweza mwona ni m baya kwenye mazungumzo yetu hata kama kwenye macho ya watu ni mzuri kisura na kiumbo.
 
Binafsi mwanamke namwona mzuri pale ninapozungumza nae , kauli zake tu na jinsi anavyo itikia mazungumzo yetu naweza mwona mzuri hata kama kwenye macho ya wengi kisura na kiumbo anaonekana mbaya , pia naweza mwona ni m baya kwenye mazungumzo yetu hata kama kwenye macho ya watu ni mzuri kisura na kiumbo.

Ni sahihi Kabisa
 
Back
Top Bottom