Uzalendo umeniishia: Sasa naipenda CHADEMA

naichukia chadema kama navyoichukia MALAWI

Naipenda Malawi lakini nachukia CCM na Sera za ubishi wengi wao wakamatwapo kwenye kona za kutotimiza ahadi. Watatuahidi tena maji, mabarabara, mameli na viwanja vya ndege kila mkoa 2015! Nimechoka kusikia!
 
Aiseeee baba yangu hakuna m2 anayeipenda cdm zaidi yangu wakitaka 2watolee damu nipo teyari kutoa yangu lita 3 kwajili ya viongozi kasoro kwa shibuda

ngoja nipige mbege ndio nikalime
 
Aiseeee baba yangu hakuna m2 anayeipenda cdm zaidi yangu wakitaka 2watolee damu nipo teyari kutoa yangu lita 3 kwajili ya viongozi kasoro kwa shibuda

ngoja nipige mbege ndio nikalime
Walosema pombe noma hawakukosea angalia tu 2015 isikukute umezima kwa mbege ukaikosesha CDM kura buree!!!!
 
Kwanini ulijiunga CHADEMA?, hili ni swali ambalo kamati kuu ya CHADEMA inapaswa kuwauliza viongozi wake ambao hivi sasa wanapitia kampeni ya fukuzafukuza.

Nimejaribu kujiuliza iwapo maswali hayo wataulizwa wahasimu wawili wakubwa ndani ya CHADEMA yaani Dr. Slaa na Mh. Zitto Kabwe. Majibu yanaweza kuwa kama ifuatavyo.

Zitto: Nimekuwa CHADEMA tangu nilipoifahamu siasa na sijawahi kuhama CHADEMA wala kufikiria kujiunga na chama kingine.

Slaa: Mimi nilikuwa mwanachama na kiongozi mtiifu wa CCM, lakini walipokataa kunipitisha nigombee Ubunge nikaona maisha yangu ya kisiasa hayana mwelekeo mzuri ndani ya CCM na nikaamua kujiunga na CHADEMA.

Je, CHADEMA ikiwanyima fursa ya kuwa viongozi mtabaki CHADEMA?

Zitto: Nilikuja CHADEMA kama mwanachama wa kawaida na nilipoona nahitajika kukitumikia chama katika nafasi za uongozi nilifanya hivyo ili kukiimarisha chama. Nimefanya harakati nyingi ndani ya chama kabla sijawa kiongozi na ninaamini ninaweza kuendelea kukiboresha chama hata kama sitakuwa kiongozi.

Slaa: Katika siasa maslahi yangu ni muhimu sana. Ndio maana hata mliponitaka niache Ubunge na kugombea Urais niliweka masharti kuwa maslahi yangu yazingatiwe kwa kulipwa mshahara wa Ubunge. Iwapo chama kitanitoa kwenye uongozi na kunihakikishia maslahi yangu yanaendelea kuwepo basi nitabaki kwenye chama, la sivyo nitatafuta chama kinachoweza kunihakikishia kipato cha kutosha.

Je, kuna chama chochote unachofikiria kuhamia au kuanzisha?

Zitto: Kama nilivyosema awali, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa zaidi ya CHADEMA, sifikirii kuihama CHADEMA wala kuanzisha chama chochote.

Slaa: Akiba haiozi, siwezi kuisemea kesho. Hivi sasa kitu pekee nilichofanya ni kuitunza kadi yangu ya CCM na kuilipia ada ili huko mbeleni lolote litakalotokea niwe sehemu nzuri.Hata hivyo, kwa sasa niko CHADEMA na naitumikia kwa kadri CHADEMA inavyoniletea maslahi ya familia yangu. Siwezi kuisaliti CHADEMA kwa sababu ndiyo inayoniwezesha kuwatunza Josephine na mtoto wetu Junior.

Mbowe: Haya tumewasikia. Sasa tokeni nje tuwajadili.

Mnyika: Naombeni panadol.

Tundu Lissu: Hivi sasa hivi saa ngapi? Mahakama bado ziko wazi?

Marando: Oooh, reminiscence...

Mdee: Maaakuuuuubwa!!!

Prof. Safari: Samahanini jamani nimepatwa na dharura...
 
Ivi hakuna mambo mengine ya kujadili humu JF kwa ujenzi wa taifa letu kuliko kuendelea kujadili migogoro inayotafutiwa ufumbuzi?
 
Hapa nakushauri urekebishe statement yako mkuu, siyo kwamba uzalendo umekuishia bali UMEUPATA UZALENDO ndo maana umeamua kuwa mwanacdm!

That is very true Umeupata uzalendo n'a umeuvua ukondoo!!
 
Wana Jf wenzangu nasikitika sana kuwa mbali ya kwamba nilijiunga CHADEMA Mwenyewe,kwa akili zangu mwnyewe,uamuzi na kwa nia ya dhati,na kwamba nimeazimia kufia CHADEMA nikikitetea kwa nguvu zote bado nakosa RAHA na AMANI kuwa ndani ya chama hiki!Sababu kubwa ni vitisho ninavyopata toka kwa mojawapo wa viongozi wa CCM Wilaya ya Rombo kwa vile kipindi nikiwapo huko nilishiriki kumpigia kampeni ndugu Selasini ambaye kwa sasa ni Mbunge wa jimbo tajwa baada ya kumbwaga B.Mramba wa CCM!Ameahidi kunifuatilia na kuniaharibia biashara zangu huku dar na dodoma baada ya kufanikiwa kumrubuni mmiliki wa nyumba nilikokuwa na biashara ya Saluni maeneo ya KDC Moshi na kuamua kuniondoa kwenye nyumba yake ambayo amepangishiwa mtoto wa kiongozi huyo!pia amefanikiwa kusambaza ujumbe kwa wanachadema wenzangu kuwa mimi nipo mbioni kuhamia CCM habari ambazo si za kweli hvyo wanachama wenzangu kuanza kukosa imani na mimi!
Naombeni ushauri wenu nifanyeje?
 
Mkuu usiogope vitisho,uwe na msimamo kwenye kitu unachokiamini.
 
The best way kama unataka msaada wa kweli, basi mtaje tu huyo kiongozi wa CCM kwa jina. Wapo wenzako humu jamvini ambao watakupa taarifa za ndani zaidi za huyo kiongozi na pengine kuna watakaochukua hatua dhidi yake. Lakini namna hii ambayo umekuja nayo itakuwa ngumu kukusaidia kwakuwa wewe hatukufahamu wala unayemsema hatumfahamu, na hivyo tutakuwa tunajadili kitu cha kufikirika zaidi. Kwa kuwa kiongozi huyo ana nia mbaya na wewe, sioni sababu ya kuendelea kulificha jina lake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom