Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imetangaza hatua mbalimbali za kuboresha usafiri wa wanafunzi katika maeneo ya mijini, kufuatia malalamiko ya wanafunzi kuhusu kunyanyaswa na baadhi ya wahudumu wa mabasi ya daladala.
Akizungumza na vyombo vya habari, Jijini Dodoma Tarehe 04 Februari, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imechukua hatua baada ya kusikiliza kilio cha mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza, Mariana Eric Mirindima wa Shule ya Sekondari Jangwani, aliyebainisha changamoto wanazokumbana nazo wanafunzi wanaotumia usafiri wa daladala, ikiwemo kugomewa nauli maalumu na kunyimwa huduma.
Prof. Mbarawa amesema Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa nauli ya Shilingi 200 kwa wanafunzi, kuanzisha mabasi maalumu ya wanafunzi nyakati za asubuhi na jioni, pamoja na kutenga mabehewa maalumu katika treni za mijini ili kuongeza usalama na upatikanaji wa usafiri kwa wanafunzi.
Aidha, Waziri Mbarawa ameielekeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kupitia Mkurugenzi wake CPA Dkt. Habibu Suluo kuhakikisha wanaimarisha udhibiti wa madereva na makondakta, kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kuwanyanyasa wanafunzi, na kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vituo vya daladala.
Wizara imetoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa na ushahidi wa vitendo vinavyokiuka Sheria za usafiri wa ardhini kupitia namba za bure za LATRA 0800 11 00 19, 0800 11 00 20 au WhatsApp 0681 300 800.
Hatua hizi zinalenga kuhakikisha wanafunzi wanapata usafiri salama, wa uhakika na wenye staha utakaowawezesha kupata elimu zao katika mazingira rafiki.