Uzuri/urembo/utanashati. Vs Jamii



Genuinely NK was waiting for you kuona ni kibomu gani utaleta.... Hujani disappoint!!

Hio technique hata mimi hutumia saana, hasa maofisini humu.... it works wonders... Nakumbuka
wakati mdogo niko form two - babangu alikua ananipeleka shule, tukasimamishwa na Traffic njiani
wa kike (i will never forget yaaani...lol..) Yule dada akamwambia my dad kua mbona gari haina taa
za mbele - (ilikua gari zile za taa ambazo ukitaka kuwasha lazima uzi switch....) bahati mbaya mkoani
huko, alikua bado hayuko exposed kwa aina hizo za gari.... Baba akamsemesha Kiingereza akawasha
na zile taa - Yule dada aliishia kuomba lifti..... it was so funny kwa wakati huo... but in reality ni aibu...
 
"Annadhafa Minnal Imaan" Unadhifu uko kwenye imani.

Hapa ndio penyewe haswa. Ikiwa yeyote hana imani unadhifu atautoa wapi? Iwe anahudumia au anahudumiwa. Iwe tajiri au maskini. Ni wapi maskini anatakiwa asiwe nadhifu? Hakuna.

Unadhifu wa kwanza ni wa moyo au roho, kama hauna huo, unaweza kuwa nadhifu wa nguo lakini roho yako isiwe nadhifu na hiyo itajionesha na kujitokeza katika uso wako, au mdomo wako, au mwendo wako.

Kwanza tuwe nadhifu kwenye nyoyo na roho zetu na mengine yatafatia.

Kweli, unadhifu ni imani.
 

..........Hapo kwenye nyekundu kumenikumbusha mbali sana, kazi yangu ya kwanza niliipata baada ya kumaliza form 6...........hata CV nilikuwa sina tena ni kazi ya kimataifa. Basi nikapewa ushauri jinsi ya kuvaa kwenye interview.........nikaambiwa kwa kuwa una umri mdogo hapo nilikuwa na 19 basi natakiwa kuvaa kiafrica zaidi ili nionekane nipo serious.

Sasa basi hata nguo ya kitenge nilikuwa sina..........ikabidi nikaazima nguo ya mama, nikavaa kiafrica na kiremba juu mtoto wa kike. Nilikutana na watu wengi wamevaa suti, u know what?? Kati ya wanawake tuliokuwepo pale mimi nilipata ile kazi japokuwa umri ulikuwa mdogo.
 


Asalam Aleykum Zomba...

Naona umetupatia darasa kidogo hapa... appreciated, na noted kabisa...
Na nakubaliana nawe kua Unadhifu ni Imani, maana ukiwa na imani kali ina
maana hata nguo nazo zitakua ni za heshima i guess.... Asante bana....
 



Hili suala la vitenge hili wewe ni third person na pata direct testimony..... I believe it

is something inatakiwa iwe seriously considered by most hasa wanaotafuta kazi...

Maana kumaliza form six with no CV and then upate kazi sio lelemama bana...

Really Impressive.... Thank you Pretty....
 
AishaDii
Thank you for this very, very useful thread
Kusema ukweli umegusia jambo zuri sana, hasa ulivyotoa mifano ya hao wabunge wawili. Mh kwa kweli inasikitisha. Nitachangia kidogo tu maana Tanesco wameniazima nusu umeme!! sitaki deni mie!

Uzuri:
- Katika hili kusema ukweli nadhani kuna makosa yanayofanyika kwa kumpatia mtu upendeleo kwa kigezo hikli (Na ni kweli inafanyioka sana tu na mfano mzuri ni hao wabunge). Yaani kwa kuangalia uzuri wa mtu tu basi unambebesha na sifa nyingine asokuwa nazo!! Hii inatucost sana kimaendeleo. Lakini pamoja na hayo labda ningependa kujua definition tuliyoitumia ya Uzuri......kama ni ule wa asili (sijui ndo sawa na urembo?!) ambao mtu hauchakachui, kama ni mzuri, ni mzuri tu.....apale matope au poda ni mzuri. Haijalishi kama kichwani ni safi au la sehemu nyingine za kazi, huduma atapata huduma,kazi kisa ni mzuri (Hii kwangu imekaa kinyanyasaji nyanyasaji vile- mtu anakuthamini wewe kwa uzuri wa sura!!)

- lakini kwa upande mwingine uzuri wako unawezakukunyima wewe kitu, huduma au kazi nzuri! au ikakunyima wewe mzuri kufulfill adhima yako ya maisha!! Mfano ushasema wasichana wazuri wanakuwa wabunge- no one will believe kuwa umeteuliwa kiuwezo (kama ni wa kuteuliwa) au kama ni oficn umepandishwa cheo kiuwezo (unless kuna achievements zinazoonekana kutokana na uwezo wako). wengi watahisi uzuri ndio umekuweka hapo ulipo. Hii mara nyingi unawezajikuta unaghairi (kama nia yako ilikuwa ni kuwa mbunge- kama huwezigombea) basi hata kwenye siasa utaogopa kuingia ili kuepusha ikitokea umeteuliwa watu watasema ni uzuri!!!

Utanashati: Hili sina experience nalo inakuwaje hasa, yaani unapata huduma, kazi, kiupendeleo kwa kuwa u'mtanashati au?'

Sometimes nawaoneaga huruma wadogo zetu/wadada walio wazuri......sometimes wanatafsiriwa vibaya.mf. ukimwona mdada mzuri anaendesha gari zuri barabarani, kitu cha kwanza kuja kichwani ni.....c'mon what do you expect kwa msichana mzuri kama yule' implying that lazima kuna pedejee kajipinda!! Au ule usemi wa kina kak wengi wa mwanamke mzuri si wa kuoa! unajitafutia presha tu.....as if mwanamke mzuri hawezi kuwa mke mwema! Mahusiano!! mwe
 


MJ1 Kwanza kabisa nashukuru for the acknowledgement.... Pili nashukuru kwa mchango wako ambao insight yake is deep and very informative... Pia nikupie pole na umeme - Kilio cha woote, ingawa ni wazi wengine ni walau japo hata hio kidogo....

Uzuri ni kama the way umedefine hapo juu... ambao katika jamii kwa kweli ni wachache mno... mtu mzuri akiongeza na urembo, kaka/baba zetu hishia kumsifia mzuri kama Malaika, au nasie akina dada kaka/baba akiwa hivo huishia kumwagia masifa kedekede... However katika jamii yetu hasa mijini wadada wazuri pia na wakaka wamekua wengi mno! Haijalishi kua wamenunua huo urembo, But end result ni kua wana mvuto na unatamani uendelee kuwaangalia tu... Hivo hapo kwenye purple hapo nakuunga mkono kabisa!!!



Hii paragraph above hasa nilipo bold, observe saana... Wadada (afadhali wakaka...) ambao since ni watoto wanasifiwa saana kua they are beautiful they tend to bweteka a lot.... mengi yanafanywa out of obligation... kwenda shule/college/University and the like.... yaani hawi Hardworking for ana experience ilo kua nurtured toka utoto wa kupendelewa na kuonewa huruma.... Ni heri binti ambae alikua wa kawaida then kaja kua mzuri ukubwani via urembo of course.... HOWEVER Ukipata binti ambae yuko very bright na intelligent and she is super beautiful- She goes places na anakua achiever ile mbaya!!


Kuhusu utanashati... ina apply saana kwa wakaka for them hatuwezi waita Warembo... Si unajua ile type of a guy he is not handsome but mvuto wake mkubwa is a result ya utanashati alonao....lol... En ways... Napenda your last paragraph.... Mdada mzuri yeyote yule huchukuliwa gari kahongwa... (which is very bad - thou in most cases true....) Na kuhusu kuoa.... Kaka yangu anasema hawezi kuja oa a very beautiful lady... anataka tu awe kawaida...

Thank you for such an insightful post....
 

You are quite right AshaDii.
Katika ulimwengu wa impression suala hili haliepukiki.
Lecturer wangu Mjerumani, miaka mingi imepita sasa, aliwahi kusema"The first impression is the deepest".
Ikiwa first impression hailingani na suala unalofukuzia , ni rahisi kutupwa kapuni.
 



Nimependa the quote and it is soo true.... However Lole G, tatizo linakuja pale kua

you have tried your best na unajikuta katika Disadvantage hio... wat do you do??
 
Nimeobserve hili swala kwenye banks nyingi hapa tanzanzania.
Wanaume watanashati, wenye mvuto na tena wakiwa weupe ni an added advantage ya kupata kazi.
Du wewe Rejao, yaani sisi weusi , tena weusi tii kama mimi-mpaka nakaribia weusi wa deep blue, hatuwezi pata kazi benki?
Naweka picha ya GF wangu ambaye vile vile ni blue black-isnt she a beut at first impression?
 
Du wewe Rejao, yaani sisi weusi , tena weusi tii kama mimi-mpaka nakaribia weusi wa deep blue, hatuwezi pata kazi benki?
Naweka picha ya GF wangu ambaye vile vile ni blue black-isnt she a beut at first impression?



Huyu binti.... genuinely speaking..... Dah!... Na hio naturality yake na kipara na

her general uniqueness ndio ilimtanya awe international model... But otherwise... mmmh!!
 
Nimependa the quote and it is soo true.... However Lole G, tatizo linakuja pale kua

you have tried your best na unajikuta katika Disadvantage hio... wat do you do??
Huwa inatokea, na mara nyingi nikiwa blue black imenitokea.
Hii inakuwa stereotype kwa mtu wa upande wa pili, na inaweza kumuumiza yeye mwenyewe akija gundua kuwa alikuwa akifanya a grave mistake.

Nitatoa mfano hai, miaka kadhaa nilienda Mwanza kumrelieve a collegue of mine ambaye alikuwa anahamishwa.Mwenzangu ambaye alikuwa na kitambi kikubwa na mwili mrefu ilibidi anitambulishe ofisi fulani ya waAsia ambayo ingewajibika kwangu.

Bahati mbaya sana I did not make a good impression kwenye ofisi ya hawa jamaa kabla ya introduction-kwa hiyo tulipofika ofisini kwao sikuchngamkiwa wala sikukaribishwa kiti.Kwa vile kiti kilikuwa kimoja out of respect mwenzangu wala hakukaa vile vile.

Baada ya introduction ndio viti vikaletwa tena mbio.
I took note.
Probably it was my problem, I did not act bossy enough and I was black to the teeth!!
Kwa wenzetu mnao wafahamu waAsia, alisikitika sana kufanya kosa hilo, and of course it cost him.
 



Lole G i love your share of experience... really hata ukiangalia comments mbali

mbali za members wengine huko nyuma, imeonekana kabisa ni muhimu saana mtu

kujitambua na kujiweka sawa kutegemea na mazingira na mahala una aim kuenda...

Pamoja na kusema it is not right kumsoma mtu haraka na kum judge hapo hapo

Saa ingine waweza epusha by having/protraying a right look...
 
nijuavyo good looks zinauzika sana...................na ndiyo maana kuna usemi usemao...............chema chajiuza na kibaya chajitembeza....................tatizo letu la mwanaadamu wa kawaida tunapima watu kutokana na maumbile yao............................kama ana mvuto atapewa kipaumbele na baadaye ndipo tabia yake itagundulika..................................we judge according to appearance but not according to the character...................................we are very weak yeah...................................you can say that again and again.......................

yule ambaye ananyanyapaliwa.................................basi afunde mate tu.....kwa sababu ushahidi si rahisi kupatikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…