Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_20191009_192426.jpg
 
Mpendwa wangu Shimba ya buyenze
Hujanitendea haki mpendwa. Yaani nilimisi picha yako kwa sekunde tu nikakuta ushaifuta. Nikalia weee uirudishe lakini wala hukujali mpendwa. Whai?

Ushombe shombe na ulimwende wa Mashariki ya Kati nitaushuhudia lini jamani? Siyo fea mpendwa. Uliyemwekea nikamuuliza na yeye akawa analia eti hakuidaunilodi. Basi mateso tupu mpendwa
 
Vimbunga msotoko?
Nadhani hata kwetu huku vinapatikana.
Kwa sasa hali ya mambo ikoje Florida ?
Florida hawana Tornado sana. Hii nadhani ni water spout - kakimbunga msokoto kanapopita juu ya maji. Tornado ni huko Tornado Alley kuanzia Alabama, Oklahoma, Texas, Nebraska na Kansas huko. Florida wao ni wazee wa hurricanes...
View attachment 1227792
 
Hujanitendea haki mpendwa. Yaani nilimisi picha yako kwa sekunde tu nikakuta ushaifuta. Nikalia weee uirudishe lakini wala hukujali mpendwa. Whai?

Ushombe shombe na ulimwende wa Mashariki ya Kati nitaushuhudia lini jamani? Siyo fea mpendwa. Uliyemwekea nikamuuliza na yeye akawa analia eti hakuidaunilodi. Basi mateso tupu mpendwa
Hivi ulikuwepo online nilipoweka picha yangu nashukuru niliifuta sekunde kabla wachomoa betri hawaja sreenshort 😀😀😀
 
Vimbunga msotoko?
Nadhani hata kwetu huku vinapatikana.
Kwa sasa hali ya mambo ikoje Florida ?
Aisee sijui. Niliondoka FL kitambo. Ila msimu wao wa hurricane huanza Juni 30 mpaka Desemba 30. Kwa hiyo sasa wapo katikati na bahari ya Atlantic inaweza kujikoroga wakati wo wote na kuleta maafa. Nilishashuhudia hurricane 4. Sikuzipenda. Mchana inageuka usiku, umeme hakuna, maji kama wakati wa Nuhu na upepo mkali unabeba mavitu na kuyagonga huku na huko. Kikija kupita ukitoka nje utafikiri jitu lenye nguvu na hasira nyingi limepita na kuitikisa miti yote na mingine kuing'oa kabisa na kurusha vitu huku na huko. Ndipo utagundua kwamba kama binadamu, pamoja na teknolojia na maarifa yetu yote, kwa mother nature bado saana tena sana...
 
Back
Top Bottom