Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Daktari raia wa Kenya nchini Uingereza amesema kuna sheria isiyokuwa na msingi inayomzuia kutochangia damu kwasababu ameoa mke raia wa Kenya.

Francis Gĩthae Murĩithi, ametoa wito wa kubadilishwa kwa sheria hiyo ili kutia moyo wachangia wengi zaidi raia wa Waafrika.
 
Wizara ya Afya Uingereza inasema kwamba ni ''marufuku kwa watu walioa au kufanya mapenzi na mtu ambaye anashukiwa kuwa huenda alishiriki mapenzi na watu wanaoishi nchi zilizoathirika na ugonjwa wa virusi vya ukimwi ikiwemo 'nchi nyingi tu za Afrika' kuchangia damu.''
 
Daktari Murĩithi, ambaye anafanyakazi kama mtalaamu wa uzazi na maradhi ya kina mama huko East Midlands, alisema yeye na mke wake wa miaka miaka saba walikuwa katika mahusiano ya mume na mke mmoja na hawajawahi kuachana.
 
Kama daktari, anasema tayari amefanyiwa vipimo tangu alipomuoa mke wake na kwamba hajawahi kupatikana na virusi vya ukimwi.

Lakini anasema aliarifiwa kuwa anaweza tu kuchangia damu ikiwa mke wake pia naye atapimwa virusi vya ukimwi na shirika hilo hilo la utoaji damu au kama watajizuia kushiriki tendo la ndo kwa miezi mitatu.
 
Murĩithi, 38, ambaye kwa sasa anaishi na Gamston, Nottinghamshire na damu yake ni ile nadra kupatikana ya kundi la AB+, alisema: "Ni sheria isio na msingi inayozuia uchangiaji wa damu.

Ikiwa utafungia watu kama mimi, na uendelee kusema kwamba Waafrika hawajitokezi kuchangia damu, itatufanya tuonekane wabaya wakati ambapo mfumo ndio kizuizi.
 
Mshauri wa Wizara ya Afya Uingereza, Su Brailsford, amesema sheria za kuwezesha na kutowezesha uchangiaji wa damu, msingi wake ni ushauri wa kitaalamu uliolenga kupunguza hatari kwa wanaopokea damu hiyo.
 
Lakini aliongeza: "Tunajua kwamba kutathminiwa kwa hatari zilizopo kwa mtu mmoja mmoja, kunaweza kuruhusu watu wengi zaidi kama daktari Murĩithi kuchangia damu kwa njia salama.

"Tumepanga kupitia upya sera hii ambayo tuna matumaini itaanza kufanyakazi kabla ya mwisho wa mwaka huu."
 
Back
Top Bottom