Umewahi kupata Hasara gani kutokana na Fundi Ujenzi kukosea makadirio ya Vifaa?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,190
4,103
Hawa mafundi kuna wakati wanatia hasara sana, anaweza kukupigia makadirio ya vifaa vya kujenga, aidha kubwa sana au ndogo sana kulingana na uhalisia.

Unakuta umepigiwa gharama ya mifuko 50 ya simenti kumbe inatakiwa 80 tofauti kubwa kabisa na umejipigapiga umeanza ujenzi inaishia katikati mnasimama ujipange maana hukua umetarajia.

Au anakupigia nondo 15 kumbe zinatakiwa 7 unajikuta zinabaki unaanza kuuza kwa bei ya hasara, wengine mabati nk.

kkoU-aGf_400x400.jpg

Umewahi kutiwa hasara gani na fundi wakati wa makadirio?
 
Yeah alipiga hesabu bati 177 mwisho wa siku zikatumika bati 155. Zikabaki bati 22 na kila bati nilinunua 37,000/=

Shilling laki nane wakanitia hasara ambayo walau ningechonga hata ma grill.

Sent from my vivo 1938 using JamiiForums mobile app

Tumieni wataalamu mnatuona wanoko! Sasa hiyo laki 8 si ingetosha kabisa kuweka injinia wa part time awe anakushauri kadri ujenzi unavyo endelea?
 
Hawa mafundi kuna wakati wanatia hasara sana, anaweza kukupigia makadirio ya vifaa vya kujenga, aidha kubwa sana au ndogo sana kulingana na uhalisia.

Unakuta umepigiwa gharama ya mifuko 50 ya simenti kumbe inatakiwa 80 tofauti kubwa kabisa na umejipigapiga umeanza ujenzi inaishia katikati mnasimama ujipange maana hukua umetarajia.

Au anakupigia nondo 15 kumbe zinatakiwa 7 unajikuta zinabaki unaanza kuuza kwa bei ya hasara, wengine mabati nk.

kkoU-aGf_400x400.jpg

Umwahi kutiwa hasara gani na fundi wakati wa makadiro?
Wez hao balaa
 
Huu ushamba wa kusoma ramani si nikanunua ramani ya vyumba 4 mbili master? Wakati sipo nkamuachia fundi na wife wakajenge msingi kuja kurudi nakuta boooonge la nyumba na msingi umekula 10+M saivi nimetulia kwanza maana hii nyumba ntapandisha vipande vipande 😂😂😂
 
Attachments

  • Screenshot_20230323-202325_WhatsApp.jpg
    Screenshot_20230323-202325_WhatsApp.jpg
    373.9 KB · Views: 67
Kaniambia anaweza kupiga ripu nikamuelewa kumbe ni mpiga ripu za utope kurudi namkuta ananiambia tusubilie cement ikauke ndipo ang'alishe..

Kesho yake narudi namkuta anahaha kurekebisha namuuliza fundi vipi.? eti itabaki hivyo hivyo, bado kidogo nimtandike vibao nikamtimua kama kuku..

mifuko yangu miwili ya cement ikafa dadeki...
 
Wacha kabisa hawa mafundi...

Wakati napauwa fundi alisema leta mbao kiasi flani nikaja na ileile idadi yake na mikaongeza hapo kidogo tena, fundi kapiga mbao plus na ile idadi yngu bado mbao zinahitajika kama PCs 15, kumuuliza anadai hajawahi fanya site kama hii adai hapo site kuna miujiza.

Nikaona huyu anacheza na akili yangu, nikampa option ya tufanyaje yeye bila kujua akasema tukaongeze mbao. Mbao ikaongezwa na mwendo ukaenda wa bati akaja na idadi yake na mwisho yakaongezwa 7 katika hiyo idadi yake. Twende kazi mwisho wa siku kuna gape tena kumuuliza anadai fundi aliyejenga sio mtu mzuri alikuwa anataka hiyo kazi iwe yake.

Kumuuliza suluhisho akasema twende dukani, tukaenda dukani akaja na idadi yake tena nikaongeza 5 kwenye yake na mwisho wasiku likabaki bati moja. Mbona mtu alilia mwisho wa siku anadai ela yake.

Nikamuuliza fundi hapo alikuwa nan kati ya mm na yeye, akasema yeye mkadiriaji wa material ni nani? Akasema yeye sasa nikamuuliza fundi akikosea kukadiri mara ya kwanza na mara ya pili hii hasara yakununua material ambayo unauziwa kwa retail na si wholesale nani anailipa, akasema ni mimi kwakuwa site ni yakwangu... Kilichofata aliondoka mweupe mfukoni atajua aliwalipaje vibarua wake izo ni additional cost ambayo yeye mwenyewe ndio alijitengenezea.
 
Kuhusu mafundi Sina hata la kusema hao watu wamefanya hata nashindwa kufurahia hatua nayopiga kwenye ujenzi
Walizidisha nondo kama nne =10000
Bati Moja 27000
Bodi za gypsum 2 =30000
PVC walizidisha
Mbao za kupaulia ndio kabisa walizidisha ila bahati nzuri nilishaleta mtu akanipigia hesabu nilienda kununua Kisha nikasimamia kwa umakini zikatosha walishindwa kabisa kujiamini
Dah!ujenzi Mungu ndie anatupa amani ila unaumiza sana
 
Tumieni wataalamu mnatuona wanoko! Sasa hiyo laki 8 si ingetosha kabisa kuweka injinia wa part time awe anakushauri kadri ujenzi unavyo endelea?
Baadhi yenu mainjinia ndiyo munachangia sana kwenye kututia hasara. Huwa hamupiti kazini mafundi wanafanya wapendavyo halafu siku unayopita unaanza 'bomoa hapa umekosea' sasa jee hiyo ni sawa?
 
Kaniambia anaweza kupiga ripu nikamuelewa kumbe ni mpiga ripu za utope kurudi namkuta ananiambia tusubilie cement ikauke ndipo ang'alishe..

Kesho yake narudi namkuta anahaha kurekebisha namuuliza fundi vipi.? eti itabaki hivyo hivyo, bado kidogo nimtandike vibao nikamtimua kama kuku..

mifuko yangu miwili ya cement ikafa dadeki...
Hahaha
 
Wacha kabisa hawa mafundi...

Wakati napauwa fundi alisema leta mbao kiasi flani nikaja na ileile idadi yake na mikaongeza hapo kidogo tena, fundi kapiga mbao plus na ile idadi yngu bado mbao zinahitajika kama PCs 15, kumuuliza anadai hajawahi fanya site kama hii
Huyu fundi hujamtendea haki.
Cha muhimu wewe hakikisha hujaibiwa materials, zote ziingie kwenye nyumba yako. Lakini mtu kutoka jasho na anaondoka bila kulipwa sio sahihi kabisa na Mungu aliyekupa uwezo wa kujenga hawezi kufurahi. Hao vibarua wamekukosea nini mpaka wafanye kazi bila malipo.
Hii story yako imeniuma sana.
 
Nlimkataa fund aliyekuja kupiga tathmin ..kwakuwa alitaja bei ya ujenzi kubwa sanaa....aseee nkampata fundi maiko akataja nusu yake....nkampa tenda ....
 
Wacha kabisa hawa mafundi...

Wakati napauwa fundi alisema leta mbao kiasi flani nikaja na ileile idadi yake na mikaongeza hapo kidogo tena, fundi kapiga mbao plus na ile idadi yngu bado mbao zinahitajika kama PCs 15, kumuuliza anadai hajawahi fanya site kama hii

Ila mkuu ulimkosea sana jamaa we ungemlipa tu aisee...

Wakati napiga bati na jirani yangu akawa ana Piga basi fund kanipa makadilio ya mbao 2*2=200 na 4*2=250

Basi Mimi nikanunua kwakupunguza 150 kwa200... Zikapungua kama 25 na 30 hiv Jiran yangu zimebak kama 50 kwa 50 hiv nikazinunua kwa bei ya hasara sana Mana bei ya kupiga dawa na ya usafir sikuhusika nayo kabisa....

Materials bora uongeze kuliko yabakie mkuu unaweza ukakosa wa kumuuzia kaka...kama Jiran mambo kibao kabak nayo
 
Huyu fundi hujamtendea haki.
Cha muhimu wewe hakikisha hujaibiwa materials, zote ziingie kwenye nyumba yako. Lakini mtu kutoka jasho na anaondoka bila kulipwa sio sahihi kabisa na Mungu aliyekupa uwezo wa kujenga hawezi kufurahi. Hao vibarua wamekukosea nini mpaka wafanye kazi bila malipo.
Hii story yako imeniuma sana.
Hakika mkuu amewafanyia kitendo kibaya sana kaz zenyewe ngumu usimlipe mtu kisa kakadiria vibaya huo ni unyama hapaswi kujisifia hapa
 
Ila mkuu ulimkosea sana jamaa we ungemlipa tu aisee...

Wakati napiga bati na jirani yangu akawa ana Piga basi fund kanipa makadilio ya mbao 2*2=200 na 4*2=250

Basi Mimi nikanunua kwakupunguza 150 kwa200... Zikapungua kama 25 na 30 hiv Jiran yangu zimebak kama 50 kwa 50 hiv nikazinunua kwa bei ya hasara sana Mana bei ya kupiga dawa na ya usafir sikuhusika nayo kabisa....

Materials bora uongeze kuliko yabakie mkuu unaweza ukakosa wa kumuuzia kaka...kama Jiran mambo kibao kabak nayo
Kuna mahali huwa nanunua material kwa wholesale bei rahisi sasa huyu fundi yeye ananipeleka kwa retail alafu anataka gharama ziwe zangu kwavile yeye ni mjengaji na anasema faida ni yakwangu, nani kakudanganya

Iyo hela ya nyongeza braa si ungenunu hata vito vya dhamani nyumba ikapendeza braa
 
Huyu fundi hujamtendea haki.
Cha muhimu wewe hakikisha hujaibiwa materials, zote ziingie kwenye nyumba yako. Lakini mtu kutoka jasho na anaondoka bila kulipwa sio sahihi kabisa na Mungu aliyekupa uwezo wa kujenga hawezi kufurahi. Hao vibarua wamekukosea nini mpaka wafanye kazi bila malipo.
Hii story yako imeniuma sana.
Sometimes unabidi uwe capitalist ili mambo yako yaende ukiwa socialism braa wewe utakuwa nimtu wakusema mungu atanilipa tuu
 
Huu ushamba wa kusoma ramani si nikanunua ramani ya vyumba 4 mbili master? Wakati sipo nkamuachia fundi na wife wakajenge msingi kuja kurudi nakuta boooonge la nyumba na msingi umekula 10+M saivi nimetulia kwanza maana hii nyumba ntapandisha vipande vipande
Mafundi wengi wa kitaa kusoma ramani hawajui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom