Uzi wa stori za vijiweni

Uzi wa stori za vijiweni

Nmb wami road Morogoro mjini 2017

Nikiwa kwa fundi viatu saa kumi jioni nikiwa nashona kobazi zangu za kuingia venue kesho asubuhi nilipata story zifuatazo

Stori 1

Bwana pale town Kuna tajiri mmoja ni tajiri kweli ila sasa ana mfanyakazi wake wa mda mrefu sana housigelo na anamlipa hela nzuri tu atawabadilisha wote ila yeye hambadilishi unadhani ni mpenzi wake ? No hapana

Ni hivi jamaa akienda chooni kunya anakunya pembeni yaani pembeni ya sink la choo lile ambalo unachuchumaa kama ni choo cha kukaa yeye hatokikalia atasogea pembeni huku atakunya na mfanyakazi huwa ndio anasafisha

Hizi pesa hizi zina mambo

Nitaendelea na story 2 .....

.
 
Nimehadithiwa:

Kuna wapemba maeneo ya posta walikuwa safarini ila walikuwa wamebeba hela nyingi sana kwa bahati mbaya zile hela zikaibiwa zimeibiwa vipi mimi sijui nimehadithiwa tu basi wakatangaza wamepoteza hela na aliyeziokota azirudishe.

Basi zikapita siku tatu kimyaa wakatoa week moja nyingine zirudishwe la sivyo watafanya kitu kibaya sana basi week ikapita hazikurudishwa jamaa wakapanda boat wakarudi zanzibar,

wakaenda sehemu moja inaitwa tumbatu huko
Kumbe jamaa waliookota zile hela walikuwa watu wa chamazi wakaenda kujenga nyumba na nyingine kugawa kwa ndugu maana zilikuwa nyingi sana basi unaambiwa wakajenga nyumba wakahamia.

wakahamia wakaanza maisha baada ya kuhamia tu wakaanza kufariki mmoja mmoja kuanzia waliokuwa wanaishi pale nyumbani mpaka ndugu wote waliotumia zile hela yaani arobaini haijafika msiba mwingine unatokea basi nasikia walipona wawili tu mmoja alikuwa nje ya nchi na mwingine alikuwa mkoa mwingine na hiyo nyumba mpaka Leo haikaliki ina mauza mauza nyumba yenyewe inaitwa,

NYUMBA NYEUPE IPO CHAMAZI

Anayeijua hii story ajazie nyama maana mi nimesikia juu juu tu.
Kwakua naishi Chamanzi, na Sina mda mrefu huku, nitaulizia juu ya uwepo wa nyumba nyeupe.
 
Naleta moja ya tajiri mmoja aliekuwa anaitwa Rwabizi..huyu jamaa alikuwa ni tajiri kiasi pale bukoba mjini...na alikuwa amefungua miradi kadhaa zikiwemo pub maarufu...utajiri wake aliutoa kwa mganga na alipewa sharti moja tu kwamba maisha yake yoote asijisaidie haja yake ndogo au kubwa chooni....kwa hiyo jamaa kila alipokuwa akibanwa na haja alikuwa akiwasha gari yake na kuelekea porini...sasa siku moja watu walimuona akinya porini kwa hiyo ikawa ndiyo story kwenye kale kamji ka bukoba...ili kuondokana na aibu hii ilibidi jamaa ajiondoe uhai..kwa story za vijiweni inasemekana jamaa walimkuta amejikatakata na viwembe hotelini huku amefariki.....
 
Ipo hii bado ya moto kabisa ilitokea mwaka jana tu maeneo ya buguruni, kuna mama mmoja wa kiarabu hakubahatika kuwa na mtoto hivyo akamchukua mmoja akamlea mpaka akawa mbaba kabisa na akamuolea na mke kabisa na pamoja na kumpa nyumba maeneo ya mbagala aishi na mkewe.
Yule mama alikua mfanya biashara mzuri tu,ila mistake yake alikua anatunza ela nyumbani inasemekana ni za kutosha kabisa na hilo alilokua analijua ni yule mwanae tu mana kuna chumba ambacho kilikua marufuku kuingia mule.
Siku moja yule mama alitoka kidogo,nyumba nzima alibakia mfanyakazi wa ndani. Hamadi ikasimama difenda ya polisi na kuugonga geti kwa nguvu kidogo,yule Dada wa kazi akatoka kutaka kujua kulikoni,akakutana na polisi waliovalia kiraia huku wakiwa na radio call mkononi.
Basi wakampush wakaingia ndani kadhaa huku wengine wakiwa wamebaki ndani ya gari wakiangalia mazingira ya njee,walivyo ingia wakaanza kumtisha yule dada awaonyeshe yalipo madawa ya kulevya,yule Dada kwenye kutaharuki akachezea kibao kizito. Baadae wakamuamulu afungue chumba kimoja kimoja kwa ajili ya upekuzi.
Itaendelea.......
 
We Jamaa vp wewe,Hivi umeona wapi Kijiweni story inaendelea...
 
Kuna jamaa yangu hapa ananipa story za matajiri,
Anasema kule mbweni kuna jamaa, alikua amelala ndani kwake (sasa sijui alijuaje).
Wakawa wanapita watu wa mnada wa nyumba, jamaa ana pesa sana . Sasa akatoka nje baada ya kusikia wale jamaa wanapiga kelele. Akauliza mnauza nini jamaa wakasema nyumba. Akawauliza iko wapi, wakasema ile kule.
Jamaa akauliza bei, akaambiwa milioni mia,
Eti huwezi amini jamaa hapo hapo akatoa hela, kanunua nyumba. Milioni Mia.
Eti jamani vipi matajiri kwenu huko mbweni.
 
Basi walifanya hivyo mpaka walipofika kwenye kile chumba ambacho akifunguliwagi bila bi mdashi mwenyewe,walivyofika pale yule Dada wa kazi akagoma kwa kuwaambia hana funguo za hiko chumba,akachezea mkofi mwingine,akaishia kulia tu Dada wa watu.
Kilichotokea wale askari wakafanya wanavyojua wakaufungua ule mlango na kuingia na kuanza kupekua kile chumba wakakuta bonge LA sanduku likiwa limefungwa vizuri wakalibeba mpaka sebureni kisha wakazuga kwa kumuamrisha yule Dada alifungue aliposhindwa kufanya hilo wakawa wanawaka kuwa mle ndio kwenye madawa ya kulevya yalipo hifadhiwa hivyo wakamwambia wanaondoa nalo kama sehemu ya ushahidi na mwenyewe akirudi aende kuripoti kituo cha buguruni pale.
Basi wale jamaa walitoka na lile sanduku na kulipakiza kwa gari yao na wakatoka mbio kama vishada. Yule mama aliporudi akazikuta stori njee mana watu walianza kukusanyika eneo LA tukio na walishangazwa sana zile mbio za wale polisi. Akaingia ndani ndio akakutana na stori mbaya zaidi na hasa pale alipogundua wale watu wameondoka na sanduku kutoka kwenye kile chumba chake maalum.
Basi akatoka kwa kwenda kituo cha polisi kama alivyoelekezwa na Dada wa kazi,kufika pale akakuta hakuna doria ya aina hiyo iliyo endeshwa na kituo hiko kwa maeneo hayo anayosema. Dah mama akajua amepigwa hivyo akarudi home akitafakari nini cha kufanya. Basi yule mama kesho yake akarudi kwao Pemba huko,baada ya siku kadhaa akarudi zake kwake huku.
Sasa kilichotokea siku kadhaa baada ya tukio majira ya saa sita mchana yule beki tatu alikua anatoka njee kwenda dukani,akamuona mtu ambaye anahisi anamjua kwenye lile tukio akiwa anapita pale njee ya kwao,anaenda mpaka juu kisha anarudi zaidi ya Mara tatu,ndipo yule mdada akapata wasaa wa kumkumbuka na kuingia ndani na kumtonya bi mkubwa kuhusu yule jamaa nje.
Walipotoka kwa pamoja wakamkuta bado anapiga "mark time" za kwenda na kurudi kama mtu aliyepotea mahala. Basi akapiga simu polisi wakafika mpaka pale na kumchukua mtuhumiwa yule mpaka kituoni na mambo mengine kuendelea ya mahojiano ndipo yule mtuhuimiwa akakili na kutaja walipo wenzake na pesa walizoiba"kumbe lile sanduku lilikua na ela zilikua za kutosha tu". Na akawaambia pesa walizotumia mpaka sasa na hazikua nyingi kama kiasi walichobakisha na walikua wanasikilizia kwanza kabla hajawapeleka mgao.
Polisi wakaenda wakawakamata wrote na kufanikiwa kuzikamata na pesa zilozosalia na kuwarudisha kituoni. Zoezi lililofata ni kuwahoji kwa mapana kwa kipigo mpaka pale walipo on a wamtaje muhisika kupunguza kipigo mana kilizidi. Hapa ndio polisi walipopata na mshtuko kusikia "master minder" wa mchezo mzima alikua yule dogo aliyelelewa na yule mama tangia akiwa kichanga,basi mama akaitwa nusu azimie baada ya kupewa taarifa zile.
Dogo akaletwa mpaka polisi kisha akachangwa na watuhumiwa wengine kisha mmoja mmoja kwa wale mapolisi feki wanapita kumtambua,wote walimtoa yeye kwenye kundi LA watu alioletwa nae hapo mama anaona yote,alilia sana mwisho wa siku akataka polisi wayamalize Yale mambo bila ya kwenda mbele kumnusuru mwanae asiende jela lakini polisi walimkomalia kuwa hili jambo lazima lisonge mbele.
Kwenye kuhojiwa yule dogo akadai kafanya vile kwa kuwa ndugu wa yule mama wamekua wanamsimanga pamoja na kumpigia simu kuwa hana urithi kwa yule mama kwa kuwa yeye sio mtoto wake wa kumzaa hivyo aondoke,dogo zile kauli zilimuuma sana sema akawa anazimezea bila ya kumuambia mama yake mwisho akafanya alilofanya kuupata urithi wake mana mpaka kile chumba yeye ndio kawaelekeza na mambo mengineyo.
 
Wazee wa Mastory ya Town, hapa ndo mastory ya kwenye vijiwe vya kahawa yanachakatwa
IMG_20220325_231940.jpg
 
Stori za gahawa songea huko sijui nilipigwa kamba kijiweni au vipi maana alisimulia Mzee zipo nyingi ila moja ni hii.

Kuna Mzungu alikua anasafiri na begi la hela wale wenye mashamba makubwa ya kahawa vijijini, Sasa akatembea akadondosha lile begi maana alikua kalifunga kwenye pikipiki nyuma sasa mwamba mmja mbeba mkaa kaliona lile begi kafungua ndani kakuta kuna Ela nyingi sana eti kalichukua kalifunga juu ya mkaa nyuma kwenye baiskeli.

Sasa Mzungu yule kufika mbele akagundua begi halipo akaanza kuludi nyuma chap ghafla akakutana na yule jamaa wa mkaa akamuuliza ilo begi umepata wap jamaa akajibu nimeokota Mzung akauliza ndani kuna nin jamaa akajibu nimeona kuna Ela kama ni zako chukua tu baba jamaa alikua anajibu kwa kuogopa rangi nyeupe Mzungu akamtukana yule Jamaa P*mbu zako mtu mweusi wew utakufa masikini huwezi kuwa tajiri kamwe kampiga na makofi mawili matatu alaf kachukua begi kasepa.
 
Hyo kweli, tena huyo mzungu alkuwa mtu wa kaniss
 
Miaka hiyo nawinda porini kulikuwa na broo mmoja anasoma town akirudi bush alikuwa friend wangu sana kwenye story

Basi anakwambia siku kaenda kijiwe cha baiskel akakuta story ya kumuhusu shabiby na utajiri wake

Kwamba mme na mke walikubaliana baada ya kuwa na ugumu wa maisha wakaenda kwa mganga ili kupata utajiri,baada ya kufika kwa mganga wakaambiwa waende kilimani chochote watakachokutana nacho wasikipishe

Safari ikaanza kama ya nusu saa bila maruweruwe ghafla ikatokea bus kutoka mlimani na speed ya train ya umeme mme akaogopa akakimbia kupisha njia,mke akakomaa mara mpaka basi inamfikia ghafla ikapotea wakarudi kwa mganga

Mganga akawambia mwanamke ndo atakuwa mwenye mali na jamaa ikabidi aambiwe haruhusiwi kuwa nae maana kakosea masharti kwahiyo yule mama akaolewa na jamaa mwingine ambaye ndo shabiby wa sasa

Kama kuna mtu anaijua story hii anaweza ongezea nyama za vijiweni
Hii kahawa ya ukweli kabisa. I mean ni story ya kahawa
 
Kuna jamaa yangu wa karibu alinipa hii,kuna ndugu yao kwenye ukoo alikua choka mbaya sana yule dogo malezi yake yalikua ya shida mpaka anakua mkubwa lakini kwa sasa maisha yamembadilikia japo watu wanalalamika bata sana kuliko kujenga maisha yake.
Ipo hivi yule dogo baada ya kufariki bi mdashi wake ndio akaja kupata siri kuhusu baba ake mana tangu udogoni hakuwai kumjua na ilikua balaa kuuliza swali hilo yani lazima achezee mimbata.
Lakini kumbe bi mdashi alishandaa maandishi yaliyompa maelekezo kuhusu baba make,dah bahati ilikua yake mana siku ile barua iliposomwa na yule aliye achiwa hakuamini masikio yake kujua moja ya watu wakubwa na tajiri nchini ndio baba ake mzazi.
Basi jamaa akaenda mpaka kwa yule tajiri akajitambulisha,yule bosi wala hakushtuka akamwambia karibu mwanangu japo jamaa alijifanya kupaniki lakini bosi akatoa sababu zake maisha yakaendelea.
Mpaka sasa jamaa anasimamia miradi ya mzee wake kwa kifupi maisha yamebadilika sana kwake lakini ubaya watu hawaoni mabadiliko zaidi ya majigambo ya kuwanunulia watu pombe ila watu wanamkumbusha kuwa familia ya huyo bosi itamkataa huko mbeleni mana ya Mungu nayo mengi mana jamaa ni black mzee wake ni coloured.
Hivi black sio color?
 
Naleta moja ya tajiri mmoja aliekuwa anaitwa Rwabizi..huyu jamaa alikuwa ni tajiri kiasi pale bukoba mjini...na alikuwa amefungua miradi kadhaa zikiwemo pub maarufu...utajiri wake aliutoa kwa mganga na alipewa sharti moja tu kwamba maisha yake yoote asijisaidie haja yake ndogo au kubwa chooni....kwa hiyo jamaa kila alipokuwa akibanwa na haja alikuwa akiwasha gari yake na kuelekea porini...sasa siku moja watu walimuona akinya porini kwa hiyo ikawa ndiyo story kwenye kale kamji ka bukoba...ili kuondokana na aibu hii ilibidi jamaa ajiondoe uhai..kwa story za vijiweni inasemekana jamaa walimkuta amejikatakata na viwembe hotelini huku amefariki.....
Huyo alikuwa muogamuoga Sana!Kwani watu walijua ana poop porini ndio Nini Sasa?wacha wajue
 
Ipo hii bado ya moto kabisa ilitokea mwaka jana tu maeneo ya buguruni, kuna mama mmoja wa kiarabu hakubahatika kuwa na mtoto hivyo akamchukua mmoja akamlea mpaka akawa mbaba kabisa na akamuolea na mke kabisa na pamoja na kumpa nyumba maeneo ya mbagala aishi na mkewe.
Yule mama alikua mfanya biashara mzuri tu,ila mistake yake alikua anatunza ela nyumbani inasemekana ni za kutosha kabisa na hilo alilokua analijua ni yule mwanae tu mana kuna chumba ambacho kilikua marufuku kuingia mule.
Siku moja yule mama alitoka kidogo,nyumba nzima alibakia mfanyakazi wa ndani. Hamadi ikasimama difenda ya polisi na kuugonga geti kwa nguvu kidogo,yule Dada wa kazi akatoka kutaka kujua kulikoni,akakutana na polisi waliovalia kiraia huku wakiwa na radio call mkononi.
Basi wakampush wakaingia ndani kadhaa huku wengine wakiwa wamebaki ndani ya gari wakiangalia mazingira ya njee,walivyo ingia wakaanza kumtisha yule dada awaonyeshe yalipo madawa ya kulevya,yule Dada kwenye kutaharuki akachezea kibao kizito. Baadae wakamuamulu afungue chumba kimoja kimoja kwa ajili ya upekuzi.
Itaendelea.......
Unakata stimu
 
Back
Top Bottom