Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika kuisheherekea siku ya wawanawake duniani tarehe 8 Machi 2019, Zoom Tanzania ikiamini nguvu ya mwanamke katika jamii ingependa kuchukua nafasi hii kutambua ujasiri na upambanaji wao katika jamii. Katika karne hii, mwanamke amepewa kipaumbele na kuwezeshwa katika jamii, jambo lililosababisha wanawake wengi kujitambua na kufanya mambo makubwa zaidi kuliko hapo awali.
 
Jasiri



Mwanamke mpambanaji ni jasiri anaona nafasi za kujiendeleza na kuzinyakua haraka. Mwanamke jasiri haogopi kushindwa na changamoto zilizo mbele yake, siku zote huchagua kuzikabili. Wanawake wengi majasiri wamefanikiwa kuinua uchumi wao na kuzisimamia familia zao, wakati mwingine bila hata ya msaada wa mwanaume. Ni wajasiriamali. Ni wanawake wenye nyadhifa za uongozi wakifanya kazi na kuleta maendeleo kwa bidii.
 
Hufanya Maamuzi Sahihi

Mwanamke mpambanaji haogopi kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yake na kufuatilia mipango yake. Hupokea maoni chanya na kuamua pia kupuuzia maoni ya watu wengine yasiyo na tija ama ambayo hayamsaidii kwenda mbele na kutimiza ndoto zake. Kutokana ma mapito yake, mwanamke mpambanaji hufanya mamuzi sahihi juu ya jinsi gani ya kubadili mwenendo wa maisha yake ili kujiboresha siku zote.
 
Ana Ndoto



Mwanamke mpambanaji ana ndoto za kuwa mtu fulani ama kufikia malengo fulani. Haogopi kuwa tofauti na mategemeo ya wengine. Pia anajua ni njia gani za kufuata ili kutimiza ndoto zake. Anajua umuhimu wa kuwa makini na kila nafasi inayopita mbele yake inayoahidi mafanikio. Ndoto zake ni muhimu kwake na huzipa kipaumbele.
 
Mbunifu

Mwanamke mpambanaji ni mbunifu kila wakati. Wanawake wamebarikiwa uwezo wa kufanya mambo mengi katika muda mchache. Hivyo basi, mwanamke mpambanaji anajua jinsi ya kujigawa katika kazi, kuongeza ujuzi na kujaribu mambo mbalimabli ili apate matokeo sahihi katka mambo anayoyafanya.
 
Anajitegemea

Mwanamke mpambanaji anajua kujisimamia katika mambo mbalimbali maishani. Hii haimaanishi mpambanaji hahitaji msaada kwa wengine bali anajua msaada peke yake hautoshi. Anafahamu kuwa lazima ajiongeze maana kuna mambo mengi anayohitaji kutimiza. Hivyo basi, anaelewa nafasi yake katika maendeleo yake na hata ya familia yake.
 
Hujitoa



Mwanamke mpambanaji anatambua mchango wake katika jamii inayomzunguka. ujitoa kwasababu ni jambo sahihi na si kwa ajili ya kupata umaarufu ama cheo. Mwanamke mpambanaji pia anajua thamani ya kuwainua wengine na kuwatia moyo wale wanaomwangalia. Siku zote, anajitambua na kutambua mchango wake katika jamii yake.
 
Anatia Hamasa

Mwanamke mpambanaji huhamasisha jamii yake kuwa bora zaidi kupitia juhudi zake na mafinikio yake huhamasisha watu wengine kuongeza jitihada katika shughuli na mambo mbalimbali. Mpambanaji sio mchoyo wa maarifa, na hupenda kuona wengine wakifanikiwa kupitia yeye.
 
Mwaka mpya unatupa mwazo mpya na nafasi ya kutafakari mipango ya mwaka jana na namna ya kujiandaa na mwaka ulio mbele yetu. Ni vema Kuweka malengo na namna ambavyo utaweza kuyafikia mapema, hasa kipindi kama hiki cha Januari. Sio kazi ngumu. Unaweza ukachukua muda mchache tu na kuandika malengo utakayotaka kukamilisha mwaka huu. Hizi ni namna ambavyo unaweza ukajiwekea malengo bora zaidi kwa mwaka huu:
 
Tafakari Kuhusu Mwaka Ulioisha



Kabla ya kuanza kupanga mipango ya mwaka huu, ni vyema ukaangalia ulipotoka kwanza. Kuna uwezekano mkubwa ukahitaji kuazima baadhi ya mbinu ulizotumia kukamilisha malengo fulani mwaka jana. Pia, itakupa nafasi ya kujifunza kutokana na mipango ambayo haikwenda kama ilivyotakiwa mwaka jana. Unaweza kujiuliza maswali machache kama;

Wapi nilitumia hela na muda mwingi sana mwaka jana?
Tabia gani nahitaji kuachana nazo?
Ni jambo gani zuri nilifanikisha mwaka jana? Na kadhalika.
Maswali kama haya yatakupa mawazo yatakayokusaidia kuweka malengo mazuri zaidi kwa mwaka huu
 
Malizia Ulivyoviacha Mwaka Jana

Ni mipango ipi au kazi zipi ambazo ulipanga kuzikamilisha mwaka jana na hukufanikiwa? Unaweza kuikamilisha kabla ya kuanza mipango mipya ya mwaka huu? Kuna uwezekano ya kuijumuisha mipango ya mwaka jana katika mipango ya mwaka huu ili uifanyiekazi pamoja? Kwa namna yeyote ile, usiache mipango ya mwaka jana ambayo hukuikamilisha iende na maji. Usikubali akili yako izoee kutokamilisha/kushindwa vitu. Tafuta namna ya kumalizia mipango yako kwanza na hapo ndio utaweza kuianza vyema ya mwaka huu.
 
Weka Mkazo kwenye Malengo Yenye Uhalisia



Sawa, tunashauriwa tuwe na ndoto kubwa. Lakini kiukweli huwezi ukajiwekea malengo makubwa ambayo huwezi kuyatimiza. Utakua unajitengenezea mazingira ya kujiona unashindwa. Kama unahitaji kukamilisha mipango yako ya mwaka huu vyema basi iwe yenye uhalisia. Weka malengo ambayo utaweza kutengeneza picha kichwani ya jinsi utakavyoyatimiza.
 
Usisahau Afya Yako Mwaka Huu

Bila kujali majukumu, malengo au umri, kamwe usiache kujali afya yako kwenye malengo yako ya mwaka huu. Fikiria kama utaweka mipango mingi mizuri kisha kushindwa kuitimiza kwa sababu ya magonjwa ambayo ungeweza kuyaepuka. Zipo namna nyingi apazo unaweza kuchagua ili kuishi maisha yenye afya bora mwaka mzima. Mfano:-
 
Kujiwekea ratiba nzuri ya kupata muda wa kutosha kupumzika. Huwezi kutimiza malengo yako ukiwa umechoka choka.
Kujijengea mahusiano mazuri ya kijamii.
Kufanya mazoezi ya kutosha. Na sio lazima uende Gym. Unaweza kujinunulia vifaa vya kufanyia mazoezi nyumbani na bado ukawa fiti mwaka mzima
Kujiwekea ratiba ya kumwona Daktari mara kwa mara.
 
Jifanye Uwe Kipaumbele Chako Mwaka Huu



Umewahi kusika ule msemo kwamba ‘huwezi kuwasaidia wengine mpaka uweze kujisaidia mwenyewe kwanza?’. Hiki ndicho hasa unatakiwa kukifanya mwaka huu kama utahitaji mafanikio. Hii haimaanishi kwamba hutakiwi kuwasaidia wengine, hapana.
 
Back
Top Bottom