Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Arsenal XI: Leno, Bellerin, Mustafi, Holding, Kolasinac, Xhaka, Torreira, Mkhitaryan, Ozil, Aubameyang, Lacazette

Liverpool XI: Alisson, Alexander-Arnold, Gomez, Van Dijk, Robertson, Fabinho, Milner, Wijnaldum, Salah, Firmino, Mane
 
Kuhusu kuvunja ndoa ya Kiba, Mchekeshaji afunguka



Msanii wa vichekesho Bongo maarufu kwa jina la Martha, amefunguka juu ya kuwa chanzo cha kuiweka pabaya ndoa ya msanii Abdu Kiba, na kusema kwamba yeye hahusiki kwa lolote

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Martha amesema kwamba licha ya kuwa aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Abdu Kiba, lakini kwa sasa hayuko naye tena, hivyo habari za kuwa chanzo cha migogoro ya ndoa yake sio kweli.

Akiendelea kufunguka juu ya mahusiano yake na Abdu Kiba, Martha amesema Abdu Kiba amekuwa akimtafuta mara kwa mara kwa njia ya simu, lakini hakuna chochote kinachoendelea kati yao, kwani sasa wamebaki marafiki wa kawaida.

“Nilikuwa natoka naye, mara nyingi ananicheck, toka nimetoka kwake tayari nilikuwa na mahusiano na mtu mwingine, ni mwanaume ambaye nilikuwa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu, lakini kuvunja ndoa yake sijui, tangu ameoa sijamfuatilia lakini yeye ndio amekuwa akinifuatilia sana, mimi nachati naye tu, mimi sijui kama mkewe anachukia”, amesema Martha.

Sambamba na hilo Martha amekwenda mbali zaidi kwa kusema hata mke wake hapaswi kuchukia kwani anatakiwa atambue kabla yeye hajaolewa, kuna watu walikuwa kwenye mahusiano na mume wake.
 
Back
Top Bottom