Ni kwa mda sasa tangu chama cha mapinduzi CCM kijifunge mkanda na kukaza soksi ili kukabiliana na hoja za nguvu na zenye kutetea wanyonge pamoja na maslahi ya taifa za CDM,lakini CCM ikajikuta kilaikipiga hatua 3 CHADEMA 14 hali hii ya kushindwa si tu kwamba ilimsikitisha mwenyekiti wao JK a.k.a Mzee wa udini bali ilionekana ni msiba kwa wana CCM wote hususani mafisadi na wachumia tumbo kadhaa,hali hii ilimpelekea JK aibuke na matamko na kauli mbalimbali ambazo ama hawana uwezo wa kuzitekeleza ama ili kuzitekeleza itabidi watumie gharama kubwa.
CCM kupitia mwenyekiti wao Jk tumeshuhudia kali mbiu kama kuvuana magamba,kuiumba upya CCM,hii yote ni kwa kuwa siku zote hawakuwa wamepata mpinzani wa KWELI ambaye kwa sasa ni CHADEMA,CDM si tu inainyima CCM usingizi wa ndoto tamu za kuendelea kuota wanaendelea kutuibia rasimali zetu bali inawanyima UHURU hata wa kuvaa nguo zao za kijani rangi ambayo haitoi matumaini mazuri unapoikuta amefunikwa nayo mgonjwa hospitali, Hali hii kwa sasa imebidi wavihusishe vyombo vya dola hususani Polisi na Usalama wa taifa hasa kitengo cha propaganda na siasa,ikajikuta pia inaachana na ilani yake ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA ikawa MAISHA MAGUMU na VITISHO KWA KILA MTANZANIA"
Kwa uwoga mkubwa iliyonayo kwa sasa ikajikuta inapanga mikakati yake ya hujuma kwa VIONGOZI WA CDM, wanaCHADEMA, wanaharakati na kila mtu anaeonekana anakikosoa kwa uwazi na bila umakini,Serikali yake ikajikuta inahusishwa na vitendo vya ung'oaji meno, kucha, utoboaji macho na mauaji kwa mgongo wa polisi,Lakini kama haitoshi CCM kwa kutumiaADA za wanachama wake na RUZUKU ya wavuja jasho wa TZ , kuajili madairector kina Mwigulu waje kutengeneza video mbalimbali kama waliyoipeleka sasa sokoni ya "Lwakatale na Ludo" pia kuwanunua vijana waliokosa dira na kukata tamaa kina Mtela na Shonza ili iwatumie kuwasahaulisha watanzania hali ngumu ya maisha iliyopokwa sasa.
Hii yote ni katika kujaribu kujinasua na mkasi wa kushuka daraja la ligi kuu ya kisiasa hapo mwaka 2015. Wakajikuta wanarusha mawe gizani ambayo yameanza hata kuwarudia wao mfano UDINI,huku wakinyimwa na mtanzania jasiri wa kisiasa na kiboko ya mafisadi katibu wa CDM dk Slaa na kujikuta hawaoni wanaongea point mpaka wamtaje,lakini niwakumbushe msemo wa wahenga kwamba"UKIONA MTU MREFU KAZAMA UJUE MFUPI KESHA KUFA"
CHADEMA hatujawahi "KUSHINDWA,TULISHINDA,TUNASHINDA NA TUTASHINDA" CHADEAM haiwezi kufishwa na CCM kwani sio walioifanya iwepo hapo ilpo.