Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa yakini zimekujieni hoja, ishara na dalili wazi kutoka kwa Rabb wenu. Atakayeona na kuzitambua, basi ni kwa faida yake mwenyewe, na atakayepofuka asizione basi hasara itamrudia mwenyewe, (sema) nami si msimamizi.
 
Na wala msiwatukane wale wanaowaomba asiyekuwa Allaah, wasije nao kumtukana Allaah kwa uadui bila ya ujuzi. Hivyo ndivyo Tumewapambia kila ummah amali zao, kisha kwa Rabb wao Pekee yatakuwa marejeo yao, Atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.
 
Na wakaapa kwa Allaah, viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba ikiwafikia Aayah (Muujiza) bila shaka wataiamini. Sema: Hakika Aayaat (Miujiza, Ishara) ziko kwa Allaah. Na kitu gani kitakutambulisheni kwamba zitakapokuja hawatoamini?
 
Na hivyo ndivyo Tulivyojaalia kwa kila Nabiy maadui mashaytwaan wa kibinaadam na kijini, wanadokezana wenyewe kwa wenyewe maneno ya kupambapamba na ya ghururi. Na lau Angetaka Rabb wako wasingeliyafanya hayo. Basi waachilie mbali na wanayoyatunga (ya uongo).
 
(Sema): Je, nitafute hakimu ghairi ya Allaah na hali Yeye Ndiye Aliyekuteremshieni Kitabu kilichofasiliwa waziwazi? Na wale Tuliowapa Kitabu (kabla) wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Rabb wako kwa haki. Basi usijekuwa miongoni mwa wanaotia shaka.
 
Back
Top Bottom