Uzi maalumu kwa watu wasiofunga kipindi cha mfungo

Uzi maalumu kwa watu wasiofunga kipindi cha mfungo

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2022
Posts
3,903
Reaction score
9,915
Salaaam...

Tupo katika kipindi ambacho Waislamu na Wakristo kwa pamoja tupo katika mfungo.

Hata hivyo ndani ya kipindi hiki, si wote tutafunga/ tunafunga na hii ni kutokana na sababu mbalimbali aidha kiafya na nyinginezo ambazo hazitaruhusu uwe katika mfungo.

Uzi huu ni maalumu kwa wale ambao hawajapata au hawatoweza kufunga katika kipindi hiki ili ku-share mawili matatu, aidha

• uliwahi kufunga ila safari hii
hautafunga na kwanini?

• Umefunga kwa siku kadhaa ila kuna siku ambayo hukufunga ndani ya mwezi wa mfungo na kwanini

• Changamoto zipi unazopitia katika
mazingira uliyopo kwa kuwa
hujafunga

• Umepanga kurekebisha
changamoto zipi na kwa namna
gani ili wakati ujao uweze kufunga?


Lengo ni kupata mawazo mbalimbali na changamoto zinazojitokeza tupate mawazo toka kwa watu mbalimbali juu ya namna ya kuzikabili ili wakati ujao tuweze kufunga pia.

Karibuni.
 
Kitabu Gani imeandikwa mkuu?
Screenshot_20250305-125711_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom