Uzi wa stori za vijiweni

Uzi wa stori za vijiweni

Nakumbuka mwaka 2013 nimeshuka kwenye ndege jijini Mwanza nilienda kikazi. Nilifikia JB Belmont Hotel ya Mwanza
Basi yule dereva taxi aliye kuwa ananiendesha akawa ananiambia " Unajua Jb Belmonte Ni ya Mkapa Na Kikwete ?

Ile J ni Jakaya na B ni Benjamin.

Nililewa bila kunywa
Hahaha,mkuu ukitaka kuenjoy hizi story za vijiweni achana na kutaka kujifanya unauliza source ya taarifa, watakumaind balaa, so chakufanya we sikiliza tu....
 
Naleta moja ya tajiri mmoja aliekuwa anaitwa Rwabizi..huyu jamaa alikuwa ni tajiri kiasi pale bukoba mjini...na alikuwa amefungua miradi kadhaa zikiwemo pub maarufu...utajiri wake aliutoa kwa mganga na alipewa sharti moja tu kwamba maisha yake yoote asijisaidie haja yake ndogo au kubwa chooni....kwa hiyo jamaa kila alipokuwa akibanwa na haja alikuwa akiwasha gari yake na kuelekea porini...sasa siku moja watu walimuona akinya porini kwa hiyo ikawa ndiyo story kwenye kale kamji ka bukoba...ili kuondokana na aibu hii ilibidi jamaa ajiondoe uhai..kwa story za vijiweni inasemekana jamaa walimkuta amejikatakata na viwembe hotelini huku amefariki.....
Hii story nimesikia sana katika viunga vya rwamishenye , kashai na uzunguni that days huko.
 
Tupo zetu kwenye Maandalizi ya Maulidi, pilika pilika za kuchambua Mchele na kuupeta akapita bwana fulani upande tuliokuwepo Wanawake akatoa Salamu ya Bashasha na kwenda zake,

Nikasikia sauti ya Mwanamama mmoja anasema, "Maskini kijana huyu, alikua ana pesa zake na biashara zake chungu nzima akavamiwa na Matapeli wa Rupia za Wajerumani wakamfilisi kila kitu"

Mie mmependa story sasa Ungo wa Mchele nikautua chini, nikauliza kulikoniiiiii,

Nikaambiwa kuna watu wanaamini kua kuna Masanduku ya Wajerumani yana Mali nyingi kama Rupia, Mercury na vitu vya kale kama Taa n.k, ukifanikiwa kupata sanduku moja wewe unakua Bilionea, yaan hao watu wanaojifaraghua huko Masaki, Mbezi beach hadi Mbweni asilimia kubwa Mali walizipata alizoficha Mjerumani,

Watu wanaenda Maporini sehemu zinatisha wanakaa huko miaka kibao wanatumiwa Pesa na ndugu zao tu ila hawarudi wakiamini watafanikiwa kupata sanduku la Mjerumani, Sanduku nalo kulipata si kazi ndogo kuna Kafara, Mizimu, Majini hadi Watumishi wa Mungu wote wanahusika na bado waweza kulipata Serikali ikakukamata na kukunyang'anya pamoja na kesi juu watakayoona inakufaa,

Basi watu wanapoteza Pesa zao wakiamini wanawekeza, watapata zingine zaidi akiwamo huyo Kijana wa Makamo, pasina Ndugu zake kumpigania atoke huko Porini alikua anapotea jumla,

Nyama ikaletwa, msimuliaji akahamia kitengo kingine na story ikaishia hapo.
 
Hizi story zako unamalizia vizuri😆😆😆😆
 
Nimehadithiwa:

Kuna wapemba maeneo ya posta walikuwa safarini ila walikuwa wamebeba hela nyingi sana kwa bahati mbaya zile hela zikaibiwa zimeibiwa vipi mimi sijui nimehadithiwa tu basi wakatangaza wamepoteza hela na aliyeziokota azirudishe.

Basi zikapita siku tatu kimyaa wakatoa week moja nyingine zirudishwe la sivyo watafanya kitu kibaya sana basi week ikapita hazikurudishwa jamaa wakapanda boat wakarudi zanzibar,

wakaenda sehemu moja inaitwa tumbatu huko
Kumbe jamaa waliookota zile hela walikuwa watu wa chamazi wakaenda kujenga nyumba na nyingine kugawa kwa ndugu maana zilikuwa nyingi sana basi unaambiwa wakajenga nyumba wakahamia.

wakahamia wakaanza maisha baada ya kuhamia tu wakaanza kufariki mmoja mmoja kuanzia waliokuwa wanaishi pale nyumbani mpaka ndugu wote waliotumia zile hela yaani arobaini haijafika msiba mwingine unatokea basi nasikia walipona wawili tu mmoja alikuwa nje ya nchi na mwingine alikuwa mkoa mwingine na hiyo nyumba mpaka Leo haikaliki ina mauza mauza nyumba yenyewe inaitwa,

NYUMBA NYEUPE IPO CHAMAZI

Anayeijua hii story ajazie nyama maana mi nimesikia juu juu tu.
Kuhusu mauzauza sijui ila nyumba nyeupe hadi leo ipo ndugu
 
KIJIWE CHA KAHAWA

Siku moja nilienda kutembelea kijiwe kimoja cha kahawa, huko mkoani Kilimanjaro bara bara ya kuelekea mlima kilimanjaro.

Kulikuwa na wazee na vijana wengi wakipata kahawa, huku wakileta stori za hapa na pale, ili mradi kuchangamsha kijiwe, huku tukisikiliza BBC matukio ya dunia. Na kutokana na hali ya hewa, kijiwe kilichangamka.

Mzee mmoja, akasema wajukuu zangu, ‘’nawausia sana, msiwe na tamaa ya pesa, mnaliona lile jengo kubwa pale karibu na mjini, lina historia ndefu.

Waliolijenga hilo jengo ambao ni wamiliki walishatangulia mbele za haki, walikuwa vijana wawili, walienda machimboni na walikuwa marafiki kweli kweli, na wote walikuwa wanatoka kijiji kimoja.

Baada ya kufika huko machimboni, walifanikiwa kupata jiwe lenye thamani kubwa; na baada ya kuliuza walipata hela nyingi, wakaamua kulijenga hilo jengo ili liwe hotel.

Wakalisimamisha hilo jengo kwa haraka sana, pamoja na kuweka mazingira ya nje kwa ajili ya kuvutia wateja.

Kwa bahati mbaya, mmoja kati ya wale wamiliki akaingiwa na roho ya ubinafsi, tamaa, na kutaka kumzidi kete mwenzie. Akamfanyia mwenzie mambo ya ajabu ajabu mpaka umauti ukamfika huko machimboni.

Kwa sababu yule kijana ndio aliyebaki, na ndiye anapafahamu kwa mwenzie ambaye ni marehemu, alitoa taarifa kwao, na akafanya utaratibu wa kusafirisha mwili kwa ajili kuweka msiba. Taratibu za mazishi zikapangwa, na akazikwa.

Lakini wazazi wa yule marehemu wakawa wana maswali mengi kuhusu kifo cha mtoto wao; ndipo wakatoa tamko, tunafanya tambiko kwa yeyote aliyehusika kwa kifo cha mtoto wetu, naye adhurike; wakafanya machinjo ya mifugo pamoja na mila zao.

Haikuchukua wiki, yule kijana akaanza kuvimba tumbo; na hatimaye akaenda kukiri ndiye aliyemsababishia umauti mwenzie, na baada ya hapo naye alifariki.

Ikawa wote wamiliki wa lile jengo wamefariki, na hakuna mmiliki mwingine aliyebaki; lile jengo likawa limetelekezwa kwa miaka mingi, na kwa sababu liko sehemu nzuri kibiashara likawa linawavutia wengi, lakini hawajui waanzie wapi kuja kulipata.

Baadaye kukawa na habari za chini chini mara limetaifishwa n.k’’

Cha kujifunza hapa, 'partnership' kwa sisi waafrika bado, mtaanza vizuri, lakini baadaye mafanikio yakionekana kuna kugeukana, kila mmoja atataka awe boss kwa mwenzie.

Leteni stori za vijiweni wakuu, tupate kujifunza
IMG-20220326-WA0573.jpg
 
Kuna jamaa alikuwa na kakikundi cha u koz men hakuna kalio la mtu wasilolijua kule mwananyamala kisiwani. Akahamia jamaa mkewe anasondomoko balaa wahuni wakamweka radani lazima wal
ikague kalio.
Sasa jamaa ana jicho moja tu moja lilikufa zamani sana,waliposeti mpango siku hiyo mama katoka zake kuoga anajifuta kwa pozi kumbe dirishani kuna watu wanamchora wameshadindi mbaya wanajibweda senema ya bure.sasa wakati wanachungulia kumbe mumewe anarudi kazini mida ya usiku. Kaona jamaa wamejazana dirishani kwake kuchunguza kwa kuvizia akagundua wanamchungulia wifee.
Akaondoka kinyonge akammwondoa wife pale karibu na darubin wahuni nje bila kujua wamehujumiwa wanasema kesho tutaendelea wakiambiana "masela mungu anafinyanga jamani. Tahamaki kesho imefika kumbe jamaa kashaandaa supoku ya besikeli anavizia na akahakikisha wife anajiachia haswa huku yeye kajibanza kikonani kwa dirisha.
Adui chongo akasogea kama ada ile anaseti jicho aone utupu mnono GHAFLA AKASEMA MAZEE WAMEZIMA TAA,TAHAMAKI KIZA KIMEKUJA NA MAUMIVU.MASIKIO YANAMSIKILIZISHA NYAYO ZA WENZIE ZINAKIMBIA. kumbe kilichozimwa ni jicho sio taa.
 
KIJIWE CHA KAHAWA

Miaka zaidi ya 20 imepita, kuna mkandarasi mmoja wa barabara alikuwa anatembea na mke wa mdosi mmoja. Huyo mdosi alikuwa ana hela na madaraka pia.

Kwa kuwa huyo mdosi alikuwa mzee, na mkewe alikuwa bado binti mwenye utamu wake, akawa ameoza kwa mkandarasi aliyekuwa akipata mawe (fedha) kwa ujenzi wa barabara.

Inasemekana mdosi alikuja kupata taarifa kuwa mkandarasi anatoka na mkewe; Bila kujua hili wala lile, mkandarasi kama kawaida yake, kaingia kwenye kijiwe chake cha kahawa na kuanza kunywa zake kahawa .

Ghafla akatokea mtu kama chizi, akamrarua yule mkandarasi na kitu chenye ncha kali, baada ya kuwahishwa hospitali, umauti ukamkuta. Uchunguzi kuendelea, ikaonekana jamaa aliyesababisha kifo, alikuwa chizi.

Mdosi naye alihamishwa kituo cha kazi, na maisha yakaendelea.
Ogopa sana mali za watu, huu usia huwa napewa kila leo na mzee wangu
 
Kuna jamaa alikuwa na kakikundi cha u koz men hakuna kalio la mtu wasilolijua kule mwananyamala kisiwani. Akahamia jamaa mkewe anasondomoko balaa wahuni wakamweka radani lazima wal
ikague kalio.
Sasa jamaa ana jicho moja tu moja lilikufa zamani sana,waliposeti mpango siku hiyo mama katoka zake kuoga anajifuta kwa pozi kumbe dirishani kuna watu wanamchora wameshadindi mbaya wanajibweda senema ya bure.sasa wakati wanachungulia kumbe mumewe anarudi kazini mida ya usiku. Kaona jamaa wamejazana dirishani kwake kuchunguza kwa kuvizia akagundua wanamchungulia wifee.
Akaondoka kinyonge akammwondoa wife pale karibu na darubin wahuni nje bila kujua wamehujumiwa wanasema kesho tutaendelea wakiambiana "masela mungu anafinyanga jamani. Tahamaki kesho imefika kumbe jamaa kashaandaa supoku ya besikeli anavizia na akahakikisha wife anajiachia haswa huku yeye kajibanza kikonani kwa dirisha.
Adui chongo akasogea kama ada ile anaseti jicho aone utupu mnono GHAFLA AKASEMA MAZEE WAMEZIMA TAA,TAHAMAKI KIZA KIMEKUJA NA MAUMIVU.MASIKIO YANAMSIKILIZISHA NYAYO ZA WENZIE ZINAKIMBIA. kumbe kilichozimwa ni jicho sio taa.
Kuna uzi wa Mshana Jr kuhusu vituko vya Mwananyamala naomba ukaweke na hiki aisee 😂😂😂
 
Back
Top Bottom