Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,744
- 870,523
Katika hali ya kawaida maisha huanza kutoka tumboni iwe yai, iwe mimba ama funza, lava na hata kiluwiluwi
Lakini kwa chura wa Suriname, uzazi wake huanzia .. Yaani mgongo hupasuka na vitoto vichanga hutoka!
Iko hivi
Baada ya kujamiiana, jike huchukua mayai yaliyorutubishwa kwenye mgongo wake. Kwa wiki kadhaa, ngozi yake hukua karibu na mayai ikiyazunguka, na kutengeneza vyumba vingi vya nyama. Ndani ya kila moja, taratibu chura mtoto hukua - mikono, miguu, na hatimaye mwili mzima
Wakati unapotimia ngozi hupasuka. Chura wadogo hujirusha kutoka mgongoni mwake kama makombora. Hakuna mayai. Hakuna viluwiluwi. Amfibia kamili tu, waliozaliwa kutoka mgongoni😀
Hii ni mojawapo ya uzazi ambayo hujawahi kuisikia...