Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Amenilazimisha mtu mmoja niandike kuhusu Ronaldo...sawa. Msimamo wangu ni huu..Madrid wamefanya biashara mwafaka wakati mwafaka...walimnunua miaka tisa iliyopita kwa pauni 80M wamemuuza kwa faida ya pauni 8M zaidi..miaka tisa baadaye akiwa ameshawapatia mataji manne ya Ulaya pamoja na mengineyo ambayo kibiashara yameipa Madrid mabilioni ya pesa...kumuachia Ronaldo hayakuwa maamuzi ya kukurupuka kutoka kwa Florentino Perez. Ana washauri wenye akili timamu wakiwemo Madaktari...wamemwambia Mwili wa Ronaldo ambaye Feb 5 mwakani atatimiza miaka 34 hautaendelea kuwa ule. Thamani yake uwanjani (licha ya kuendelea kufunga) lakini itapungua tu kwa sababu ametoka katika tumbo la mwanamke kama binadamu wengine...Kwa miaka mitatu sasa mtachunguza na kugundua kuwa Ronaldo amekuwa mviziaji zaidi kuliko Ronaldo wa zamani. anajua kwenda na mwili wake. Labda sasa Perez atahitaji kasi ya zamani ya Ronaldo kutoka kwa Mbappe, na mabao anaweza kuongeza kutoka kwa mtu mwingine (Benzema naye kachoka tu). Kwa Ronaldo halisi wa miaka mitano nyuma Perez asingekubali aondoke ng'oo...VIPI JUVENTUS?...kuna wasichana wazuri sana ambao kijana fulani mwenye pesa ya kawaida hauwezi kuwapata mpaka wakianza kuchoka...ndicho walichofanya Juventus...wanaumalizia ubora wa Ronaldo kibiashara na mabao pia..wasingeweza kupoteza fursa hii hata kama Ronaldo wa leo sio wa miaka mitano iliyopita. Kwa Ronaldo mwenyewe? alitaka kuonja kucheza soka la Italia. tunawadharau tu Waitaliano kwa sasa lakini soka la Italia lina historia na heshima...De Lima alicheza pale...Maradona alicheza pale..Hata mimi nusura nicheze pale basi tu Mzee Kumwembe alinizuia niende Lutengano kusoma na kuvuta bangi
 
BBC Dira TV: Ufaransa wameshinda Kombe la Dunia wakiwa na wachezaji wapatao 14 ambao ni waafrika. Kaka yake Paul Pogba, Florentin anaichezea Guinea, huku kaka wa kipa Steve Mandanda anaichezea DRC. Iwapo wachezaji hao wameweza kushinda Kombe la Dunia, kwanini timu za Afrika zinashindwa kutumia viaji vyake kufanya vizuri katika Kombe la Dunia. Tweets Salym
 
Back
Top Bottom