Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mdomo uko Bahari ya Hindi kati ya Mtwara (Tanzania) na Rasi ya Delgado (Msumbiji). Mdomo wenyewe una umbo la delta. Athira ya maji kujaa au kupwa baharini huonekana km 20 kabla ya mdomo wenyewe.

Kabla kufika kwenye delta kuna feri inayobeba magari kati ya Tanzania na Msumbiji. Feri ilipelekwa hapa na mapadre Wabenedikto wanaofanya kazi pande zote mbili za mto.

Tawimito muhimu ni Muhuwesi na Lumesule upande wa Tanzania, halafu Lucheringo na Lujenda upande wa Msumbiji.
 
Geita. Mtoto wa miaka sita amefariki dunia akiombewa mlimani alikopelekwa kutolewa mapepo, huku mama yake mzazi akishikiliwa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akizungumzia tukio hilo amesema lilitokea Februari 18,2018 saa tano asubuhi katika mlima Gambiwe.

Amesema mama wa mtoto Neema Petro (25) na mke mwenzake Raheli Musa (25) walikwenda mlimani na mtoto huyo kwa ajili ya maombi na kufunga.

Kamanda amesema wanawake hao wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang'hwale wanashikiliwa kutokana na kifo cha mtoto Frank Bariki (6), ambaye mwili wake umekutwa na majeraha shingoni na kwenye mbavu.
 
Walinzi watatu na muuguzi mmoja wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, wamejeruhiwa baada ya kutembezewa kichapo na ndugu wa mgonjwa aliyefariki dunia wakiwatuhumu wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa uzembo.

Mkurugenzi mkuu wa Bugando, Dk Abel Makubi amesema tukio hilo la aina yake lilitokea Februari 18, siku moja baada ya mgonjwa huyo wa kike aliyekuwa na miaka 80 kufikishwa hospitalini hapo.
 
Mgonjwa huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu na shinikizo la damu,” amesema Dk Makubi

Alisema baada ya ndugu kupokea taarifa za kifo cha mgonjwa aliyefariki saa 9:00 usiku wa kuamkia Februari 18, walivamia hospitalini hapo na kuanza kutembeza kipigo kwa muuguzi wa zamu na walinzi waliokuwa zamu usiku.
 
Katika tukio jingine, Dk Makubi amesema hospitali hiyo imeanzisha uchunguzi maalumu dhidi ya baadhi ya watumishi wanaodaiwa kushirikiana na madalali na mawakala kuwahamisha wagonjwa na kuwapeleka hospitali binafsi za jijini Mwanza. “Hii ni hujuma na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za nidhamu na kisheria,” alisema Dk Makubi.
 
Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA) imekamata dhahabu yenye thamani ya Ksh100 milioni (takriban Sh2 bilioni za Tanzania) na inamshikilia Mtanzania anayehusika na mzigo huo.

Katika taarifa yake, KRA imesema imekamata gramu 32,255.50 za dhahabu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
 
tapatalk_1500973856149.png
 
Taarifa hiyo imesema, Mtanzania huyo mwenye miaka 46 alikuwa na ankra inayoonyesha mzigo huo una thamani ya dola 859,890 za Marekani.

"Mtuhumiwa alikamatwa baada ya kupata taarifa za kiintelijensia. Alifika Uwanja wa JKIA Ijumaa Februari 16, 2018 akisafiri kwa ndege ya Shirika la Precision kutoka Mwanza kupitia Kilimanjaro na alikuwa akienda Dubai kwa ndege ya shirika la Kenya Airways," taarifa ya mamlaka hiyo imesema.
 
Timu ya maofisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ikiongozana na maofisa wa huduma za udhibiti wa mapato walichukua maelezo kutoka kwa mtuhumiwa.

"Usafirishaji wa bidhaa ni kinyume cha vifungu vya Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya mwaka 2004 sehemu ya 85 (3) na Sura ya Pili ya sehemu B (4) katika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki," imesema KRA.
 
Kifungu hicho cha sheria hakiruhusu usafirishaji wa madini yasiyoongezwa thamani na vito katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hivi sasa dhahabu iliyokamatwa iko chini ya KRA, huku maofisa wa forodha na udhibiti wa mipaka wakiendelea na uchunguzi.
 
Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri kupiga marufuku vifaa vinavyowekwa kwenye bunduki kama vile vilivyotumiwa na mtuhumiwa ambaye aliwaua watu 58 waliohudhuria tamasha mwaka jana Las Vegas.
 
Akizungumza katika Ikulu ya White House, Trump alisema tayari ameiagiza Wizara ya Sheria kupendekeza sheria ya kuharamisha vifaa hivyo vinavyowekwa kwenye bunduki za semi-automatic ili kumwezesha mtumiaji kurusha mamia ya risasi kwa dakika moja.

Mjadala juu ya udhibiti wa bunduki ulichukua sura mpya na uharaka baada ya watu 17 kuuawa shuleni huko Florida wiki iliyopita.
 
Wanafunzi na wazazi walioathiriwa na mauaji hayo katika Shule ya Sekondari ya Marjory Stoneman Douglas Jumatano wamepanga kufanya maandamano katika mji mkuu wa Tallahassee.

Baadhi yao waliwasili Jumanne ili kuweza kuonana na mamlaka kushuhudia wakikataa pendekezo la kupigwa marufuku kwa silaha za mashambulizi na zenye magazine kubwa. Hata hivyo, mamlaka itafikiria marufuku kwa sehemu kubwa.
 
Geita. Mtoto wa miaka sita amefariki dunia akiombewa mlimani alikopelekwa kutolewa mapepo, huku mama yake mzazi akishikiliwa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akizungumzia tukio hilo amesema lilitokea Februari 18,2018 saa tano asubuhi katika mlima Gambiwe.

Amesema mama wa mtoto Neema Petro (25) na mke mwenzake Raheli Musa (25) walikwenda mlimani na mtoto huyo kwa ajili ya maombi na kufunga.

Kamanda amesema wanawake hao wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang'hwale wanashikiliwa kutokana na kifo cha mtoto Frank Bariki (6), ambaye mwili wake umekutwa na majeraha shingoni na kwenye mbavu.
Maulana Mola wangu tuepushe walahi
 
Back
Top Bottom