Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa HakiElimu: Zaidi ya 80% ya Vijana walioko Shuleni hawajawahi na hawahamasishwi kushiriki mikutano ya Kampeni na Siasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,982
Ripoti ya Utafiti wa Mchango wa Elimu ya Uraia Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia imezinduliwa rasmi Dar es Salaam, leo Alhamisi Septemba 22, 2022

FdPhPJPXEAEbDR8.jpg

Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari akizindua ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchin, hafla hiyo imefanyika leo Septemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam.
Utafiti wa HakiElimu uliozinduliwa, vijana wanatarajia kuwa shule ndio chanzo kikuu kwao cha kujifunza na kujengewa uzoefu wa kushiriki shughuli za kidemokrasia katika ngazi mbalimbali.

Kaimu Mkurugenzi wa Haki Elimu “Waswahili wanasema "Samaki Mkunje angali mbichi" kwa kuzingatia hilo tumeanza kuangalia ushiriki wa vijana wa sekondari nchini katika michakato ya kidemokrasia.”

Dkt. Lyabwene Mtahabwa, mwakilishi wa mgeni rasmi “Demokrasia izingatie samaki mkunje angali mbichi, hongereni kwa kushuka chini katika ngazi ya sekondari niwaombe mshuke pia katika ngazi ya chini zaidi ya msingi na awali hususani miaka 8 ya mwanzo ya mtoto.”

Dkt. Mtahabwa, Kamishna wa Elimu: “Demokrasia ijengwe kwenye msingi wa uzalendo hapo itakua na baraka, amani na mafanikio. Katika mapitio ya mitaala yanayoendelea tumeliingiza suala la uzalendo katika ngazi ya mwanzo kabisa yaani elimu ya awali tunataka watoto wawe wazalendo.
FdPfOySX0AAEET0.jpg

Dkt. Lyabwene Mtahabwa.
Utatifi: Vijana 95.7% wanaamini shule ndio sehemu ya kujifunza demokrasia
Utafiti wa HakiElimu umeonesha kuwa vijana wengi wanaamini shule ndio sehemu sahihi kwao kujifunza na kujengewa uzoefu wa kushiriki shughuli za kidemokrasia katika ngazi mbalimbali.

Waliotoa mtazamo huo ni 95.7% ya waliohojiwa katika Wilaya za Mkuranga, Kilwa, Arusha, Tabora, Ukerewe, Sumbawanga.


Sheria ambazo zinaminya ujifunzaji wa demokrasia
Utafiti umebainisha uwepo wa Sheria ambazo zinaminya ujifunzaji wa demokrasia katika maeneo mengine nje ya shule, katika zama hizi za Utandawazi vijana wengi hususani wa mjini wanategemea sana kushiriki na kujifunza demokrasia kwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Kwa ujumla matokeo ya utafiti huu yanaonesha kutoridhika kwa vijana na katiba na sheria ya uchaguzi ambavyo zinazolazimisha vijana kuanza kupiga kura katika umri wa miaka 18, wamesema hili linachangia katika kuchelewesha vijana kuanza kushiriki katika masuala ya demokrasia.

Vijana hawahamasishwi kushiriki mikutano ya kampeni na siasa
Zaidi ya asilimia 80 ya vijana waliko shuleni hawajawahi na hawahamasishwi kushiriki mikutano ya kampeni na siasa; asilimia 67.8 hawajawahi kuhudhuria mikutano ya Kijiji au mtaa na asilimia 67.5 hawajawahi na hawaoni umuhimu wa wao kushiriki shughuli za kijamii.

Viongozi wa wanafunzi shule za sekondari hawapatikani kidemokrasia
Utafiti pia umeonesha kuwa 47% ya viongozi wa wanafunzi shule za sekondari hawapatikani kwa njia ya chaguzi za kidemokrasia bali kwa kuteuliwa na uongozi wa shule; 11% kwa kujitolea. Ni asilimia 42 pekee ndio ambao hupatikana kwa kufanyika uchaguzi.

Utafiti: Somo la Uraia linapewa muda mchache shuleni
Imebainika kuwa moja ya changamoto ya somo la Uraia katika shule mbalimbali ni muda wa fukundishwa kwa somo hilo, kuwa linatengewa muda mchache tofauti na masomo mengine ndani ya wiki.

Hayo yamebainika katika Ripoti ya Utafiti wa Mchango wa Elimu ya Uraia Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia ya Haki Elimu.


Ripoti: Wanafunzi hawana demokrasia ya kuchagua viongozi wao
Utafiti wa Haki Elimu umebaini kati ya changamoto za Kidemokrasia zilizopo katika baadhi ya shule Nchini ni wanafunzi kutokuwa na uhuru wa kutosha kuchagua viongozi wao.

Utafiti huo umeonesha Walimu wengi wanashiriki katika kuchagua viongozi wa wanafunzi shuleni ili wafuate matakwa yao na siyo ya wenzao wanaowaongoza.

Vijana hawashirikishwi
44.4% ya wanafunzi wa Sekondari hawaelewi maana ya demokrasia, huku asilimia 85.5 hawajawahi kushiriki, kushirikishwa katika vikao rasmi vya shule vinavyofanya uamuzi.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 22 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu HakiElimu, Godfrey Boniventure katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa Elimu ya Uraia Shule za Sekondari na ushiriki wa vijana katika michakato ya kidemokrasia nchini.

Amesema utafiti huo umebaini kuwa asilimia 68.9 ya wanafunzi hawajawahi kugombea au kuonesha nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ngazi ya shule, huku asilimia 44 hawashiriki katika chaguzi za uongozi wa wanafunzi.

“Asilimia 26 hawajawahi kushiriki kabisa katika midahalo na mijadala ya hoja kama sehemu ya kuwajengea uwezo wa ushawishi na demokrasia,” amesema Boniventure.

Amesema utafiti huo, uliofanyika katika Wilaya za Mkuranga, Tabora, Ukerewe, Kilwa, Sumbawanga na Arusha, unaonesha ushiriki hafifu wa vijana katika mifumo ya kidemokrasia ndani na nje ya shule unachangiwa na upungufu katika mtaala wa elimu ya uraia itolewayo shule za sekondari.
 

Attachments

  • Youth Engagement in Learning and Democratic Processes in Tanzania - Copy.pdf
    1.9 MB · Views: 3
Hizi siasa za mashuleni huwa naona zina manufaa na hasara pia, sio vibaya kijana akitimiza miaka kumi na nane ndio aanze kuhusishwa na siasa, lakini chini ya hapo, naona ni kumvuruga akili.

Kusema watoto wa miaka kuanzia minane waanze kuhusishwa na mambo ya siasa, kwangu naona ni utani, huyu anaelewa nini kuhusu sera za vyama watakazopelekewa kunadiwa kwao, kwanza hata hawaruhusiwi kupiga kura.

Hata hao wa miaka kumi na nane, kwangu napendekeza waachwe kuwa huru, wakitaka kushiriki hiyo mikutano ya siasa waende, wasiotaka wasiende, badala yake somo la uraia ndio lipewe kipaumbele mashuleni.

Kwanza kwa hizi siasa zetu za kurithishana kifamilia, kuwasumbua hao watoto badala ya kuwaacha wawekeze kwenye elimu yakuwakomboa wao na familia zao, naona ni dhambi.
 
Iko ivyo na ndo ukweli wenyewe utahudhuria vipi mkutano wa adhara wakati magari ya washawasha na mabomu yametanda kila kona siku iyo hata mgambo wanakua polisi wanatanda kila kona nani aende haka mie bado nasoma
 
Iko ivyo na ndo ukweli wenyewe utahudhuria vipi mkutano wa adhara wakati magari ya washawasha na mabomu yametanda kila kona siku iyo hata mgambo wanakua polisi wanatanda kila kona nani aende haka mie bado nasoma
Nadhani hii ilifanywa makusudi ili kuwadumaza kuhusu maswala ya Siasa
 
Back
Top Bottom