Uzi maalum kwa wapenda "ADVENTURE"

Uzi maalum kwa wapenda "ADVENTURE"

20220215_122159.jpg

Huu ni mto Simiyu, umeanzia Arusha/Manyara ukatembea wee hadi unaingia ziwa Victoria hapa Magu. Tembea uyaone, zurura unione
 
Nakumbuka nikiishi znz 2005 tutakodi gari private na mpenzi wangu ambaye sasa ni mama watoto basi tukaenda nungwi kula raha sana tukaamua kulala kulekule sasa kesho yake kurudi tulipopanga zile gorofa za kilimani tukawa tulisahau pump ya maji switch tuliacha on umeme ulikuwa umekatika .umeme kurudi ukaanza kupump maji na tank lilikuwa mle mle ndani bwana eee tukakuta nyumba nzima vyombo vinaelea makochi yamejaa maji .

Maji yalipanda hadi zamu ya mgao ilipokoma ndio ikawa salama yake
 
Nilikuwa camping serengeti.
Wageni 3 mi driver na mpishi.
Ilikuwa 4 days camping.
Katika ile campsite ajabu tukajikuta wenyewe tu.
Tukaweka tents zetu tukalala!
Asubuhi after bfast tukatoka kufanya game.
Muda wa mchana ukafika safari ikaanza kurudi kempu.kwaajili ya hotlunch.

Kufika pale simuoni mpishi ni mboga tuu inaungua.nikaanza kumuita ikawa kimya.

Nikaanza kuzunguka na gari hapo kempu huku nikimuita.chini ya mti nikakuta simba kama 5 hivi.jamaa alipotuona ndio akaanza kuniita huku analia.nilipojua yuko juu ya mti ule simba wako chini basi nikawatawanya wale simba kwa gari wakakimbia.tulicheka sana siku hiyo.

Ingine tulilala katika tented camp moja.
Tent zao pale ni kubwa sana.kulikuwa na vitanda vinne.
Basi usiku tumelala akaingia pundamilia.
Yaani alichana ile tent akazama hadi ndani.afu ilikuwa giza kinoma.
Wote hatukujua ni mnyama gani zaidi ya roho kuhisi kama zinatoka leo.ikawa kimya pale ndani.nikawasha tochi kumulika naona pundamilia.nikazima tochi.mshkaji pembeni akamulia kwenye kidirisha ziko simba kama 7 hivi.simba ni mnyama makini sana huwa haingii sehem kiboya.wakawa wanamsubiri jamaa atoke!
Tent sisi tupo iko mbali sana na tent zingine.ile siku sitakuja kusahau.
Tutamtoaje punda maana yuko stressed na nje anajua anasubiriwa.yaani ikawa kitanda kikilia tuu kidogo punda anarusha mateke ya kufa mtu.ukikohoa punda anapiga mateke ya hatari.
Ikabidi tutulie kama masaa 3 kimyaaaa.
Ndio punda akatoka akawa anaangalia kama kuna noma.hapo tukabeba kitanda kizima tukazibia pale kwenye tobo.punda hakupiga hata hatua 10 jamaa wakamtaiti.akawa kitoweo.asubuhi wageni wameamka wanakuta hiyo tukio wakafurahi sana.
 
Very interesting
 
Back
Top Bottom