Uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji Dodoma: Bwana asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo na Asalam Aleikum za nini?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
1,216
2,000
Kuna matangazo mbashara kupitia TBC1.

Ni uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji na usafi wa mazingira kwa mwaka 2019/2020.

Ni tukio zuri. Watendaji wote wa RUWASA kutoka nchi nzima wapo hapa

Nafuatilia.

Tatizo: wengi wanaosimama salamu ni Bwana Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Asalam Aleikum.

Hapana, hizi sio salam za kiserikali.

Tenganisheni salamu za kidini na kazi za serikali.

Serikali inayo misamiati yake.

Dhambi, maombi, maombezi, na maneno kama hayo hapana.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,940
2,000
NI kupoteza muda bure huku wanaotamka hizo salamu ni watenda dhambi hatari sn
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,940
2,000
Job Ndugai atangaza kuandaa Sheria ya Kuacha Kujenga Nyumba MAANA zilizopo zinatosha ikiwa ni pamoja na kujua mapungufu ya nyumba zilizopo labda jamii itajifunza Maisha ya kuishi na Watu pamoja na kujua chimbuko la chuki ambazo zinaburudisha jamii yetu kila siku...
Kazi ipo
 
ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
9,677
2,000
Mkuu naomba uendelee kuweka updates maana Mimi Ni mdau mkuu wa sekta ya maji
 
Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
496
1,000
Hoja yako hapa ni nini? Hizo salam au uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa mamlaka ya maji? Kama hoja ni salam mi sioni tatizo kwan pamoja na kuwa serikali haina dini lkn watumishi wa serikali na wananchi wa kawaida wengi wana dini. Kwahiyo ikitolewa salam aleikum hiyo inakuwa kwa niaba ya waislam wataitika, ikitolewa bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu kristo pia wakristo wataitika, na mwisho ni salam ya wale wasiokuwa na dini na hata wenye dini pia ambayo inatamkwa nawasalim kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tanzania kama Taifa kuna mambo mengi ya msingi ya kulalamikia kama vile kuiomba serikalj iboreshe mfumo wetu wa elimu, kuiomba serikali isambaze maji safi nchi nzima bila kusahau na umeme, watumishi au wafanyakazi kazi kuongezwa mishahara, kuongeza ajira serikalini na kuangalia njia nzuri ya kupunguza umasikini nk. Sio kutumia muda mwingi mtandaoni kulalamikia salam ambayo haiwezi kukuongezea wala kukupunguzia chochote.
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
5,870
2,000
Kuna matangazo mbashara kupitia TBC1.

Ni uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji na usafi wa mazingira kwa mwaka 2019/2020.

Ni tukio zuri. Watendaji wote wa RUWASA kutoka nchi nzima wapo hapa

Nafuatilia.

Tatizo: wengi wanaosimama salamu ni Bwana Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Asalam Aleikum.

Hapana, hizi sio salam za kiserikali.

Tenganisheni salamu za kidini na kazi za serikali.

Serikali inayo misamiati yake.

Dhambi, maombi, maombezi, na maneno kama hayo hapana.
Unataka ule ujinga wa "kazi iendeleeee". Kazi gani?
 
Thailand

Member
Nov 15, 2019
83
150
Shetani anaadhibiwa na Mungu kisa wivu Mungu Mwenye Enzi kupewa sifa. Acha Mungu asifiwe toka kwenye kundi la mpinga Mwenyezi Mungu
 
Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
1,502
2,000
Kuna matangazo mbashara kupitia TBC1.

Ni uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa mamlaka za maji na usafi wa mazingira kwa mwaka 2019/2020.

Ni tukio zuri. Watendaji wote wa RUWASA kutoka nchi nzima wapo hapa

Nafuatilia.

Tatizo: wengi wanaosimama salamu ni Bwana Asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Asalam Aleikum.

Hapana, hizi sio salam za kiserikali.

Tenganisheni salamu za kidini na kazi za serikali.

Serikali inayo misamiati yake.

Dhambi, maombi, maombezi, na maneno kama hayo hapana.
Hatujawahi kuwa na spika mjinga na mpumbavu Kama Ndhughai
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,886
2,000
Hivi watu wakisalimiana salamu za dini zao msikitini na makanisani haitoshi? Kwa nini mnalazimisha kuleta mambo ya kidini katika shughuli za serikali? Faida yake ni ipi hasa??
Hoja yako hapa ni nini? Hizo salam au uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa mamlaka ya maji? Kama hoja ni salam mi sioni tatizo kwan pamoja na kuwa serikali haina dini lkn watumishi wa serikali na wananchi wa kawaida wengi wana dini. Kwahiyo ikitolewa salam aleikum hiyo inakuwa kwa niaba ya waislam wataitika, ikitolewa bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu kristo pia wakristo wataitika, na mwisho ni salam ya wale wasiokuwa na dini na hata wenye dini pia ambayo inatamkwa nawasalim kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Tanzania kama Taifa kuna mambo mengi ya msingi ya kulalamikia kama vile kuiomba serikalj iboreshe mfumo wetu wa elimu, kuiomba serikali isambaze maji safi nchi nzima bila kusahau na umeme, watumishi au wafanyakazi kazi kuongezwa mishahara, kuongeza ajira serikalini na kuangalia njia nzuri ya kupunguza umasikini nk. Sio kutumia muda mwingi mtandaoni kulalamikia salam ambayo haiwezi kukuongezea wala kukupunguzia chochote.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom