Askari wa Israel wazidi kupukutika. Watu wa Gaza washangaa kifaru kupigwa na bunduki za RPG

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,200
10,948
Jeshi la Israel limekiri kupoteza askari wake 15 katika masaa 24 yaliyopita.Idadi halisi ya waliokufa huenda ni zaidi ya wale 67 waliotangazwa na Hamas hapo jana.

Katika taarifa za leo vikosi vya Hamas vimesema mapambano makali ya ardhini yanaendelea katika viunga vya mji wa Gaza na kwamba wamefanikiwa kuviripua vifaru kadhaa vya jeshi hilo.

Kwa upande wa watu wa Gaza wameshukuru kwamba Mola wao hajawasahau.Wakasema wameona maajabu ya vifaru vya Israel kupigwa kirahisi na bunduki za RPG ikiwa ni miongoni mwa silaha nzito za Hamas ijapokuwa ni silaha duni kulinganisha na silaha walizonazo jeshi la IDF.

Kuna uwezekano iwapo taarifa za vifo vya askari wa Israel zitaendelea kuwekwa wazi askari waliobaki wa miguu wanaweza wakaanza kuasi na kukimbia vifaru vyao.Hiyo ni miongoni mwa sababu za Israel kupendelea kupambana na Hamas huku mawasiliano yakiwa yamekatika.

Katika hatua nyengine Marekani imesema kuanzia sasa itaanza kutumia aina mpya ya silaha za Laser ili kujilinda na makombora yanayoendelea kurushwa dhidi yao kutoka Yemen,Syria na Iraq.

Faida ya silaha hizo ni kuwa hazina gharama kulinganisha na makombora yaliyozoeleka.Hatua hii imekuja wakati aina nyingi ya silaha zinazomilikiwa na majeshi hayo zikiwa pia zinamilikiwa na majeshi mengine na wanamgambo wenye ugomvi nao.

Pamoja na hivyo wachambuzi wa silaha wanasema aina hizo mpya za silaha huwa zinafanya kazi wakati hali ya hewa ikiwa ni nzuri tu.Huwa hazina uwezo wa kuona makombora yanayokuja kukiwa na ukungu au hali nyengine mbaya za hewa.

Suali la kujiuliza ni mpaka lini nchi hizo zitaendelea kuishi kwa uhasama na ubabe huku kila kukicha silaha zinazovumbuliwa huwa zinaingia mikononi mwa maadui zao.

1698850712976.png

Aina mpya ya silaha ya Lazer Marekani na Israel wanayokusudia kuitumia kujilinda dhidi ya makombora kutoka ardhini wanayorushiwa.
 
Mmh ila tunayoyashuhudia Aljazeera tena Pro HAMAS ni ya kusikitisha zaidi.Gaza wanapukutika mpaka imebidi wengine waruhusiwe kwenda Egypt kwa matibabu ya dharura.

Msemaji wa Wizara ya Afya anasema kila Hospital imefikia hatua wanachagua nani wajaribu kuokoa maisha yake na nani wamwachie ajifie tu.Hali ni mbaya sana Gaza huo ndiyo ukweli lakini.
 
Mleta uzi ni shehe flani unategemea aandike vitu gani kuhusu Israel?
Yeye na jamaa mmoja aitwa Malaria 2 kwa siku wanaandika hata nyuzi 50 za kuonesha namna gani wafuasi wa mnyazi mungu wa kikuresh wanavyowashambulia na kuua askari wa Israel.

Yaani habari zao ni israel kupigika toka kila pande za dunia. Toka Yemen hadi Somalia, toka Saudia hadi Zanzibar wanajeshi wa Israel wanapigika tu. Jamaa wanaripoti moja kwa moja toka uwanja wa mapambano pale Gaza.

Hadi nawaonea huruma, yaani Wapalestina wa madongo kuinama sidhani hata kama wapata muda wa kula maana kila dakika ni uzi tu.
 
Jeshi la Israel limekiri kupoteza askari wake 15 katika masaa 24 yaliyopita.Idadi halisi ya waliokufa huenda ni zaidi ya wale 67 waliotangazwa na Hamas hapo jana...
Hahaha we jamaa Gaza watu wanapukutika unasema watu wanashukuru. Sasa ulitegemea hakuna mjesh wa Israel hata kufa. Suala ni nani mshindi baada ya yote.
 
Jeshi la Israel limekiri kupoteza askari wake 15 katika masaa 24 yaliyopita.Idadi halisi ya waliokufa huenda ni zaidi ya wale 67 waliotangazwa na Hamas hapo jana...
Aisee, askari wa Israel wanakaribia kuisha.Hadi kufikia kesho taifa la Israel litakuwa majivu.Wanamuqawama wa Hamas wakipambana kwa kusaidiana na majihadist wengine wanawamaliza wazayuni.

Allah u akbar
 
Jeshi la Israel limekiri kupoteza askari wake 15 katika masaa 24 yaliyopita.Idadi halisi ya waliokufa huenda ni zaidi ya wale 67 waliotangazwa na Hamas hapo jana...
We bwana mujahidin hujitambui, habari bila picha ni upumbavu na uongo, unaongelea kifaru kinacho waka moto, ila picha ni kingine waarabu bwana🤣🤣🤣🤣🤣
 
Aisee,askari wa Israel wanakaribia kuisha.Hadi kufikia kesho taifa la Israel litakuwa majivu.Wanamuqawama wa Hamas wakipambana kwa kusaidiana na majihadist wengine wanawamaliza wazayuni.Allah u akbar
Kujifariji huku ni kupatwa kwa mujahedeen chini ya shimo🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hahaha we jamaa Gaza watu wanapukutika unasema watu wanashukuru. Sasa ulitegemea hakuna mjesh wa Israel hata kufa. Suala ni nani mshindi baada ya yote.
Watu wanashangaa gaza??? Are you serious kweli?? wakati Gaza watu wote ni vilio tu🤣🤣🤣🤣🤣🤣🏳️‍🌈
 
Wanauchungu na Palestina kuliko watanzania wawili waliotekwa.
Hii dini ni ya kinafiki sana
Wapalestina wanauliwa.Hawa watanzania matarajio bado wako hai
Lakini wakipatikana wahojiwe wazi wazi kwenye TV walitekwa wapi na je walikwenda kusoma kilimo au masomo mengine.
 
Back
Top Bottom