Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

nsamaka,mwanamke wa furaha yangu,uliye zaliwa kwa lengo la kuwa mama bora wa familia,faraja ya moyo,furaha ya maisha.Usiye weza kujieleza,hata ukikwazwa bado unalibeba kosa kuwa lako,unaishia kulia tu,kwanini unakimbilia kuomba msamaha wakati kosa sio lako?msukuma wangu upo peke yako wa aina hiyo.Mwanamke wa huruma,nisemaje nsamaka unielewe ulivyo muhimu kwenye familia hii? Wewe sio mke tu bali ni rafiki yangu mkubwa na msiri wangu,hakika utaishi nafsini mwangu daima milele... hongera kwa kutimiza miaka hiyo japo bado nakuona mtoto sana,hasa umwagapo chozi la kukwazika napenda nikunyamazishe kwa kukupakata huku umeegamia shingoni kwangu,ukinirowanisha kwa chozi na kamasi laiiiniii nsamaka wewe ni mpaka kifo.Ya dunia yaone ila usiyajali.Ishi utakavyo ili niwe na wivu. Nakupenda mama,nakupenda nsamaka Furahia siku yako ya kuzaliwa na rafiki zako.Jifunze kuishi na watu vizuri.Nakupenda sana.
Uuuuh si kwa ujumbe huu mzuri, kweli sikufanya kosa kupata mwenza maana ww ni zaidi ya mwenza.
Thanks in advance my swity andjul.
 
Back
Top Bottom