Umaskini wa Fikra na Uzalendo wa Kinafiki wa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaskini wa Fikra na Uzalendo wa Kinafiki wa Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hossam, Apr 30, 2012.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  WanaJF,
  Ifike wakati tusiogope kuelezana ukweli tu kwa sababu tuna michakato mizito uvunguni, huo sio uzalendo na zaidi sana sio uanaharakati.

  Kwa kipindi sasa nimekuwa nikiombwa kujitokeza humu JF ili kufikisha mawazo na fikra zangu kwa Watanzania wenzangu na hususan wana Tabora, mkoa ambao ama umetengwa, umesahaulika, ama yote kwa mpigo.

  Nimekuwa nikiandika makala nzuri na zenye kupewa support nyingi katika magazeti ya Dira, Tanzania Daima, na Mwananchi na leo hii nimeamua kujitokeza kwa jina sahihi na ID sahihi ili wote tuwe pamoja, naitwa Godfrey Kassanga, mzaliwa wa Tabora, nimesoma Tabora, nimeanza kazi Tabora na nimeoa mke hukohuko Tabora. Narudi kiivi sasa.

  Kila siku Watanzania tumekuwa na lawama na kulalamika kusikoisha hususan kwa serikali iliyokuwepo madarakani 'serikali sikivu kwa mafisadi' na wala hakuna anaye aidha chukuwa hatua stahili ama kutoa mawazo mbadala, ilimradi ni lawama na ulalamishi tu. Taifa hili la Tanzania limekuwa chini ya TANU na baadaye CCM wala hakuna jipya lililofanyika zaidi ya ukwapuaji wa maliasili za walalahovyo na hoi. Hakuna wa kuwakataza viongozi wetu. Kila 'mkubwa anakwiba bila soni' ni wizi kuanzia ngazi ya mtaa hadi serikali kuu, magamba tu. Cha ajabu ni sisi tu wanaharakati ndio tumekuwa mstari wa mbele ama kulaani ama kuwajulisha wanyonge namna jamaa wanavyobwia utamiri wetu. Sio ajabu kwamba somo linaeleweka lakini jee hali hii inafanywa kizalendo, kinafki, ama kwa msukumo unasababishwa na ukinzani wa Magamba?

  Kama jibu ni uzalendo, basi ni wangapi miongoni mwetu, hasa huko vijijini ambao wanaendeleza wimbi la mabadiliko? Ama niulize hivi, ni wangapi kati yetu wanaotumia muda wao mwingi kuelimisha jamii ya Kitanzania mageuzi na demokrasia ya kweli bilz kujali gharama ama matokeo? Sote tunakubalu na kuamini kwamba Chadema ndio chama gangwe pekee chenye majembe yakiyojitolea kuifia nchi yao ili vizazi vyetu vijavyo vifaidi utajiri wa Tanzania, lakini hoja iko palepale kwamba haya majembe tunayasaidia kwa namna ipi? Ni kwa kujaa tu kwenye mikutano ya hadhara ama kwa kuitikia maandamano? Kwangu mimi haitoshi hii, Watanzania tutoe saada na ushirikiano ili demokrasia ya kwelu inayovuishwa sasa isiwe ya msimu wala isiwe ya kubip. CCM hawajalala na wala hawatalala hadi wahakikishe tunakufa vibudu, ni afadhali tuamke na kwa nguvu ya umma wetu tusonge mbele tukiongozwa na dhamira na sio ushabiki.

  Ni kwa takribani wiki mbili sasa nchi yetu imetikiswa na ombwe kuu la uongozi, huku Tanzania 'watawala na magavana' wetu wameumbuana, serikali imetikisika lakini nawahakikishia hakuna jipya kubwa sana litafanyika potelea mbali hoja ya Zitto na udhaifu wa Pinda. Kimsingi namshukuru Zitto lakini nina swali kwa waliopokea hoja yake kwa mikono miwili, 'je wako tayari kuifia yamini na dhaira yao'? Hapa ndipo penye uzalendo. Isije kutoa tafsiri ya kukomoana, maana hata spika madam Anne anaweza tu kuizima hoja hii ikawa ya Lema na uongo wa Waziri mkuu Pinda.

  Nchi inayumba, kila mzalendo na awe mstari wa mbele kuelimisha mwenzake bila kujalu kama Chadema wanakuja ama laah! Ni juzi tu tumeanza kusikia makada wa CCM wanajisalimisha Chadema, lakini je hawa, ambao wengi wao wana tuhuma za 'umagamba' wa afuata nini huku Chadema? Sasa hivi hawahawa walikimbilia Chadema na sisi kushangilia kubomoka kwa ccm ndio hawa sasa wanatugharimu, nani asiyejua kwamba akina Shibuda, Mh MB, wanakinzana na hoja ya Chadema ya kuzikataa posho? Je sio hawa waliotoka ccm na kuja huku kwa wazalendo tukiamini ni wenzetu? Hata kama tutasema hatukujua kama watarudia umaji wao japo wanadai wao ni mvuke, lakini jee wananchi majimboni mwao wamechukua hatua gani ya kizalendo? Je tuamini leo kwamba ni siasa za ushabiki? Hamuwezi kuwa hamjanielewa hapa. Wahenga walisema kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, yaani kila penye ukweli na uongo huwapo na huwa ni juu ya mtu kuchagua bega.

  Chadema kina mengi ya kuyaweka sawa kwa kuwa dola iko mbioni kuangukia kwetu, lakini jee tunawaandaa vipi wananchi wetu kwa mabadiliko haya makubwa, na jee utayari wa Wananchi ukoje katika hili? Ni wangapi watakuwa tayari kupigwa misumari mikononi kwa ajili ya haki?

  Tabora, nirudi kwetu sasa, kwa muda imekuwa ngome mara ya CUF yaani CCM B, mapokezi ya rais ?Kikwete leo Tanga ni ushahidi, mara CCM, lakini Wanyamwezi hawa wamepata nini zaidi ya kuwa mkoa usioungwa kwa lami na mkoa mwingine wowote? Ni sawa tumejitahidi kuwaelimisha wana Tabora, sasa imefika wakati tutashika bakora, bakora ya wimbi kubwa litakalombeba aliyemo na asiye kuwemo, kwa muda huu Tabora ni lazima ikombolewe ili na sisi tuanzishe 'the western liberated zone' tukiungana na wale wa Kigoma, na kule northern Tanzania. Tabora na utajiri wake wa maziwa, asali na misitu, na ardhi nzuri iwanufaishe wana Tabora na Watanzania kwa ujumla, yote haya yatafikiwa tu kwa sisi wenyewe wazawa kwanza kukubali ukweli na pili kuamua mageuzi kwa maendeleo yetu, hii ni kweli.

  Mwisho ndugu zangu niwasihi na kuwaomba kuwa macho na ndumilakuwili ambao huuma upande wauoendao kwa muda wao, wote tuwe makini na walaghai ambao huishi kwa maneno yao, lakkni zaidi sana tujiepushe na akina Pangu Pakavu ambao dhamira na hamu yao ni Mchuzi.

  Nina mengi kwa Wanatabora wenzangu ambayo mimi, Kassanga, nimekata shauri kuifia. Tuwe wote katika mpito huu na huzuni ya taifa katika kupeana moyo na kuelimishana ili siku moja sote kwa umoja wetu tufaidi matunda ya uhuru wetu.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Tabora.
  Godfrey Kassanga.
   
 2. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  umenena mkuu. Ila punguza hasira.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ndio wale wale.
   
 4. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Magamba on duty, sasa kibaya ni kipi alichosema mtoa maada?
   
Loading...