Uzalendo umeniishia: Sasa naipenda CHADEMA

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Wana Jamvi

Kwa muda mrefu nimekuwa katika mgogoro wa kimtizamo kuhusu mvutano kati ya CCM na CHADEMA. Kwetu kizazi kilicholelewa na CCM, imekuwa inatuwia vigumu kusema hadharani kuwa chama chetu kinaboronga. Tatizo kubwa kwetu lilikuwa ni ikiwa tukikubali kuwa CCM inaboronga, twende wapi maana vyama vingine vilikuwa havionyeshi unafuu wote.

Sasa uzalendo umetuishia, na tunaona wazi yafuatayo:
-CCM haiwezi tena kufufuka na kurejesha heshima yake
-CHADEMA kinaelekea kimejipanga vema katika jamii na sasa ni kimbilio hata la wana CCM
-Kazi ya CCM sasa inafanywa na Polisi na Mahakama
-Hata baadhi ya watendaji wa CCM wanapayuka payuka kama walivyokuwa wanapayuka wapinzani.

Naandaa utaratibu wa kutoka kwenye closet na kujiunga na CHADEMA.

Naomba mniunge mkono.
 
Kwenye hilo huhitaji kuomba kuungwa mkono kwani wimbi la mabadiliko lina ongezeka kasi na ukubwa kila siku. Du hata wewe limekukumba? Kazi iliyobaki ni kupata tume huru ya uchaguzi ili uhesabiwe na wenzio na upate haki unayostahili Kama mwananchi mzalendo
 
Hongera, CHADEMA ni chama kwa watanzania kama wewe na walioko CCM
 
Huko wewe peke yako unayeishiwa uzalendo na CCM, kwa sasa ni ukweli usiopingika kuwa CHADEMA ndiyo inayogusa nyoyo za Watanzania wengi popote walipo.

Mfano juzi nilikuwa mjini Napoli, Italia ambao ni mji pekee nchini humo wenye tawi la CCM lakini wanachama wengi wa CCM hawataki tena kusikia ya CCM. Wamesema wazi kuwa wamechoshwa na CCM.

Ni jopu la uongozi wa tawi hili tu ndiyo labda wamebaki na mapenzi kwa chama tawala ambao hupatwa na kigugumizi wanapokutana na hoja za CHADEMA.

Kifupi CHADEMA ndiyo inayowavuta Watanzania wengi hapa ughaibuni na ndiyo inayoongelewa zaidi kwa hisia za kizalendo na mwamko wa kujiunga nayo. Watu wengi wamehamasika na CHADEMA.

Nasikitika kusema kuwa CCM haina watetezi.
 
Karibu sana chadema,chadema inahitaji uungaji wako mkono kwa mawazo,hali na mali,....kulikomboa taifa ni gharama sana!

Kusema kwamba mimi ni mwanachadema kwa sababu leo nimechukua kadi ya chadema hua sikubaliani nako,maana kesho unaweza kumuona JK ukampelekea kadi ya chadema ili akupe kadi ya ccm,....

Chadema isiamini katika wingi wa watu wanao chukua kadi zao, wengi sasa wamegundua ili uthaminike katika ccm lazima upitie upinzani kwanza, then urudi na kadiya upinzani ccm,....

I support chadema, ila sina kadi ya chadema na sidhani kama kuchukua kadi ya chadema ndo kutanifanya niipende chadema zaidi ya sasa
 
Karibu sn ktk chama cha Chadema kwa upinzani wa kweli,Ila uwe na moyo mgumu Kama wa chuma sbb polisi FFU huwa wanapenda sn kutufanyia majaribio ya silaha zao
 
Umefanya uamuzi sahihi ndugu,na ni kweli chama cha magamba kwa sasa kiko kwenye hali mbaya hadi wana magamba wamelikubali juzi kati nilikuwa naongea na mmoja wa makada maarufu wa magamba mwenyewe alikubali na wengi tu wataondoka
 
Karibu sana,na asante kwa kufanya uamuzi uliosahihi kabisa
 
Speaker

Kusema ule ukweli Chadema inao wananchama wengi ambao kadi zao siyo hizi za makaratasi bali ni mihuri yaaa CHADEMA katika mioyo yao.

Binafsi sina kadi na wala sina mpango wa kuwa nayo lakini moyo wangu umejaa Chaddema na hivyo ndivyo walivyo watu wengi wanaoiunga makono chadema.

Viongozi wa chadema fanyeni kazi ya kupiga mihuri ya Chadema kwenye mioyo ya watu na sikugawa kadi za karatasi majukwaani. Mtindo huo ni wa wanamagamba maana kadi kwao ni ulaji siku za uchaguzi.

Chadema furahieni mnapoona watu wakiwanyuma yenu kwenye maandamano hakika hawa ndiyo wanachama wenu maana mmewashawishi pasipo kuwapa chochote lakini wamekubali kwa sasbabu mmegusa mioyo yao.

Mingu ibariki Chadema
Mungu wabariki vionzi wa chadema
Mungu wabariki watu waliokubali kuunga mkona harakati za chadema kuikomboa hii nchi yetu.

Amen.
 
Last edited by a moderator:
Wakubwa, salamuni

Ninaomba kutoa tangazo kuwa, siku usajili wa magari ukifikia herufi za chini CDM, mnishitue, nahitaji gari/pikipiki yangu iwe na namba kati ya hizi hapa chini, au namba yoyote lakini herufi zimalizike na CDM

DSC_0000535.jpg

DSC_0000536.jpg

DSC_0000537.jpg

Nawasilisha. sina mpango wa kusajili usafir wangu kwa miherufi ya ajabu kama CCM na ADC
 
Kwa yeyote atakayebaini namba hizo kuaanza kusajiliwa, in pm anikumbushe ili nisajili chombo changu kwa namba hizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom