Kwa wale wakulima wa mbogamboga hii itawasaidia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wale wakulima wa mbogamboga hii itawasaidia

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by CHASHA FARMING, Mar 8, 2012.

 1. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280


  [FONT=&amp]KILIMO[/FONT]
  [FONT=&amp]CHA[/FONT]


  [FONT=&amp]MBOGA MBOGA[/FONT]

  [FONT=&amp]SOMO LA KWANZA[/FONT]
  [FONT=&amp]KILIMO BORA CHA ZAO LA NYANYA.[/FONT]

  [FONT=&amp]I. MUHTASARI.[/FONT]

  [FONT=&amp]Nyanya ni mojawapo ya mazao makuu ya kilimo cha mbogamboga ulimwenguni na hushika nafasi ya 2 baada ya viazi mbatata. Hapa nchini Tanzania nyanya hulimwa kwa wingi karibu mikoa yote hususani mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mwanza, Dodoma, Pwani na mbeya.[/FONT]

  [FONT=&amp]LISHE.[/FONT]

  [FONT=&amp]Matunda ya nyanya zilizoiva hutupatia:-[/FONT]
  § [FONT=&amp]Vitamini A,B na C[/FONT]
  § [FONT=&amp]Madini aina ya chokaa.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Maji - 94%[/FONT]
  § [FONT=&amp]Utomwili(Protini )– 1%[/FONT]
  § [FONT=&amp]Mafuta – 0.1%[/FONT]
  § [FONT=&amp]Wanga – 4.3%[/FONT]
  § [FONT=&amp]Nyuzi nyuzi (Fibres) – 0.6%[/FONT]

  [FONT=&amp]MATUMIZI.[/FONT]

  [FONT=&amp]Nyanya hutumika kama:-[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kiungo cha kupukia.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Huliwa ikiwa mbichi kama kachumbari.[/FONT]
  § [FONT=&amp]……………………………………………………………………...[/FONT]
  § [FONT=&amp]………………………………………………………………………[/FONT]
  § [FONT=&amp]……………………………………………………………………..[/FONT]

  [FONT=&amp]CHANZO CHA ZAO LA NYANYA[/FONT][FONT=&amp].[/FONT]
  [FONT=&amp]Mmea wa nyanya uligundulika huko Amerika ya kati na kusini, baadaye ukaenea katika mabara mengine, ulizalishwa huko Mexico na kuletwa hadi Ulaya na baadaye ukasambaahadi kwenye nchi za tropiki.[/FONT]

  [FONT=&amp]II. MAZINGIRA. [/FONT]

  [FONT=&amp]Nyanya hustawi katika udongo wa aina nyingi ili mradi uwe na wepesi na usiotuamisha maji. (PH 5 – 7) Hali ya unyevu na joto jingi la usiku huleta majani mengi na matunda machache. Joto ni kati ya 18[SUP]o[/SUP]C -30[SUP]o[/SUP]C.Vilevile joto jingi, mwanga kidogo pamoja na hali ya unyevunyevu husababisha:-[/FONT]
  § [FONT=&amp]Magonjwa mengi kuenea.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Mmea kuwa na majani mengi.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Matunda madogo ambayo huchelewa kukomaa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Zao ili hupendelea mvua za wastani pamoja na kipindi kirefu cha jua.Hali ya mvua nyingi pamoja na baridi kali husababisha kuenea kwa magonjwa na wadudu waharibifu.Hii ndio sababu nyanya zinazozalishwa kwa kilimo cha umwagiliaji huwa na mavuno mengi yenye ubora kuliko wakati wa mvua.[/FONT]

  [FONT=&amp]III. AINA ZA NYANYA.[/FONT]

  [FONT=&amp]Zipo aina za nyanya zinazolimwa hapa nchini zinazofahamika na wakulima wengi ambazo hutoa mavuno mengi na bora, zinazostahimili magonjwa, zinazokomaa mapema na zenye ladha nzuri, umbo la kuvutia.[/FONT]
  [FONT=&amp]Aina hizo zimegawanyika katika makundi makuu mawili kutegemea ukuaji wake.[/FONT]
  [FONT=&amp]Aina fupi: Roma, Dwarf germ, ………………………………………………..[/FONT]

  [FONT=&amp]Aina ndefu:-Moneymaker, ………………………………………………………..[/FONT]

  [FONT=&amp]IV. KUSIA MBEGU.[/FONT] [FONT=&amp]Mbegu za nyanya huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye huhamishiwa shambani.Matayarisho ya kitalu hufanyika wiki 1 au 2 kabla ya kusia mbegu. Tengeneza tuta lenye upana wa mita 1 na urefu wa kuanzia mita 5 hadi urefu unaoweza kuhudumia kwa urahisi. Vunja mabonge makubwa kwa kutumia jembena kulainisha udongo vizuri.Changanya mbolea za asili zilizooza vizuri kama vile Samadi au mboji kiasi cha debe 1- 2 katika eneo la mita mraba 1. [/FONT]

  [FONT=&amp]Sawazisha kwa kutumia reki au kifaa kingine. Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kusia, kisha sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya sentimita 10 – 15 kutoka mstari hadi mstari. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kiasi kinachotosha eneo la mita mraba 1 ni gramu 3 – 5 (sawa na nusu kijiko cha chai hadi kimoja) Kiasi hiki cha mbegu huweza kutoa miche inayoweza kutosha kupandikiza katika eneo la mita mraba 100. Kiasi cha mbegu kinachohitajika kwa hekta 1 ni gramu 300. [/FONT]

  [FONT=&amp]Weka matandazo kama vile nyasi kavu na kasha mwagilia maji asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota.Mbegu huota baada ya siku 5 – 10. Ondoa matandazo baada ya mbegu kuota na endelea kumwagilia maji hadi miche itakapofikia kupandikizwa.Jenga kichanja ili kzuia jua kali na matone ya mvua yasiweze kuharibu miche michanga.[/FONT]

  [FONT=&amp]V. KUTAYARISHA SHAMBA.[/FONT]

  [FONT=&amp]Matayarisho ya shamba kwa ajili ya kupandikiza miche ya nyanya yaanze mwezi 1 kabla.Katua ardhi katika kina cha kutosha hadi kufikia sentimita 30. Lainisha udongo kwa kuvunja mabonge makubwa kwa kutumia jembe. [/FONT]

  [FONT=&amp]Weka mbolea ya asili wiki 2 kabla ya kupandikiza. Tani 20 kwa hekta 1 (sawa na ndoo 1 – 2) kwa mita ya mraba.Hii ni muhimu sana kwani zao la nyanya huhitaji chakula kingi toka kwenye udongo.(heavy feeders).[/FONT]

  [FONT=&amp]VI. KUPANDIKIZA.[/FONT]

  [FONT=&amp]Upandikizaji wa miche shambani hufanyika baada ya wiki 4 – 6 tangu kusia mbegu kitaluni na hutegemea hali ya hewa.Siku ya 10 – 14 za mwisho kwenye kitalu izoeshe miche hali halisi ya shambani.(hardening off). [/FONT]

  [FONT=&amp]Wakati huu ipatie miche maji na ondoa kivuli. Mwagilia maji kwenye kitalu kabla ili kurahisisha ungoaji wa miche na kuepuka kukata mizizi. Pia ni muhimu kumwagilia shamba siku moja kabla ya kupandikiza. Iwapo mbolea za asili hazikutumika wakati wa kutayarisha shamba unashauriwa kuweka mbolea ya mchanganyiko (NPK 5.10.5) kiasi cha gramu 5 kwa shimo wakati wa kupandikiza.Baada ya kungoa miche kitaluni usichelewe kuipandikiza, pandikiza muda wa asubuhi sana au jioni ili kuepuka jua kali linaloweza kunyausha miche.[/FONT]

  [FONT=&amp]Wakati wa kupandikiza hakikisha mizizi haipigwi na jua kwa kuiweka kwenye ndoo au chombo chochote chenye udongo wa unyevunyevu. Pandikiza miche katika kina cha sentimita 2 – 3 zaidi ya ilivyokuwa kwenye kitalu, hii husaidia:-[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kupata mizizi mingi mipya.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kunyonya viini lishe.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Miche kukua kwa nguvu zaidi.[/FONT]  [FONT=&amp]NAFASI:[/FONT]
  [FONT=&amp]Nafasi zinazotakiwa kutumika kwenye miche shambani hutegemea na:-[/FONT]
  § [FONT=&amp]Aina ya nyanya.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kama[/FONT][FONT=&amp] mimea ya nyanya itawekewa miti.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kama[/FONT][FONT=&amp] itaondolewa machipukizi.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Rutuba iliyoko kwenye udongo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Aina fupi ya nyanya: hupandikizwa katika nafasi ya sentimita 90 x 50 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 50 toka mche hadi mche. Nafasi kati ya tuta ni sentimita 60. Aina hii haihitaji kuegeshwa miti.[/FONT]

  [FONT=&amp]Aina ndefu inayohitaji kuegeshwa kwenye miti hupandikizwa katika nafasi zifuatazo:-sentimita 75 mstari hadi mstari na sentimita 50 – 60 toka mche hadi mche.[/FONT]

  [FONT=&amp]VII. KUTUNZA SHAMBA[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kuweka matandazo.[/FONT]
  [FONT=&amp]Baada ya kuhamisha miche shambani weka matandazo ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu. Pia husaidia mmomonyoko wa udongo na kutunza rutuba, pia hupunguza udongo kurukia kwenye matunda na kuyaacha katika hali ya usafi. Nyanya zenye matandazo huzaa matunda yaliyo bora zaidi.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kusimika miti ya kuegesha mimea ya nyanya[/FONT][FONT=&amp].[/FONT]

  [FONT=&amp]Wiki 2 baada ya kupandikiza simika miti ya kuegeshea nyanya, miti ni muhimu iwe imara na isiyooza wala kuanza kuota.Simika miti kiasi cha sentimita 8 – 10 toka kwenye sina la mmea.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mti usimikwe upande wa nje wa mstari ili kuzuia kuumiza mimea wakati wa kuhudumia.Kisha ushindilie mti sentimita 20 – 50 kwenda chini ya ardhi.Mti uwe na urefu wa mita 1.5 – 2 na unene wa sentimita 2 – 3.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kufunga nyanya kwenye miti.[/FONT]
  [FONT=&amp]Aina ndefu ya nyanya ni lazima ifungiwe kwenye mti ili:-[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kuzuia mmea usitambae chini.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kurahisisha unyunyuziaji wa dawa.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Umwagiliaji wa maji.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Uchumaji matunda.[/FONT]

  [FONT=&amp]Muhimu:[/FONT]
  [FONT=&amp]Wakati wa kufunga kamba, isiwe imekazwa sana na wala isiwe imelegea kupita kiasi. Kamba ifungwe umbo la nane kati yam mea na mti.Kamba ya katani au ya mgomba huweza kutumika. Funga kamba chini ya jani kila baada ya sentimita 20 – 25.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kuondoa machipukizi:[/FONT]
  [FONT=&amp]Kwa aina ndefu ya nyanya ni muhimu kuondoa machipukizi kila mara baada ya wiki 1. Muda mzuri ni asubuhi.Ondoa machipukizi yote na acha shina 2 tu. Usitumie kisu au mkasi bali vunja kwa mkono ili kuepuka kueneza magonjwa ya virusi na bacteria.[/FONT]
  [FONT=&amp]Sababu za kuondoa machipukizi:[/FONT]
  [FONT=&amp]- Huchukua chakula cha mmea.[/FONT]
  [FONT=&amp]- Mmea hutoa matunda mengi madogo ambayo hayafai kwenye soko.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kuondoa Majani[/FONT][FONT=&amp]:[/FONT]
  [FONT=&amp]Ondoa majani yote yanayoonyesha dalili zote za magonjwa au kushambuliwa na wadudu, yale yote yaliyozeeka ili kupunguza hali ya unyevu na kuruhusu hewa ya kutosha kwa mimea. Majani yote yaliyoondolewa yachomwe moto ili kuliweka shamba katika hali ya usafi.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kukata kilele:[/FONT]
  [FONT=&amp]Kwa kawaida aina ndefu ya nyanya huzaa ngazi 6 – 8 za matunda lakini mmea una uwezo wa kubeba ngazi 5 – 6. Hivyo ni muhimu kukata sehemu ya juu yam mea (kilele) ili kusimamisha ukuaji wake. Hii husaidia chakula kingi kwenda kwenye ngazi chache na hivyo kupata matunda makubwa. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kata kilele wakati mimea ifikiapo ngazi ya 6 na usikate karibu sana na ngazi na kata mkato wa mlalo ili kuruhusu maji kutiririka. Hata hivyo kama udongo una rutuba nyingi sana unaweza kuachia hata ngazi 8.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Palizi:[/FONT]

  [FONT=&amp]Palilia mara kwa mara kwa kupandishia udongo kwenye shina kwa uangalifu ili kuepuka kukata mizizi. Palizi husaidia maji na hewa kupenya kwa urahisi kwenye udongo. Hata hivyo kama mimea imewekewa matandazo ya kutosha na haina miti ya kuegeshea ni vyema palizi ikaachwa ili kuepuka kuumiza matunda.[/FONT]  § [FONT=&amp]Kumwagilia maji:[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa kawaida nyanya hutoa mazao mengi wakati wa kiangazi kuliko wakati wa mvua za masika.Mwagilia maji ya kutosha mara 2 kwa siku hasa wakati matunda ya kwanza yanapoanza kutunga. Kumwagilia maji mengi kupita kiasi au kidogo sana husababisha matunda yawe na hitilafu ya kupasuka.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kuweka mbolea ya kukuzia:(top dressing).[/FONT]

  [FONT=&amp]Mbolea zenye nitrogeni ndio hutumika kwa kukuzia,mfano S/A,UREA au CAN na hutumika wiki 2 – 4 tangu kupandikiza miche kwani inakuwa tayari na mizizi mipya itakayonyonya mbolea hiyo. [/FONT]

  [FONT=&amp]Mbolea hii ya kukuzia huwekwa mara 2. Mara ya kwanza weak gramu 5 kwa kila mmea za SA au CAN. Rudia tena wakati inaanza kutoa matunda.[/FONT]

  [FONT=&amp]Muhimu:[/FONT]
  [FONT=&amp]Kiwango cha nitrogeni kinatakiwa kidhibitiwa na kurekebishwa ili kitumike kiasi kile tu kinachohitajika vinginevyo mimea itakuwa na majani mengi sana yenye afya bila matunda na itachelewa kukomaa na kuiva kwa matunda.[/FONT]


  [FONT=&amp]VIII. MAGONJWA:[/FONT]

  [FONT=&amp]Nyanya ni zao ambalo hushambuliwa sana na magonjwa mbalimbali.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Magonjwa ya ukungu (Early blight):[/FONT]
  [FONT=&amp] Ambukizo[/FONT][FONT=&amp]:- Fungusi aitwae Altenaria solani.[/FONT]

  [FONT=&amp]Dalili:[/FONT]
  [FONT=&amp]Majani: Kingo za majani huwa na madoa ya rangi nyeusi iliyochanganyika na kahawia, pembe zake huwa za njano.[/FONT]

  [FONT=&amp]Shina: Huwa na madoa kama ya kwenye majani lakini makubwa na kusambaa zaidi.Baadaye madoa hupanuka na kuwa mabaka makubwa ya rangi nyeusi, makavu na yaliyodidimia,shina huwa jembamba, usawa wa ardhi na hudumaa na huvunjika kwa urahisi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Matunda: Huwa na madoa meusi ya mviringo yenye umbo la yai.Madoa huonekana zaidi kwenye kikonyo cha tunda na kwenye sehemu iliyopasuka. Kadri tunda linavyozidi kuiva madoa haya huongezeka zaidi.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Bakajani (late blight[/FONT][FONT=&amp])[/FONT]
  [FONT=&amp] Ambukizo: Phytophthora Infestans.[/FONT]
  [FONT=&amp]Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana kwenye jani la chini. Majani na shina huwa na mabaka makubwa yenye rangi nyeusi au kahawia nzito. Katika hali ya unyevunyevu, majani huoza na hatimaye uyoga mweupe huonekana chini ya jani. [/FONT]

  [FONT=&amp]Baadaye majani huakuaka na kuwa yameunguzwa na moto. Matunda yaliyopatwa na ugonjwa huu huwa madoa ya rangi ya kijani iliyochanganyikana na kahawia. Baadaye huwa makubwa na kuoza, ukipasua tunda lilooza utaona weusi. Nyanya zenye ugonjwa huu zikihifadhiwa kwenye sehemu zenye unyevunyevu, hutoa uyoga mweupe.[/FONT]

  [FONT=&amp]Jinsi unavyoambukizwa na kuenea:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Ukungu wa ugonjwa huu hutokea kwenye majani ama shina huambukizwakutoka mmea hadi mmea kwa njia ya upepo, mvua na umwagiliaji wa majai ya mashambani.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia Ugonjwa wa Bakajani[/FONT][FONT=&amp]:-[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kubadilisha mazao, usipande nyanya katika eneo moja mfululizo.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kuweka matandazo shambani[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kupunguzia matawi na kuondoa majani yaliyoshambuliwa.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kung'oa masalia yote shambani mara baada ya kuvuna na kuchoma moto.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Sia mbegu katika kitalu kilichotayarishwa vizuri.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia mbegu bora ambazo hazijashambuliwa na ugonjwa.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha aina ya nyanya zinazovumilia mashambulizi ya ugonjwa huu.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia dawa za ukungu kama vile Dithane M-45, Ridomil, Tposin M70, Copper Oxichloride (Cipro), Cupric Hydroxide, (Champion)[/FONT]

  § [FONT=&amp]Mnyauko Bakteria:- (Bacteria Wilt)[/FONT]

  [FONT=&amp] Ambukizo:- Pseudomonas Solanacerium[/FONT]
  [FONT=&amp] Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla bila kuwa njano hasa wakati wa jua kali na njano. Baadaye mmea hudumaa majani na vikonyo vyake hukunjamana, shina likikatwa karibu na usawa wa ardhi rangi ya kahawia nzito huonekana kwenye sehemu ya kusafirishia maji.[/FONT]
  [FONT=&amp]Sehemu iliyokatwa ikiwekwa kwenye maji uji mzito kama maziwa huchuruzika.[/FONT]

  [FONT=&amp]Jinsi ugonjwa unavyoambukizwa na kuenea:-[/FONT]

  [FONT=&amp]Ugonjwa huu huwa katika udongo na kujitokeza zaidi wakati wa joto na pale ardhi ikiwa na unyevenyevu. Huweza kuishi ardhini muda mrefu katika masalia ya mimea ya nyanya na kushambulia mimea mingine. Ugonjwa ukishakuwepo ardhini huenea haraka kwa njia ya umwagiliaji maji na maji ya mvua kufuata mteremko wa ardhi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Pia huenezwa toka mmea hadi mmea kwanjia ya mizizi kugusana.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia ugonjwa:-[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha mbegu kwenye kitalu ambacho hakina ugonjwa huu.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Epuka kupanda nyanya kwenye sehemu ambayo ina ugonjwa huu.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Badilisha mazao shambani[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha nyanya zinazostahimili ugonjwa huu.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ng'oa na choma moto mimea yote iliyoathirika na usipande tena nyanya au jamii yake kwa kipindi cha miaka 4- 5.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Mnyauko Fuzari ( Fuzarium Wilt[/FONT][FONT=&amp])[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni ugonjwa wa ukungu. Husababisha majani kuwa rangi ya njano na mimea kunyauka hasa wakati wa jua kali, majani yaliyoshambuliwa huvunjika kwa urahisi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kama[/FONT][FONT=&amp] shina likinyofolewa karibu na usawa wa ardhi rangi ya kahawia huonekana.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mmea: Hunyauka ----- huwa njano --- hufa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia ugonjwa:[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kung'oa mimea iliyoshambuliwa na kuichoma moto.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha aina ya nyanya zenye ukinzani kama vila Roma, VFM, n.k.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia dawa kama vile Topsin M70, dawa inyunyiziwe kwenye udongo.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Batobato (Tomato Mosaic Virus)[/FONT]

  [FONT=&amp]Husababishwa na virusi. Hushambulia majani machanga na yaliyozeeka. Majani yaliyoshambuliwa hukunjamana na kudondoka. Hali kadhalika majani yaliyozeeka huvunjika kwa urahisi na huwa na rangi nyeusi, kijivu au kikahawia china ya jani. Mwisho majani kuhakauka na kufa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Zuia ugonjwa kwa yafuatayo:-[/FONT]

  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Epuka kuotesha nyanya kwenye eneo lililoathirika[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ng'oana choma moto mimea yote iliyoshambuliwa.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha mbegu zilizodhibitishwa kitaalamu[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Epuka kuhudumia mimea mingine baada ya kuhudumia ile iliyoathirika. osha mikono kabla ya kuhudumia mingine.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Safisha vifaa vyote kama vile visu, mikasi kwa maji na sabuni baada ya kuvitumia.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Usivute sigara ndani ya shamba la nyanya.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha aina ya nyanya zinazostahimili magonjwa ya batobato.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Ugonjwa wa madoa jani (Septoria leaf spot)[/FONT]

  [FONT=&amp]Husababishwa na ukungu na kushambulia majani na kuwa na madoa meusi na kingo zake huwa na rangi ya kijivu iliyoambatana na madoa meusi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Nyunyiza dawa za ukungu kama vile Dithane M45, Blitox na Coper fungicides.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Scleretonia Rot:[/FONT]
  [FONT=&amp] Ambukizo:[/FONT]
  [FONT=&amp] Ni mdudu aina ya fungusi aitwaye sleratinia scerotirum.[/FONT]


  [FONT=&amp]Dalili za ugonjwa:-[/FONT]

  [FONT=&amp]Muozo mwepesi katika shina ikifuatiwa na unyaukaji wa ncha za mmea na matawi. Wakati wa unyevunyevu, viini vyeupe vya fungusi hutokea katika sehemu zilizoshambuliwa na ugonjwa. [/FONT]

  [FONT=&amp]Viini vikubwa vya ugonjwa vigumu na vyenye rangi nyeusi huwepo ndani ya mmea ulioshambuliwa na kisha mmea mzima hunyauka na kufa au hukauka.[/FONT]  [FONT=&amp]Jinsi unavyoambukiza na kuenea:[/FONT]
  [FONT=&amp]Fungusi wa ugonjwa wana uwezo wa kuishi ardhini kwa muda mrefu. Nyakati za baridi na unyevunyevu wale waliokuwa usawa wa ardhi huzaana kwa wingi na kisha kupeperushwa na upepo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ugonjwa unaambukizwa pale ambapo maua makavu na majani yenye ugonjwa yakigusana na sehemu za mimea isiyo naugonjwa. Ugonjwa huu hutokea zaidi wakati wa mvua, baridi na nyakati za ukungu na umwagiliaji ndipo ugonjwa huenea zaidi. Mimea mingi ilimwayo na majani hushambuliwa sana na ugonjwa huu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia dawa za aina ya fungicide.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Epuka kupanda mimea katika eneo lililoshambuliwa sana na ugonjwa hasa wakati wa baridi.[/FONT]

  [FONT=&amp]HITILAFU ZA MATUNDA[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kupasuka matunda[/FONT][FONT=&amp]:[/FONT]
  [FONT=&amp] Kuna aina mbili za mipasuko; mpasuko wa mviringo na mpasuko wa nyota.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mpasuko wa mviringo[/FONT][FONT=&amp]:[/FONT]

  [FONT=&amp]Hutokea wakati mmea haukupata maji ya kutosha hasa wakati wa jua kali. Wakati huu maji yaliyoko kwenye tunda hayawezi kulingana na maji yanayopotea angani kama mvuke.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mpasuko wa umbo la nyota[/FONT][FONT=&amp]:[/FONT]

  [FONT=&amp]Hutokea hasa tunda linapokuwa na maji mengi na wakati huo unyevu angani ni mwingi sana. Hivyo tunda hushindwa kupoteza maji kwa njia ya mvuke na hupasuka kabla ya kukomaa. [/FONT]
  [FONT=&amp]Hutokea zaidi kwenye nyanya aina ya Marglobe. Mpasuko wa mviringo na umbo la nyota huzuiwa kwa kumwagilia maji ya kutosha.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Kuoza kitako:[/FONT]

  [FONT=&amp]Vidonda vyeusi vilivyodidimia huonekana kwenye kitako cha tunda. Sehemu hii baadaye hunyauka na ngozi huwa nyeusi. Hali hii hutokea zaidi wakati wa jua kali na katika sehemu zenye udongo wenye chumvichumvi na tindikali nyingi. Zuia hali hii kwa kuhakikisha udongo una unyevunyevu wa kutosha wakati wote. Pia epuka kuweka mbolea nyingi za chumvichumvi.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Mabaka ya matunda:[/FONT]

  [FONT=&amp]Matunda yaliyopigwa na jua kali huwana mabaka hasa sehemu za ubavuni. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kuepuka kupunguza matawi mengi kwa wakati mmoja.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Matunda ya kijani kibichi:[/FONT]

  [FONT=&amp]Mabega ya tunda huwa na kijani kibichi. Hitilafu hii hutokana na chanikiwiti kuwa nyingi na hutokea hasa wakati wa jua kali. Ili kuepuka hali hii unashauriwa kutoweka mbolea nyingi ya chumvichumvi na punguza mwanga wa jua kufunika matunda na majani makavu.[/FONT]

  [FONT=&amp]WADUDU WAHARIBIFU[/FONT]

  § [FONT=&amp]Funza wa vitumba (AmericanBollworm)[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni funza watokanao na aina Fulani ya nondo. Wana rangi ya kijani hutokea baada ya mayai ya nondo kuanguliwa, kisha hutoboa matunda na kuishi humo. Jinsi wanavyokula na kukua husababisha matunda kuoza. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia[/FONT][FONT=&amp]:- Nyunyiza dawa za Carbarly, Dimethiote , Sumucidin na Dichlorvos.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Utitiri (Red spider mites)[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni wadudu wadogo sana na wenye rangi ya machungwa, nyekundu au kahawia. Vijidudu hivi hushambulia kwa kufyonza utomvu chini ya majani. Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya njano, hukunjamana, hukauka na hatimaye mmea hufa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT][FONT=&amp] Tumia dawa aina ya Morestan, Kelthane, Dimethoate, Diazinon, Ekalux, Poltrin na Profenofos.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Vidukari/wadudu mafuta (Aphids)[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni wadudu wadogo wenye rangi ya kijani, nyeusi au kahawia. Baadhi wana mabawa wengine hawana. Hufyonza utomvu wa majani na kusababisha mmea ulioshambuliwa kudhoofika, kudumaa, majani kunyauka na hatimaye kukauka.[/FONT]


  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Tumia Dimecron, Actellic 50 Ec, Selecron, Sumicidin, Karate, Dichlorvos na Dimethoate.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Minyoo fundo:[/FONT]

  [FONT=&amp]Wadudu wadogo weupe ambao hawaonekani kwa macho na huishi kwenye udongo. Hushambulia mizizi na kusababisha mimea kudhoofika na kushindwa kutoa matunda. Pia husababisha matunda kuiva kabla ya kukomaa. Uking'oa mmea ulioshambuliwa utaona mizizi ina vinundunundu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Tumia mzunguko wa mazao kwenye enneo moja.[/FONT]
  [FONT=&amp]Baada ya kuvuna nyanya zao litakalofuata lisiwe la jamii ya nyanya, mfano Hoho, bilinganya.[/FONT]
  [FONT=&amp]Kama madhara ni makubwa sana tumia dawa ya Furadan, na dawa za kufukiza ardhini kama Curaterr, Dazomet.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kumbuka:-[/FONT][FONT=&amp] Kumwagilia kwa kutumia mifereji kunaweza kusambaza minyoo shambani.[/FONT]

  [FONT=&amp]SOMO LA PILI[/FONT]
  [FONT=&amp]USTAWISHAJI WA ZAO LA KABICHI[/FONT]

  [FONT=&amp]I. UTANGULIZI:[/FONT]

  [FONT=&amp]Zao la kabichi hulimwa katika mikoa ya Morogoro, Arusha,Tanga, Iringa, Kilimanjaro na Mbeya.[/FONT]
  [FONT=&amp]Kama mboga zao la kabichi lina viini lishe kama chokaa, protini, kambakamba na maji kwa wingi. Hutumika kutengeneza kachumbari, pia kuchanganywa na nyama au maharage.[/FONT]

  [FONT=&amp]II.HALI YA HEWA[/FONT]

  [FONT=&amp] Zao la kabichi hupendelea:-[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]hali ya ubaridi [/FONT]
  [FONT=&amp]Mwinuko[/FONT][FONT=&amp]: Kuanzia mita 1200 hadi 1900 kutoka usawa wa bahari.[/FONT]
  [FONT=&amp]Udongo[/FONT][FONT=&amp]: - - Tifutifu [/FONT]
  [FONT=&amp] - Rutuba nyingi na [/FONT]
  [FONT=&amp] - Unaohifadhi unyevu kwa muda mrefu[/FONT]
  [FONT=&amp] - Usiotuamisha maji[/FONT]
  [FONT=&amp] - Usio na chumvichumvi nyingi.[/FONT]
  [FONT=&amp] - Kama hauna rutuba ya kutosha ongeza mbolea ya samadi [/FONT]
  [FONT=&amp] au mbolea vunde.[/FONT]

  [FONT=&amp]III. AINA ZA KABICHI[/FONT]
  · [FONT=&amp]Early Jersey Wakefield[/FONT][FONT=&amp]: [/FONT]
  [FONT=&amp]- Umbo lilochongoka kidogo, [/FONT]
  [FONT=&amp]- Hufunga vizuri,[/FONT]
  [FONT=&amp]- Uzito ni kati ya kilo 1.5 hadi 2.0,[/FONT]
  [FONT=&amp]- Hukomaa mapema siku 90 – 100 tangu kupandikiza.[/FONT]

  · [FONT=&amp]Copenhagen[/FONT][FONT=&amp] Market[/FONT][FONT=&amp]:[/FONT]
  [FONT=&amp]- Vichwa vya mviringo na hupasuka kirahisi[/FONT]
  [FONT=&amp]- Hukomaa mapema, siku 90 – 100 tangu kupandikiza[/FONT]

  · [FONT=&amp]Prize Drumhead[/FONT][FONT=&amp]: [/FONT]
  [FONT=&amp]- Vichwa vikubwa (kilo 2- 2.5),[/FONT]
  [FONT=&amp]- Vichwa ni bapa, huchelewa kukomaa (siku 110 – 120)[/FONT]
  [FONT=&amp]- Huvumulia hali ya jua kali, [/FONT]
  [FONT=&amp]- Pia vichwa hupasuka.[/FONT]

  · [FONT=&amp]Oxheart: [/FONT]
  [FONT=&amp] - Vichwa vidogo huchongoka kama moyo, [/FONT]
  [FONT=&amp] - Hupendwa sana na walaji,[/FONT]
  [FONT=&amp] - Ladha yake ni tamu, hukomaa mapema, [/FONT]
  [FONT=&amp] - Hazina tabia ya kupasuka.[/FONT]

  · [FONT=&amp]Glory of Enkhuizen: [/FONT]
  [FONT=&amp]- Vichwa vya mviringo,[/FONT]
  [FONT=&amp]- Huvumilia hali ya jua kali, [/FONT]
  [FONT=&amp]- Huchelewa kukomaa (siku 110 – 120)[/FONT]
  [FONT=&amp]- Ina tabia ya kupasuka.[/FONT]

  [FONT=&amp]IV. KUOTESHA MBEGU:[/FONT]

  [FONT=&amp]Mbegu za kabichi huoteshwa kitaluni na baadaye huhamishiwa shambani. Andaa kitalu vizuri na weka mbolea za asili zilizooza vizuri kwa kiasi cha ndoo 5 – 10 za ujazo wa kilo 20 kwenye eneo la mita za mraba 10. Changanya na udongo kisha lainisha udongo kwa kuvunja mabonge makubwa kwa kutumia reki.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tengeneza tuta lililoinuka kwa sentimita 25 na lenye upana wa mita 1. Mwagilia maji kwenye tuta siku moja kabla ya kusia mbegu. Kiasi cha mbegu zinazohitajika ni gramu 1 kwenye eneo la mita 1 ya mraba hivyo hekta 1 huhitaji gramu 200 – 300. [/FONT]

  [FONT=&amp]Sia katika umbali wa sentimita 15 toka mstari hadi mstari na kina cha nusu sentimita.Funika mbegu na udongo laini kasha tandaza nyasi kazu ili kuhifadhi unyevu.Mwagilia maji kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu ziote, huota kwa muda wa siku 5 – 10.[/FONT]

  [FONT=&amp]V.KUTAYARISHA SHAMBA[/FONT]

  [FONT=&amp] - Shamba litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupandikiza.[/FONT]
  [FONT=&amp] - Katua ardhi kwa kina cha sentimita 30[/FONT]
  [FONT=&amp] - Lainisha udongo na tengeneza matuta[/FONT]
  [FONT=&amp] - Weka mbolea za asili kwa kiasi cha ndoo 2 kwa kila hatua moja au[/FONT]
  [FONT=&amp] - Mbolea iwekwe kwa kila shimo kwa kiasi cha kilo kwa shimo.[/FONT]
  [FONT=&amp] - Mbolea ya N.P.K. 5:15:5 yaweza kuwekwa kwa kiasi cha kijiko 1 cha[/FONT]
  [FONT=&amp]chai chenye gramu 5 kwa kila shimo.[/FONT]

  [FONT=&amp]VI.KUPANDIKIZA MICHE[/FONT]

  [FONT=&amp]Miche huwa tayari kupandikizwa shambani baada ya wiki 3 – 5 tangu kusia mbegu . Miche huwa na urefu wa sentimita 15 – 20.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ng'oa miche kwa uangalifu na pandikiza kama ilivyokuwa kitaluni na hakikisha mizizi haipindi wakati wa kupandikiza.[/FONT]

  [FONT=&amp]Nafasi ya kupandikiza: [/FONT]

  [FONT=&amp]Hutegemea aina ya kabichi [/FONT]
  [FONT=&amp]– [/FONT][FONT=&amp]zenye vichwa vikubwa (Drumhead) ni sentimita 60 kutoka mche hadi mche na sentimita 75 toka mstari hadi mstari.[/FONT]
  [FONT=&amp]– [/FONT][FONT=&amp]Zenye vichwa vidogo (Oxheart) ni sentimita 40 – 50 kutoka mche hadi mche na sentimita 60 toka mstari hadi mstari.[/FONT]
  [FONT=&amp]– [/FONT][FONT=&amp]Umbali toka tuta moja na jingine ni sentimita 60.[/FONT]
  [FONT=&amp]– [/FONT][FONT=&amp]Muda mzuri wa kuotesha ni asubuhi au jioni[/FONT]
  [FONT=&amp]– [/FONT][FONT=&amp]Baada ya kupandikiza weka matandazo kama vile nyasi kavu ili kuhifadhi unyevu na kuzuia magugu kuota kwa urahisi.[/FONT]

  [FONT=&amp]VII. PALIZI[/FONT]

  [FONT=&amp]Zao la kabichi halina mizizi ya kina kirefu hivyo wakati wa palizi ni muhimu kuwa mwangalifu kwa kupalilia juu juu ili kuepuka kukata mizizi. Kuongeza matandazo husaidia kupunguza palizi a mara kwa mara..[/FONT]

  [FONT=&amp]VIII. UMWAGILIAJI[/FONT]

  [FONT=&amp]Kabichi hustawi vizuri zaidi iwapo kuna maji ya kutosha kwenye udongo. Mwagilia mara mbili au zaidi kwa wiki kutegemea hali ya hewa na aina ya udongo. [/FONT]

  [FONT=&amp]Kabichi ambazo hazikupata maji ya kutosha huchelewa kufunga na huwa na vichwa vidogo. Zikikosa maji kwa muda mrefu na zikapata maji mengi ghafla, vichwa hupasuka.[/FONT]

  [FONT=&amp]IX. MBOLEA[/FONT]

  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Mbolea ya kukuzia (S/A) huwekwa baada ya 4 – 6 baada ya kupandikiza miche na kabla ya vichwa havijaanza kufunga.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kiasi cha kilo 80 huhitajika kwa eka moja.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kilo 40 ziwekwe baada ya wiki 4 – 6 na kilo 40 ziwekwe tena baada ya mwezi mmoja[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Mche mmoja huhitaji kiasi cha kidogo cha gramu 5[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Mbolea iwekwe kuzunguka shina umbali wa sentmita 10 – 15 kutoka kwenye shina.[/FONT]

  [FONT=&amp]Muhimu:[/FONT][FONT=&amp] Epuka kuweka mbolea nyingi, kwani husababisha vichwa visifunge vizuri (kabichi zinakuwa nyepesi)[/FONT]

  [FONT=&amp]x. KUBADILISHA MAZAO[/FONT] [FONT=&amp]Kabichi nizao linalotumia virutubisho vingi kulinganisha na mboga nyingine,hivyo kabla ya kuotesha kabichi panda mazao jamii ya mikunde ili kuongeza rutuba.[/FONT] [FONT=&amp]Baada ya kuvuna kabichi otesha mazao yanayotumia chakula kidogo kama vile karoti, radishi au lettuce. Kubadilisha mazao pia hupunguza kuenea kwa wadudu waharibifu na magonjwa.[/FONT]

  [FONT=&amp]XI. WADUDU WAHARIBIFU[/FONT] · [FONT=&amp]Viwavi wa kabichi:[/FONT] [FONT=&amp]Hawa ni viwavi wenye rangi ya kijani na alama ya mstari wa kung'aa mgongoni. Nondo hutaga mayai chini ya jani na baada ya kuanguliwa viwavi hawa hula sehemu ya chini ya jani na kucha ngozi nyembamba mfano wa dirisha la kioo. Ni muhimu kuwadhibiti viwavi hawa kwa sababu ndio wanaoleta madhara makubwa.[/FONT] [FONT=&amp]Viwavi wa kabichi huzuiwa kwa kunyunyizia moja ya dawa zifuatazo:- Nogos, Permethrin,Dimethoate, Sevin W.P. na Sumicidin.[/FONT]
  [FONT=&amp]Nzi wa Kabichi:[/FONT] [FONT=&amp]Mashambulizi hufanywa na kiluwiluwi mwenye rangi ya kijani au bluu. Hula majani yote ya kabichi na kubakisha vena au vishipa vya majani.[/FONT] [FONT=&amp]Inzi wa kabichi wanaweza kuzuiwa kwa kutumia dawa za Sevin, Dimethoate, Permethrin na Fenvalerate(sumicidin)[/FONT]

  [FONT=&amp]Sota:[/FONT] [FONT=&amp]Hawa ni funza wakubwa wenye rangi ya kijivu. Hupendelea kujichimbia katika udongo wakati wa mchana na kukata miche michanga karibu na usawa wa ardhi wakati wa usiku.[/FONT] [FONT=&amp]Zuia wadudu hawa kwa kutumia majivu au dawa kama vile Carbaryl, Fenvalerate au Decis mara baada ya kuotesha. Kama mche utakatwa, mtoe mdudu huyu kwa kumfukua na kumuua. Kisha pandikiza mche mwingine.[/FONT]
  [FONT=&amp]Vidukari au wadudu mafuta:[/FONT] [FONT=&amp]- Wadudu hawa ni wadogo sana wenye rangi ya kijani,[/FONT] [FONT=&amp] nyeusi au khaki. [/FONT] [FONT=&amp]- Baadhi yao wana mabawa na wengine hawana.[/FONT] [FONT=&amp]- Hufyonza utomvu wa mimea na husababisha majani [/FONT] [FONT=&amp] kubadilika rangi na kuwa meupe au njano iliyopauka.[/FONT] [FONT=&amp]- Mmea hudumaa na hatimaye hukauka.[/FONT] [FONT=&amp]Zuia kwa kunyunyiza mojawapo ya dawa hizi Fenvalerate, Dimethoate, Karate, Nogos.[/FONT]

  [FONT=&amp]Minyoo Fundo:[/FONT] [FONT=&amp]Ni minyoo wadogo wanaoishi ardhini na ambao hawaonekani kirahisi kwa macho. Hushambulia mizizi na kusababisha kabichi kudhoofu na kushindwa kufunga vizuri. Mimea iliyoshambuliwa, mizizi yake huwa na nundunundu.[/FONT]
  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Matumizi ya mbolea za asili kila msimu husaidia kupunguza kuzaliana kwa wadudu hao.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia mzunguko wa mazao, usiotesha zao la jamii ya kabichi baada ya kuvuna kama vile kabichi ya kichina, koliflawa,n.k Otesha mboga kama vile karoti, radishi, vitunguu au mahindi.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ondoa masalia yote shambani ambayo yanaweza kueneza wadudu hawa na yachome moto.[/FONT]

  [FONT=&amp]XII. MAGONJWA[/FONT][FONT=&amp]:[/FONT] · [FONT=&amp]Kuoza shingo[/FONT][FONT=&amp]:-[/FONT] [FONT=&amp] - Husababishwa na vidudu vya bacteria ambavyo viko [/FONT] [FONT=&amp] kwenye udongo. [/FONT] [FONT=&amp]- Hushambulia kabichi na kuzifanya zibadilike rangi.[/FONT] [FONT=&amp]- Kuoza na kutoa harufu mbaya.[/FONT] [FONT=&amp]- Vidudu vidovidogo huonekana pia kwenye sehemu iliyooza.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Epuka kujeruhi kabichi wakati wa kuvuna[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Vuna kabichi wakati hakuna mvua[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Usilundike kwa wingi na kwa muda mrefu.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Hifadhi kwenye sehemu yenye ubaridi na hewa ya kutosha.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ng'oa masalia, choma moto na lima shamba mara moja baada ya kuvuna[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia mzunguko wa mazao.[/FONT] ·

  [FONT=&amp]Uozo Mweusi:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]husababishwa na Bakteria[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Majani hugeuka kuwa njano na baadaye kuwa kahawia[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Majani huanza kunyauka kutoka kwenye kingo zake na kuacha alama ya "V" yenye rangi nyeusi isiyokolea.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Baadaye majani hunyauka na kupukutika[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kama[/FONT][FONT=&amp] ukikata jani au shina, mviringo mweusi huonekana kwenye vena.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Badilisha mazao. Usipande kabichi au jamii yake kwa muda wa miaka 2 kwenye eneo lililoadhirika.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha kabichi kwenye sehemu ambayo haituamishi maji.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Kitalu na mazingira yake viwe safi daima.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Punguza miche ili kupunguza msongamano.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ondoa masalia yote baada ya kuvuna ya yachomwe moto.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha mbegu zilizodhibitishwa na wataalam.[/FONT]

  · [FONT=&amp]Kuoza shina:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ni ugonjwa waukungu[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Madoadoa yaliyodidimia yenye rangi ya kahawia huonekana kwenye shina karibu na usawa wa ardhi, ikifuatiwa na kuvimba kwa shina.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Baadaye uyoga mweusi huonekana kwenye uvimbe huo.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Uozo wa rangi ya kahawia huonekana ndani ya shina.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Majani huwa na madoa meusi ya mviringo yaliyozungukwa na uyoga mweusi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Otesha kabichi sehemu ambayo haituamishi maji[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Badilisha mazao, usioteshe kabichi kwenye eneo lililoathirika kwa muda wa miaka 3.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Lima[/FONT][FONT=&amp] shamba mara baada ya kuvuna ili kuwezesha masalia kuoza haraka kabla ya kuotesha tena.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ondoa kabichi zote zilizoshambuliwa shambani.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia dawa ya kuzuia ukungu kama vile Ridomil.[/FONT]

  · [FONT=&amp]Uvimbe wa mizizi:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Husababishwa na ukungu[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Hushambulia mizizi na dalili zake ni kudumaa kwa mmea na majani kukunjamana[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Baadae mmea huoza
  [/FONT] [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT][FONT=&amp] Badilisha mazao shambani.[/FONT] ·

  [FONT=&amp]Madoa Meusi:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Chanzo ni ukungu.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Majani huwa na madoa madogo madogo ya mviringo yenye rangi ya njano .[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Baadae madoa huwa makubwa na hugeuka kuwa meusi.[/FONT]
  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Badilisha mazao[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Hakikisha shamba ni safi wakati wote[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ikibidi tumia dawa za ukungu kama vile Kocide,Cupro, n.k.
  [/FONT] · [FONT=&amp]
  Ubwiri Vinyoya[/FONT]
  [FONT=&amp]:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Ni ugonjwa wa ukungu.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Hupendelea hali ya unyevunyevu na baridi kali.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Huanzia kwenye kitalu[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Mabaka ya mviringo yenye rangi ya njano huonekana upande wa juu wa jani.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Baadae hubadilika na kuwa rangi ya zambarau iliyochanganyika na nyeupe upande wa chini wa majani.[/FONT]
  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia mzunguko wa mazao.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Hakikisha udongo hautuamishi maji na kitalu ni kisafi wakati wote.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Tumia za ukungu kama Zineb, Didhane, M45, Kocide, Topsin-M na Ridomil.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuoza shinaau Kinyaushi:-[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Husababishwa na ukungu.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Hushambulia miche michanga[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Miche iliyoshambuliwa huonyesha dalili za kukauka.[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Miche mikubwa huonyesha dalili za kudumaa[/FONT] [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Sehemu ya shina iliyo karibu na ardhi hulainika na kuwa rangi ya kahawia.[/FONT] [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT] [FONT=&amp] -Punguza miche kama imesongamana.[/FONT] [FONT=&amp] -Nyunyiza dawa ya ukungu Kama Didhane M-45, Ridomil, Topsin-M.[/FONT]

  [FONT=&amp]XIII. KUVUNA [/FONT] [FONT=&amp]Kabichi hukomaa katika siku 60 mpaka 210 tangu kupandikiza miche. Hata hivyo muda wa kukomaa hutegemea ain aya kabichi.Uvunaji hufanyika kwa kukata shina sentimita 2 – 3 kutoka kwenye kichwa kwa kutumia kisu.[/FONT] [FONT=&amp]Ondoa majani ya nje na acha majani 2 au 3 ya kijani kwa ajili ya kuzuia kabichi zisikwaruzike na kuoza wakati wa kusafirisha. Punguza urefu wa majani ili kurahisisha ufungaji.[/FONT] [FONT=&amp]Ni muhimu uvunaji ufanyike asubuhi au jioni. Ondoa kabichi zilizooza au kuharibika wakati wa kuvuna, kisha panga zilizobaki kufuata daraja kama vile ndogo, za kati na kubwa.
  [/FONT] [FONT=&amp]Mavuno:[/FONT][FONT=&amp]- Kiasi cha tani 40 au zaidi za kabichi hupatikana kwa hekta moja kama zao limetunzwa vizuri.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]XIV. HIFADHI[/FONT] [FONT=&amp]Kabichi ni zao linaloharibika kwa haraka, hivyo halina budi kutumika mapema iwezekanavyo baada ya kuvuna. Kabichi kwa ajili ya kuuzwa zisafirishwe mara moja kwa walaji. Kama usafiri ni mgumu, zihifadhiwe kwenye sehemu yenye ubaridi na hewa ya kutosha.[/FONT] [FONT=&amp]Wakati wa kusafirisha, ziwekwe kwenye matenga au visanduku vya mbao vilivyo na matundu yanayoingiza hewa ya kutosha.[/FONT]
  [FONT=&amp]SOMO LA TATU[/FONT]
  [FONT=&amp]UZALISHAJI WA ZAO LA VIAZI MVIRINGO[/FONT]

  [FONT=&amp]I. UTANGULIZI:[/FONT]
  [FONT=&amp]Viazi mviringo au kwa jina jingine viazi ulaya ni jina ambalo hutumika kutofautisha zao hili na zao la viazi vitamu. Zao hili ni muhimu kati ya mazao ya mizizi katika maeneo ya miinuko ya Afrika mashariki.[/FONT]

  [FONT=&amp]Katika maeneo ya miinuko zaidi, zao hili huwa na mavuno makubwa zaidi kwa zao la mahindi na hukua kwa kipindi cha mwaka mmoja.[/FONT]

  [FONT=&amp]Viazi mviringo hutumika sana kama zao kuu la chakula hapa nchini na pia husafirishwa katika maeneo ya mbali kama vila Kampala, Mombasa na Dar,es salaam.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hapa Tanzania viazi mviringo kuzalizwa katika maeneo yenye miinuko ya kaskazini kama vile Moshi, Arusha, Lushoto na meneo ya kusini yenye miinuko kama vile Njombe mkoani Iringa na wilaya za mkoa wa Mbeya.Pia maeneo ya Morogoro yenye miiunuko hususani Tarafa ya Mgeta yameonekana kuweza kuzalisha zao hili kwa wingi.[/FONT]

  [FONT=&amp]II. MMEA WA KIAZI ULIVYO[/FONT]

  [FONT=&amp]Kiazi ni mzizi wa mmea unaovimba ukiwa chini ya ardhi na kuwa na vijicho vingi, ambavyo baada ya miezi 2 – 3 vijicho hivi huchipua na kuota shina, kijicho kimoja huweza kutoa zaidi ya shina 1 ambapo hutoa vitawi vingine.[/FONT]

  [FONT=&amp]Pingili zilizopo kwenye shina hutoa mizizi inayomea chni ya ardhi na miisho yake huvimba na kuwa kiazi. Viazi nyenye ngozi nyeupe huwa na maua meupe na ileyenye rangi hutoa maua ya rangi aidha pinki, bluuau zambarau.Katika mzunguko wa ukuaji kiazi huendelea kukua hata baada ya maua kutoka; ili mradi kuwe na na unyevunyevu wa kutosha kwenye udongo na yasiwepo magonjwa.[/FONT]

  [FONT=&amp]II. HALI YA HEWA[/FONT]

  [FONT=&amp]Mvua:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Viazi huhitaji mvua za kiasi cha sentimita 25 kwa wiki ambazo hutakiwa kuendela kwa muda wa miezi 3 .5 hii huweza kukuza viazi na kupata mavuno mazuri.[/FONT]


  [FONT=&amp]Joto:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Viazi hukua vizuri zaidi kwenye baridi kwa mwinuko wa mita 1,800 kulikoni kwenye joto. Maeneo machache ya mwinuko wa mita 1,500 huweza kukuza viazi, japo pia hukua kwenye mwinuko wa mita 2,900.[/FONT]
  [FONT=&amp]Udongo:-[/FONT]

  [FONT=&amp]Viazi hutoa mavuno mazuri kwenye udongo usiokuwa mzito na unaopitisha maji kwa urahisi. Udongo wenye viini lishe vya kutosha au kuongeza samadi na mbolea za viwandani.[/FONT]

  [FONT=&amp]IV. AINA ZA VIAZI[/FONT]

  [FONT=&amp]Aina zote za viazi zimeingizwa Afrika Mashariki kutoka Ulaya ambako huzalishwa kwa wingi.[/FONT]


  1. [FONT=&amp]Dutch Robijn [/FONT][FONT=&amp] - kutoka Holland[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]ndani ni njano[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]inavumilia kidogo ugonjwa wa ukungu[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]hushambuliwa sana na Mnyauko Bakteria[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]hupendwa na walaji wengi[/FONT]

  [FONT=&amp] ii. Roslin [/FONT][FONT=&amp] - kutoka Scotlland[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]ngozi yake ni nyeupe[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]ndani ni nyeupe[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]huvumulia ugonjwa wa ukungu[/FONT]

  [FONT=&amp] iii. Kerr's Pink[/FONT][FONT=&amp] - ngozi yake ni nyeupe au nyekundu[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]ndani ni nyeupe[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]hushambuliwa sana na ukungu na Mnyauko Bakteria[/FONT]

  [FONT=&amp]iv. Atzimba [/FONT][FONT=&amp] - kutoka Mexico[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]huvumilia ugonjwa wa ukungu[/FONT]

  [FONT=&amp]V. MBEGU ZAKUZALISHA VIAZI[/FONT]
  [FONT=&amp]Viazi vyenye umbile dogo hutumika kama mbegu, hutakiwa kuwa na upana wa sentimita 3 – 6. Kiasi cha robo tatu za tani huhitajika kuotesha ekari 1 sawa na tani 1.85 kwa hekta 1.[/FONT]
  [FONT=&amp]Mbegu hazitakiwi kuhifadhiwa kwenye giza nene kwani zitaanza kutoa vichipukizi virefu vyeupe.[/FONT]

  [FONT=&amp]VI. KUANDAA SHAMBA[/FONT]
  [FONT=&amp]Shamba linatakiwa kuandaliwa vituta vidogo vidogo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka tuta hadi tuta, hiihusaidia kuhifadhi udongo na maji na hutoa nafasi nzuri wakati wa upanukaji wa viazi.[/FONT]
  [FONT=&amp]Inashauriwa pia kama matuta hayajatumika basi ni muhimu kujaza udongo kwenye shina kwani pingili za chini kwenye shina ni lazima zifunikwe na udongo ili zitoe viazi kwa wingi na hivyo mavuno huongezeka.[/FONT]

  [FONT=&amp]VII. KUTOSHA VIAZI[/FONT]

  [FONT=&amp]Viazi hutakiwa kuoteshwa mara karibu kabisa na mvua zinapotaka kuanza kuchelewa kuotesha kutapunguza kipindi cha ukuaji wa ile mizizi ili iwe viazi na hivyo kukabiliwa na kipindi cha ukavu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Uoteshaji hufanyika kwa mikono na mbegu ziwekwe chini udongo kwa kina cha sentimita 10. Kama mbegu zitaoteshwa bila matuta basi zioteshwe kwa kina cha sentimita 15 na kufunikwa na udongo mchache na wakati wa palizi udongo utaongezwa ili kuongeza utoaji wa viazi kwa wingi. [/FONT][FONT=&amp]Nafasi ya kuotesha ni sentimita 75 toka mstari hadi mstari na sentimita 23 – 30kwa mche hadi mche.[/FONT]

  [FONT=&amp]VIII. MBOLEA[/FONT]

  [FONT=&amp]Viazi hustawi vizuri zidi kwenye udongo ulioongezwa samadi na ni muhimu chimbiwe katika kina kirefu. Mbolea za viwandani zinazotakiwa ni zile zenye Nitrogeni kwa kiasi cha kilo 22 – 45 kwa ekari; zenye Chokaa P2O5 kwakilo 45 – 65 kwa ekari.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni vyema kuongeza mbolea na samadi wakati kuna mategemeo mazuri ya mavuno kwa kuzingatia kuwa mbegu zilizooteshwa hazina magonjwa ya aina yoyote.[/FONT]

  [FONT=&amp]IX. PALIZI[/FONT]

  [FONT=&amp]Zao la viazi likioteshwa kwa nafasi zilizoshauriwa basi huweza kufunika ardhi yote na hivyo kugandamiza magugu, hii husaidia kwa kipindi cha wiki 6 za mwanzo. Katika mpando wa matuta, basi huwa ni kuondoa magugu na kujaza udongo kwenye mashina.[/FONT]

  [FONT=&amp]X. KUVUNA[/FONT]

  [FONT=&amp]Uvunaji wa viazi hufanyika kwa kutumia jembe la mkono, viazi vikishang'olewa kutoka chini ya udongo visiachwe kwa muda mrefu kwani vitabadilika rangi na kuwa kijani.[/FONT]

  [FONT=&amp]Ili kuifanya ngozi yaviazi kuwa ngumu na isiharibike kirahisi basi mashina yote yanyofolewe wiki 2 – 3 kabla ya kuvuta viazi juu ya udongo. Baada ya viazi kuvunwa haviwezi kuhifadhiwa kwa muda mrefu kwani huanza kuchipua. Viazi huweza kuhifadhiwa kwenye ardhi, lakini si zaidi ya wiki 6 kwani vitakabiliwa na magonjwa na kushambuliwa na minyoo fundo.[/FONT]

  [FONT=&amp]XI. MAVUNO[/FONT]

  [FONT=&amp]Mavuno huwa mengi kama utunzaji wa kitaalamu umezingatiwa ikiwa ni pamoja na kudhibiti magonjwa, kutumia aina zinazostahimili magonjwa. Kiasi cha tani 6 – 8 kwa ekari huvunwa,sawa na tani 15 – 20 kwa hekta.[/FONT]

  [FONT=&amp]KUHIFADHI:[/FONT][FONT=&amp]- [/FONT]
  [FONT=&amp]Uhifadhi wa zao hili ni mgumu, hivyo inashauriwa kuwa sehemu iliyotengwa kwa biashara iuzwe mapema, sehemu ya kutumia nyumbani ihifadhiwe katika banda au ghala safi lenye sakafu, lisilo na unyevu, mwanga wala joto- liwe na hewa safi na ya kutosha. Vinginevyo husababisha viazi kuota haraka. Viazi vilivyowekwa ghalani visilundikwe kwa kina kirefu, visambazwe ili visipate joto.[/FONT]

  [FONT=&amp]XII. WADUDU[/FONT]


  • [FONT=&amp]Vidukari:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Ni wadudu wadogo wanoshambilia majani na mashina kwa: [/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]kufyonza utomvu na kusababisha kunyauka kwa mmea. [/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Majani kujikunja kuelekea juu.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Majani kuwa magumu[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Mimea kudumaa[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Pia hubeba vimelea aina ya virusi ambao huathiri mimea. [/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT][FONT=&amp]Pia hueneza ugonjwa wa virus.[/FONT]

  [FONT=&amp]Tiba:[/FONT][FONT=&amp]- Wakati wa utunzaji wa mbegu za viazi ni muhimu kupiga dawa ya wadudu ili kuepuka kupuliza shambani kwani dawa nyingi itapotea.[/FONT]


  • [FONT=&amp]Nondo wa viazi[/FONT][FONT=&amp]:- [/FONT]
  [FONT=&amp]Wadudu huathiri viazi vilivyooteshwa wakati ambao sio wa msimu wa viazi. Viwavi wanaoanguliwa huingia ndani ya viazi na kusababisha kuoza. Pia huingia ndani ya viazi wakati vikiwa stoo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:- [/FONT]
  [FONT=&amp]- Otesha viazi katika kinachoshauriwa au zaidi ya sentimita 3 kwani kiwavi [/FONT]
  [FONT=&amp]aingiae ndani ya hawezi kuchimba kina kirefu na inulia matuta wakati viazi vinakuwa, hii husaidia kuzuia nondo kutaga mayai.[/FONT]

  [FONT=&amp]- Viazi vyote vilivyochimbwa ni muhimu viwekwe kwenye mifuko na mapema kabla ya alasiri ili kuepuka nondo kutaga mayai.[/FONT]
  [FONT=&amp]- Vikihifadhiwa stoo majani ya aina ya LANTANA CAMARA yaweza kutumika.[/FONT]
  [FONT=&amp]- [/FONT]
  [FONT=&amp]Tiba:- [/FONT][FONT=&amp]Wakati viazi vikiwa stoo, dawa ya unga ya Aldrin hutumika kwenye viazi vya mbegu.[/FONT]
  [FONT=&amp]Nyunyizia majani ya viazi wakati mmea ukiwa na mwezi 1dawa aina ya Dipterex, Diazon, Thiodan, Permethrin, ACtellic au Sumithion.[/FONT]
  [FONT=&amp]Kama ni viazi vya kula basi tumia PYRETHRUM.[/FONT]


  • [FONT=&amp]Minyoofundoo:[/FONT][FONT=&amp]-[/FONT]

  [FONT=&amp]Hushambulia viazi vilivyoachwa kwa muda mrefu ardhini na kwenye ardhi iliyoathirika na mmomonyoko.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT]

  [FONT=&amp]- Usioteshe mbegu ambazo zimeshambuliwa na wadudu.[/FONT]
  [FONT=&amp]- Andaa shamba mapema ili masalia yote ya mazao yaweze kuoza ili [/FONT]
  [FONT=&amp] kutoruhusu makazi ya minyoo fundo. [/FONT]


  • [FONT=&amp]Mbawakavu:-[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni wadudu wadogo ambao hutafuna majani na kuacha matundu matundu.[/FONT]

  [FONT=&amp] Kuzuia: Tumia dawa aina ya Malathion, Thiodan[/FONT]

  [FONT=&amp]MUHIMU:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Pamoja madhara ya wadudu pia hueneza magonjwa mbali mbali ya mimea, hivyo kutunza shamba kuwa safi hasa kupalilia; kuchimba na kutupa mbali maotea pamoja na masalia yote na kubadilisha viazi na vipando kama maharage, mahindi, hupunguza madhara.[/FONT]
  [FONT=&amp]SOMO LA NNE[/FONT]
  [FONT=&amp]KILIMO CHA NJEGERE[/FONT]
  [FONT=&amp]UTANGULIZI:[/FONT]

  [FONT=&amp]Njegere ni moja ya mazao ya mikunde inayolimwa katika maeneo ya ukanda wa juu. Hapa nchini Tanzania hulimwa nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru. Katika ulimwengu hulimwa kwa wingi katika Asia ya kati, Mediterania na Afrika ya kaskazini.[/FONT]

  [FONT=&amp]AINA ZA NJEGERE:[/FONT]

  [FONT=&amp]Zipo aina mbili za njegere:-[/FONT]
  [FONT=&amp] I. [/FONT][FONT=&amp]Njegere zinazolimwa shambani – Pisum salivum.[/FONT]
  [FONT=&amp] II. [/FONT][FONT=&amp]Njegere zinazolimwa bustanini – Pisum arrences.[/FONT]

  [FONT=&amp]Pisum – salivum:[/FONT]

  [FONT=&amp]Aina hii hupandwa kwa wingi shambani na hutumika kwa kuliwa punje kavu na maua yake huwa meupe na mbegu zenye rangi ya kijani kibichi au njano nyepesi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Pisum – arrences:[/FONT]

  [FONT=&amp]Aina hii huwa na maua yenye rangi nyekundu / zambarau. Mbegu huwa na rangi ya kijani kibichi au kijivu. Huvunwa kabla ya kukomaa kama mbogamboga, pia huhifadhiwa kwenye kopo.[/FONT]
  [FONT=&amp]Aina za njegere zinazopatikana Tanzania:-[/FONT]
  [FONT=&amp] I. [/FONT][FONT=&amp]Tanganyika[/FONT][FONT=&amp] yellow.[/FONT]
  [FONT=&amp] II. [/FONT][FONT=&amp]Idaho[/FONT][FONT=&amp] white.[/FONT]
  [FONT=&amp] III. [/FONT][FONT=&amp]Rondo.[/FONT]
  [FONT=&amp] IV. [/FONT][FONT=&amp]Mbegu za kienyeji.[/FONT]

  [FONT=&amp]UMUHIMU WA NJEGERE:[/FONT]

  [FONT=&amp]Matumizi punje teke-[/FONT]
  - [FONT=&amp]Hutumika kama mboga na ina protein nyingi, punje zilizokomaa na pia hutumika kwa chakula.[/FONT]
  - [FONT=&amp]Mmea uliobaki hutumika kwa chakula cha mifugo, mbolea na kuhifadhi unyevunyevu ardhini.[/FONT]
  - [FONT=&amp]………………………………………………………………………[/FONT]
  - [FONT=&amp]………………………………………………………………………[/FONT]
  - [FONT=&amp]……………………………………………………………………….[/FONT]
  - [FONT=&amp]……………………………………………………………………….[/FONT]
  - [FONT=&amp]……………………………………………………………………….[/FONT]


  [FONT=&amp]HALI YA HEWA:[/FONT]

  [FONT=&amp]Zao la njegere hupendelea:-[/FONT]
  - [FONT=&amp]Hali ya ubaridi 17 – 21[SUP]0[/SUP] C[/FONT]
  - [FONT=&amp]Mwinuko zaidi ya mita 1200 usawa wa bahari.[/FONT]
  - [FONT=&amp]Mvua, unyevu wa kutosha na maji yasiyotuama.[/FONT]
  - [FONT=&amp]Udongo, zao hukubali katika udongo uliowekwa mbolea, kulimwa kwa kina na wenye tindikali ya PH 5.5 – 6.5.[/FONT]

  [FONT=&amp]KUTAYARISHA SHAMBA:[/FONT]

  [FONT=&amp]Shamba / bustani itayarishwe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina.[/FONT]

  [FONT=&amp]MUDA WA KUPANDA NJEGERE.[/FONT]
  [FONT=&amp]Inashauriwa kupanda njegere mwanzo wa msimu wa mvua.[/FONT]

  [FONT=&amp]KUPANDA.[/FONT]

  [FONT=&amp]Nafasi za kupanda:-[/FONT]
  [FONT=&amp] I. [/FONT][FONT=&amp]60 sm – 90 sm x 5.7 sentimita kwa mbegu fupi.[/FONT]
  [FONT=&amp] II. [/FONT][FONT=&amp]12 sm – 15 sm x 5 – 7.5 sentimita katika safu mbili za sentimita 90 kwa mbegu inayotambaa.[/FONT]
  [FONT=&amp] III. [/FONT][FONT=&amp]Njegere hustawi vizuri zikipata sehemu za kutambalia.[/FONT]
  [FONT=&amp] IV. [/FONT][FONT=&amp]Mbegu ya njegere huota baada ya siku 7 – 10.[/FONT]

  [FONT=&amp]KUKOMAA KWA NJEGERE[/FONT][FONT=&amp]:[/FONT]
  [FONT=&amp]Kwa njegere teke / mbichi hukomaa siku 60 – 90 na kwa njegere kavu huchukua siku 80 -150 kukomaa.[/FONT]

  [FONT=&amp]KUZUIA MAGUGU.[/FONT]

  [FONT=&amp]Njegere hustawi vizuri katika shamba / bustani isiyo na magugu. Magugu hushindana na kunyanganyana na mimea kutumia virutubisho. Pia huongeza kivuli wakati wa utoaji maua na kusababisha upungufu mkubwa wa mazao. Palizi hufanyika kwa mkono au kutumia dawa za kuua magugu.[/FONT]

  [FONT=&amp]MATUMIZI YA MBOLEA[/FONT][FONT=&amp].[/FONT]

  [FONT=&amp]Mazao yanayowekwa samadi hustawi vizuri. Katika kipindi cha ukuaji ni muhimu kuweka mbolea ya chumvichumvi za nitrogen kwa kipimo cha kg 40 kwa hekari.[/FONT]

  [FONT=&amp]WADUDU WAHARIBIFU[/FONT][FONT=&amp].[/FONT]
  [FONT=&amp]Wapo wadudu wengi ambao hushambulia zao la njegere. [/FONT][FONT=&amp]Baadhi ni kama:-[/FONT]
  - [FONT=&amp]American bollworm[/FONT]
  - [FONT=&amp]Bean flies.[/FONT]
  - [FONT=&amp]Bean Aphids.[/FONT]
  - [FONT=&amp]Pea Aphids huambukiza virusi[/FONT]
  - [FONT=&amp]Green peach aphids.[/FONT]

  [FONT=&amp]Inashauriwa kumwona mtaalam wa kilimo aliye karibu yako kwa ufafanuzi wa kuwazuia wadudu waharibifu.[/FONT]

  [FONT=&amp]MAGONJWA.[/FONT]


  1. [FONT=&amp]Ascochyta:-[/FONT]

  [FONT=&amp]Kutokea kwa mabaka makubwa ya kahawia kwenye majani na matunda. Pia hutokea hata kwenye shina. Katikati ya baka huwa rangi ya kijivu, kingo nyekundu / nyeupe husababishwa na fangasi aina ya Ascochyta pisi.[/FONT]


  1. [FONT=&amp]Root Rot na Blight disease.[/FONT]
  [FONT=&amp](kuoza kwa mizizi na Blingt)[/FONT]

  [FONT=&amp]Husababishwa na fangasi A. pinodella na mycosphaerella pinodes.[/FONT]

  [FONT=&amp]Dalili:-[/FONT][FONT=&amp] madoa madogomadogo yenye rangi ya zambarau / rangi ya kahawia iliyokaza au madoa meusi ambayo huungana na kusababisha jani na maua kuwa yenye rangi nyeusi .[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kutumia mbegu zisizo na magonjwa.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Kuzika mabaki ya mazao yaliyoadhirika kwa miaka 3 – 4.[/FONT]


  1. [FONT=&amp]Downy mildew.[/FONT]

  [FONT=&amp] Husababishwa na fangasi Erysiphe polygoni.[/FONT]

  [FONT=&amp]Dalili:-[/FONT][FONT=&amp]Majani kuonekana kama yamemwagiwa unga na baadae na [/FONT]
  [FONT=&amp] kufa. Ugonjwa unaathiri zaidi mimea kipindi cha uhaba wa [/FONT]
  [FONT=&amp] unyevunyevu.[/FONT]
  [FONT=&amp] Kuzuia:-[/FONT]
  [FONT=&amp] Kutumia sulphur ya unga kama inavyoshauriwa.[/FONT]


  1. [FONT=&amp]Fusarium wilt:[/FONT]
  [FONT=&amp] Husababishwa na fangasi / ukungu Fusarium oxysporum.[/FONT]

  [FONT=&amp] Dalili:-[/FONT]
  § [FONT=&amp]Majani kubadilika rangi kuwa manjano.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Mimea kudumaa.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Ugonjwa ukitokea kwenye mimea michanga huua mmea wote.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Tumia mbegu yenye uvumilivu kwa ugonjwa huu.[/FONT]


  1. [FONT=&amp]Virusi.[/FONT]

  § [FONT=&amp]Mmea huonekana kuwa na uvimbeuvimbe kuzunguka jani. Mmea hudumaa.[/FONT]
  §
  [FONT=&amp]Kuzuia:-[/FONT]
  [FONT=&amp]Kutumia mbegu zisizo na maradhi.[/FONT]

  [FONT=&amp]KUVUNA:[/FONT]

  § [FONT=&amp]Njegere teke huvunwa punje zikiwa bado mbichi.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Uvunaji hufanyika mara 2 – 3 kwa wiki wakati wa kipindi cha ukuaji.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Zaidi ya kilo 3000 kwa hekta za njegere teke huvunwa.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Njegere kavu huvunwa wakati punje zimekauka na kuwa ngumu.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Ni muhimu kuwahi kuvuna njegere kavu ili kutopoteza mavuno zikipasuka.[/FONT]
  § [FONT=&amp]Mavuno ya punje kavu na kilo 1500 kwa hekta.[/FONT]
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu chasha kwa hili, nilikuwa natafuta sana hii kitu
   
 3. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante sana mkuu kwa moyo wako wa ukarimu. Kwli jamii forums ni zaidi ya darasa
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Si kweli nyanya zote asili yake ni Amerika ya kati na kuja kusambazwa duniani. Nchi za tropic kumekuwa na upatikanaji wa nyanya hasa sehemu za rutuba ambazo nyanya mwitu nimezikuta ningali mdogo nakua. Chimbuko la kusema nyanya zimetokea Mexco ni hawa wa ulaya wanaotaka kukuza mambo yao na hitoria zao kwa vile sisi tumekuwa nyuma kuandika mambo yetu kwa kutoweka elimu , matukio na uvumbuzi kwenye maandishi.

  Ndio maana nyoka mwenye pembe nimemwona ningali mdogo na juzi kaja mzungu na kusema amegundua na kumpa jila la mtoto wake. hii ni kutudhalilisha sana.
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo afrika nyanya zilikuwepo hata kabla ya huko ulaya hawajaandika historia yake? na kama ni hivyo sisi tulikuwa tunaziitaje na tulikuwa tunazitumiaje?
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ni kweli je utalifanyia kazi au ndio kama maisha ya wanafunzi akishajibia mtihani ndio mwisho..
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Bidhaa au mazao ya kuingizwa toka nchi nyingine utakuta majina na vishina vya majina yanaelekeana. Sala angalia hii tomato/nyanya hutofautiana misingi ya uambishaji wa asili ya maneno. kwa hiyo hii ni dhahiri nyanya zimekuwepo hapa, ila zilikua ndogondogo sana tofauti na hizi ambazo zimeingizwa toka nchi nyingine.
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ubarikiwe Chasha;

  Nina maswali katika maeneo uliyotaja ya Tanzania yanayostawisha nyanya; ni aina gani zinastawi? b; ni aina gani zina tija kwa mkulima kwa upande wa kutoshambuliwa sana na kutoa mazao yenye faida kwa mkulima?
   
 9. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #9
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu kwa kweli nisikudanganye sina uelewa na hiyo kitu, na hii manua nilikutana nayo mahali nikaona ni bora niwawekee wana janvi ili basi iweze kuwasaidia
   
 10. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Usijali JF ni kisima wataotokea wengine kujibu
   
 11. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  noted with thanx...
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Hii manual umeniletea mkulima mimi, ubarikiwe sana.
   
 13. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hivi Kabechi kanda ya kati kama Dodoma Haikubali? Naona Mwinuko unaotakiwa hapo ni kuanzia Mita 1200 - 1900
   
 14. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kabichi zinakubali sana dom cha muhimu ni maji mengi
   
 15. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Ubarikiwe mkuu kwa taarifa
   
 16. benisrael

  benisrael Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kiukweli kuna aina nyingi tu za nyanya mfono tanya,tengeru97,tengeru 2010,kiboko,meru nk hizi ni aina za nyanya ambazo mbegu zake zimezalishwa kwa mtindo huru (open polinated variety),lakini pia kuna aina zingine ambazo ni chotara (hyrid) kama vile ana fi nk ambazo hukuwa nakufikia zaidi ya mita 3 urefu,huzaa sana hadi kg 25 kwa shina moja,huzaa kwa muda mrefu hadi miezi 6,
  Kwa upande wa nyanya zinazostaimili magonjwa mfano tengeru 97 hustahimili magonjwa kama minyoo fundo roots nematods,yellow leaf curl virus,fusarium wilt nk pia unaweza kuvuna tani 16-18 kwa ekari,pia matunda yake yanaweza kudumu hadi wiki mbili bila kuharibika ,kwa tanya inastamili ukame,matunda yake yana ganda gumu na yanadumu hadi siku 20 bila kuharibika,ni nzuri zaidi kwa kusafirisha kwani hazipondeki kwa urahisi.
   
 17. LIVERPOOL Man

  LIVERPOOL Man Member

  #17
  Oct 14, 2014
  Joined: Oct 8, 2014
  Messages: 5
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  Thanks Chasha Poultry Farm, ni somo zuri kwa watu wote, more especially to the people who grow vegetables.
   
 18. rangau

  rangau Member

  #18
  Feb 7, 2015
  Joined: May 12, 2013
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ungeacha mahali ambayo hujui kuliko kudanganya
   
 19. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #19
  Feb 8, 2015
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Narubongo uko wapi? Moja ya wadau muhimu ambao kwa kweli haijulikani walipo basi ni huyu Narubongo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Ansah Miles

  Ansah Miles JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2015
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nikushukuru chasa kwa shule hii muhimu,umetupatia darasa la ukweli kwa kile ulichopata bila kujali utaalamu ulionao,nishauri tu anayehoji ama kukejeli chapisho hapa si mahali pake,ila kama una swali uliza jf wataalamu ni wengi na watakujibu ipasavyo,nikuombe chasa ukipata chapisho lingine lolote tuwekee ubaoni,ni faida kwa wote
   
Loading...