Uzembe wa Askari kulenga shabaha na kupoteza risasi 49 unaposingiziwa ushirikina

Kupiga Target inayo tembea na kukosa risas n ktu cha kawaida hata kwenye movie, ndo maana sniper akikosa risas moja huwa haendelei kukaa eneo alilochagua kukaa kwasababu anafaham atakosa risas zingine nyingi zaid na anakua kwenye hatari ya kushambuliwa yeye
Suala la fisi kuhusishwa na iman ya kishirikina hizo ni iman za watu tu kitu Cha msingi ilikua ni lazima auwawe hata ingetumika risasi 60 hicho ndo kitu Cha msingi kwakua ni fisi aliesumbua kwa muda mrefu ndo maana hawakupewa risasi 1 ili wakauwe fisi na wakapewa risasi nyingi zaid kwakua wao ndo wataalam wa mambo hayo na wanajua Kuna kukosa target hasa inayo kimbia zigzag
 
Sasa kama wana intelijensia kwamba risasi hazifanyi kazi kwanini waendelee kutumia hizo risasi ? Kuna mambo ukishayakubali nusu tu ni kwamba unaingia kwenye unkown territory yaani itabidi kila kitu umeze tu (hakuna haja ya logic wala kuuliza) na tungeendelea hivyo tokea kali mpaka leo watu wangekuwa wanatolewa kafara na kuzikwa na wafalme wakiwa hai....

Haya mambo yafanyike individually huko ila sio kwenye taasisi muhimu wala kuyafanya kama taifa...
Wakati unasema haya, ukumbuke kuwa mnyama huyo alikuwa ameleta maafa huko nyuma, na wala halikuwa tukio jipya. Maafa aliyoleta ni pamoja na kuuwa watu, wanyama, nk. Kuonekana tena kwa mnyama huyo, ni dhahiri kuwa alitakiwa akabiliwe kwa namna yoyote ile ilimradi auwawe.

Hivi nikuulize ndugu yangu, ukikutana na adui (iwe mtu, mnyama, au vyovyote), na huyo adui ana nia mbaya na wewe, je, sihala moja ikifeli, basi unaacha kupambana naye na hivyo kumpa nafasi nzuri ya kukumaliza? Hapa namaanisha; katika mazingira ya huyo mnyama alivyojitokeza, je askari baada ya kumkosa kwa risasi kadhaa, wangeachana naye ili aendelee kuleta madhara?

Mimi na wewe tushukuru tu kuwa mambo haya hayajatukuta, yakikukuta ndugu yangu utatumia sihala zote zilizo jirani yako, na zikiisha, utajikuta unatumia hadi meno!
 
Tabora huko....na kila anayesimulia anahusisha na imani za kishirikina, kunzia Msemaji wa Polisi.

Inasikitisha, Taifa limeoza likiongozwa na Wanahabari wetu.
Askari unakuta tangu atoke mafunzoni ajawahi lenga tena shabaha unazani nini tena kitatokea
 
Kupiga Target inayo tembea na kukosa risas n ktu cha kawaida hata kwenye movie, ndo maana sniper akikosa risas moja huwa haendelei kukaa eneo alilochagua kukaa kwasababu anafaham atakosa risas zingine nyingi zaid na anakua kwenye hatari ya kushambuliwa yeye
Suala la fisi kuhusishwa na iman ya kishirikina hizo ni iman za watu tu kitu Cha msingi ilikua ni lazima auwawe hata ingetumika risasi 60 hicho ndo kitu Cha msingi kwakua ni fisi aliesumbua kwa muda mrefu ndo maana hawakupewa risasi 1 ili wakauwe fisi na wakapewa risasi nyingi zaid kwakua wao ndo wataalam wa mambo hayo na wanajua Kuna kukosa target hasa inayo kimbia zigzag
Tatizo ni hao watoa taarifa wanapojitahidi kuonesha kanakwamba hilo ni suala ni la kishirikina, hapo ndipo tatizo langu lipo.

Sijui hali iliyokuwepo kwene eneo husika...ila kwa maelezo kuwa kusema alikuwa anakwepa risasi inaleta picha ya kama vile Fisi naye alikuwa anajaribu kukabiliana na Wa/Mpigaji hivyo akawa anakwepa risasi....nadhani hata wewe unajaribu kuhisi tu hali ilivyokuwa ya kwamba Fisi alikuwa kwenye movement.

Iwapo maelezo ya Msemaji wa Polisi yangejikita kwenye utaalamu zaidi basi bila shaka angeongea jambo linalomake sense kuliko alivyoongea...kwa mfano angesema Fisi alikuwa anakimbia huku Askari wetu wakijaribu kumpiga rusasi na zikatumika zaidi ya risasi 40 na hatimaye walifanikiwa kumlenga.

Suala la movement nalifahamu na hata inashauriwa unapokuwa kwenye hali ya kushambuliwa kwa bunduki ni vizuri kufanya movement kuliko kusimama au kukaa mahali pamoja, haswa kama hakuna kizuizi ha kujibanza karibu.
 
Wakati unasema haya, ukumbuke kuwa mnyama huyo alikuwa ameleta maafa huko nyuma, na wala halikuwa tukio jipya. Maafa aliyoleta ni pamoja na kuuwa watu, wanyama, nk. Kuonekana tena kwa mnyama huyo, ni dhahiri kuwa alitakiwa akabiliwe kwa namna yoyote ile ilimradi auwawe.

Hivi nikuulize ndugu yangu, ukikutana na adui (iwe mtu, mnyama, au vyovyote), na huyo adui ana nia mbaya na wewe, je, sihala moja ikifeli, basi unaacha kupambana naye na hivyo kumpa nafasi nzuri ya kukumaliza? Hapa namaanisha; katika mazingira ya huyo mnyama alivyojitokeza, je askari baada ya kumkosa kwa risasi kadhaa, wangeachana naye ili aendelee kuleta madhara?

Mimi na wewe tushukuru tu kuwa mambo haya hayajatukuta, yakikukuta ndugu yangu utatumia sihala zote zilizo jirani yako, na zikiisha, utajikuta unatumia hadi meno!
Hoja ya aliecomment ilikuwa ni kupingana na imani kuwa kuna miujiza ya kukabiliana na risasi.

Risasi ikikupata sehemu hatarishi hakuna namna ukapona, ni labda upoteze maisha kwa kupoteza kiasi kikubwa cha damu kutokana na jeraha au risasi hiyo ifikie na kujeruhi sehemu hatari(sensitive) ambapo utapoteza maisha papo hapo.

Kwa tukio hilo la Fisi suala la muhimu lilikuwa ni kumpata Fisi kwa risasi ili afe, na sidhani kama kuna Mtu ana tatizo na inatumiaka silaha ya aina gani na kwa mara ngapi, ilikuwa alimradi Adui anayekusudiwa aanguke.

Hoja ya uzi ni namna Jeshi na Jamii wanavyojaribu kufunika suala la Askari kutumia idadi tajwa ya risasi kwa maelezo kuwa Fisi alikuwa anakwepa...hai make sense hata kidogo...wao ndio walikuwa wanamkosa, sasa ndio watuambie labda kama Fisi alikuwa anakimbia nao wanalazimika kumkimbiza huku wanamshoot.
 
Nilimsikiliza Msemaji wa Polisi, Mwanamama akiwa anazungumzia tukio hili kana kwamba kulikuwa na miujiza na si uzembe wa Wahusika.

Ni aibu sana kwa karne hii kama bado tuna ujinga wa kuabudu vitu ambavyo havipo halafu hapohapo tunataka tupate Vijana wa kuleta mapinduzi ya sayansi na teknolojia.

Hatuwezi kufika kokote kwa ujinga wa aina hii, na ukweli ni kwamba Askari hao hawakuwa na uwezo. Na huenda hata kwenye matukio ya Ujambazi Polisi hupoteza risasi nyingi mpaka kufanikiwa kumlenga Muhusika.

Huyo/hao Askari waliohusika kupoteza silaha zote hizo wahakikiwe uwezo wao wa kutumia silaha kwa ufanisi...huenda Askari wetu ni legelege kiasi cha kutumia silaha huku wakiwa wanatetemeka kwa kumuogopa Fisi.

Tukiendelea kuendekeza haya mambo ya kijinga tutakuza taifa la Wanaume 'Mashoga' na kutafuta visingizio. Taifa tunahitaji Wanaume wenye balls (Men with balls)

MEN WITH BALLS

View attachment 1871310
View attachment 1871501
wewe utakuwa ulitoka tumboni mwa mama yako kwa njia ya UPASUWAJI- NYAMAZA
 
Tuna taifa lenye ujinga sana.

Na wenye akili wanajua ku take advantage....ndio yale ya kuambiwa Pesa za Vikoba zimebenwa na chuma ulete.

Taifa linahitaji tiba hili...taifa limejaa ujinga.
Haya wote tujifanye ni wajinga tukubali ni ushirikina. Sasa ilikuwaje hiyo moja ikampata baada ya kukwepa nyingine zote? Huo ushirikina unachagua risasi ipi isipate shabaha na ipi ipate shabaha? Hii nchi imani za ushirikina kila kona. Ndiyo maana kina Gwajima wanapata sadaka kwa wingi mpaka wanakuwa matajiri kwa sababu zinapelekwa na watu wanaodhani wakienda huko kanisani hawatalogwa.
 
Kuna mengi huyajui, hao askari wanakutana na mambo mengi sana, mengine hadi wao wenyewe wanaenda kwa waganga ili kutimiza. kuna majambazi mengine hata ukiyalenga risasi haziingii na yanakusogelea yakunyang'anye bunduki,

Utafanya nini kama sio kutoka nduki...hahaha, risasi 49 kulenga na fisi anakwepa sio kitut rahisi, ushirikina upo, kama hauamini kuna siku utakunyorosha hadi urudi hapa useme kweli upo.

Niko Sumbawanga hapa nakula Ugali Kwa mzee anaogopeka Sana lakini simwogopi hata Kwa nukta na yeye anajua Uchawi ni wewe na jirani yako kutishana
 
Kuna mengi huyajui, hao askari wanakutana na mambo mengi sana, mengine hadi wao wenyewe wanaenda kwa waganga ili kutimiza. kuna majambazi mengine hata ukiyalenga risasi haziingii na yanakusogelea yakunyang'anye bunduki,

Utafanya nini kama sio kutoka nduki...hahaha, risasi 49 kulenga na fisi anakwepa sio kitut rahisi, ushirikina upo, kama hauamini kuna siku utakunyorosha hadi urudi hapa useme kweli upo.
Na kwanini hutaki kuamini kuwa inawezekana askari hao hawana shabaha? Si unajuwa kuna wale wakali wa shabaha (masnaipaz) na wengine hawajafikia huko, nawengine pengine mimi na wewe ndo hatujui kabisaa..!!
 
Bado nasisitiza kama huyo Fisi hakuwa anakimbia basi kutumia risasi 50 ni uzembe wa hali ya juu.

Lazima tutofautishe Mtu mwenye mafunzo na raia wa kawaida kwenye matumizi ya silaha.
 
Haya wote tujifanye ni wajinga tukubali ni ushirikina. Sasa ilikuwaje hiyo moja ikampata baada ya kukwepa nyingine zote? Huo ushirikina unachagua risasi ipi isipate shabaha na ipi ipate shabaha? Hii nchi imani za ushirikina kila kona. Ndiyo maana kina Gwajima wanapata sadaka kwa wingi mpaka wanakuwa matajiri kwa sababu zinapelekwa na watu wanaodhani wakienda huko kanisani hawatalogwa.
Ahahahahahaha labda ushirikina uliekispayaa...!!!
 
Kuna vitu Kama mtanzania lazima ujifumze kufikiria Yan kujiuliza maswali ya msingi.

1. Kasha la kuhifadhi risasi kwenye bunduki huwa Lina risasi ngapi?

2. Askari polisi/wanyama pori anapowewa silaha huwa anapewa na risasi ngapi?

3. N Askari wangapi walienda au walitumwa kwenda kurudisha utulivu baada ya janga la fisi kutokea?

4. Je kwa tukio la fisi kushambulia kulikuwa na ulazima kwenda na risasi zaidi ya 20
 
Nilimsikiliza Msemaji wa Polisi, Mwanamama akiwa anazungumzia tukio hili kana kwamba kulikuwa na miujiza na si uzembe wa Wahusika.

Ni aibu sana kwa karne hii kama bado tuna ujinga wa kuabudu vitu ambavyo havipo halafu hapohapo tunataka tupate Vijana wa kuleta mapinduzi ya sayansi na teknolojia.

Hatuwezi kufika kokote kwa ujinga wa aina hii, na ukweli ni kwamba Askari hao hawakuwa na uwezo. Na huenda hata kwenye matukio ya Ujambazi Polisi hupoteza risasi nyingi mpaka kufanikiwa kumlenga Muhusika.

Huyo/hao Askari waliohusika kupoteza silaha zote hizo wahakikiwe uwezo wao wa kutumia silaha kwa ufanisi...huenda Askari wetu ni legelege kiasi cha kutumia silaha huku wakiwa wanatetemeka kwa kumuogopa Fisi.

Tukiendelea kuendekeza haya mambo ya kijinga tutakuza taifa la Wanaume 'Mashoga' na kutafuta visingizio. Taifa tunahitaji Wanaume wenye balls (Men with balls)

MEN WITH BALLS

View attachment 1871310
View attachment 1871501
Hawa ndio watumishi wanaoapata nafasi kwa kubebwa na ndugu,au kufoji,huyu hata kuongea Kwake,unaona kabisa hana weredi,anaongea kama mtu aliyeishia darasa la saba,yaani anatuletea story za kinjekitile ngwale,risasi kuwa maji!fisi anakwepaje risasi?!ishu ni kuwa hakukuwa na Askali wanaojua kulenga shabaa,Askali wetu wanajua mikwala ya Kutishia Raia,kubambikizia watu kesi,
Huyu kamanda hii nafasi alibebwa tu,au atakuwa ni goma la mkubwa,unatumika kuanzia chuo,mpaka kazini,
 
Halafu kuna yule mama alisema askari "wao" hawawezi kupiga risasi 16 na kukosa kwenye kampeni😂😂

Sijui jina lake anaitwa nani yule mama. I'll nashangaa wamama wanapingana kauli zao
Mama Wanu
 
Kuna vitu Kama mtanzania lazima ujifumze kufikiria Yan kujiuliza maswali ya msingi.

1. Kasha la kuhifadhi risasi kwenye bunduki huwa Lina risasi ngapi?

2. Askari polisi/wanyama pori anapowewa silaha huwa anapewa na risasi ngapi?

3. N Askari wangapi walienda au walitumwa kwenda kurudisha utulivu baada ya janga la fisi kutokea?

4. Je kwa tukio la fisi kushambulia kulikuwa na ulazima kwenda na risasi zaidi ya 20
Kuhusu kubeba silaha ya aina gani au silaha ngapi na risasi ngapi si suala la kuumiza kichwa sana kwani lengo kuu ni kwenda kuimaliza hatari kadri itakavyowezekana.

Kule kwa wenzetu nionavyo kupitia vipasha habari mbalimbali ni kuwa Mtu anapotoa taarifa ya tatizo kwa Polisi, Polisi huhitaji taarifa muhimu za awali kujua hali ilivyo eno husika ili nao wafike wakiwa na nafasi ya kumaliza tatizo lililopo...kwa mfano hutaka kujua kama tayari kuna Majeruhi ili wanapokuja waje pamoja na Watoa huduma ya kwanza n.k.

Maisha ya Mtu au Watu huja kwanza na sio silaha, kama uliwahi kuona kuna Zoo kule Marekani walilazimika kumuua Sokwe maarufu aliyeitwa Harambee kwa sababu ya kuokoa maisha ya Mtoto(binaadamu), ulikuwa ni uamuzi mgumu sana lakini ilibidi.

Kwa tukio hili la Tabora kinacholeta sintofahamu sio walifikaje, bali ni namna ambavyo Waliokuwa wanamlenga Fisi kwa risasi na kuishia kutumia risasi takribani hamsini na kati ya hizo 49 zimemkosa...alafu Wahusika wanataka kuiaminisha Jamii kuwa suala zima lina ushirikina nani yake kwani Fisi yule alikuwa anakwepa risasi.

Hata kama walienda na Difenda iliyojaa silaha bado si hoja sana, jambo la kushangaza ni namna Askari mwenye mafunzo kukosa shabaha kiasi hicho bila maelezo ya kitaalamu badala yake kuishia kusingizia kuwa Fisi alikuwa anakwepa risasi.
 
Back
Top Bottom