Changamoto kwa watanzania na wana-JF

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,838
8,944
Kwa takribani miongo miwili iliyopita Tanzania imebadilika sana katika nyanja mbali mbali, ni kipindi ambacho tumeshuhudia raslimali nyingi sana zikianza kuvunwa na watawala wakitwambia kwamba mambo yanakuwa mazuri, Ni kipindi ambacho watanzania tumepewa ahadi nyingi kuliko kipindi kingine chochote cha uhuru wetu wa bendera, Lakini hizi ahadi na matumaini yamekuwa makubwa zaidi katika utawala wa kiongozi wetu Jakaya Kikwete. Ni katika utawala wa Kikwete ambaye tulimchagua kwa kishindo mstakabali wa taifa letu umezidi kuzua maswali mengi kuliko majibu, ni kiongozi aliyebeba matamanio na mategemeo ya wengi, lakini vile vile amekuwa kiongozi ambaye kwa kusema ukweli ametokea kuyafifisha haya matamanio kwa kasi ya ajabu mpaka wengine tunajiuliza kama kweli tunaenda nchi ya ahadi kama Musa na wana wa Israeli, mbona tunafuata njia ya ahela? Kwa wale wanaotumia neno uzalendo, waweza diriki uliza kama kweli JK ni mzalendo na sio investor kama Andrew Young na akina Sinclair!

Mengi yameongelewa sihitaji kuyarudia hapa. Swali langu kubwa kwa leo humu kwenye jamvi letu, ni nini wajibu wetu kama watanzania katika kulinusuru taifa? especially watanzania wasomi, wenye exposure mlioko nje ya nchi na walio ndani ofcourse? mengi yameandikwa, wengi tumetofautiana kisera na kimtizamo, lakini ukweli una baki pale pale, Tanzania inatuhitaji wote CCM, CUF, CHADEMA NK! Hakika yabidi tubadili mkakati mbinu (strategy) katika kubadili mwelekeo wa taifa, kinachoonekana sasa, hakuna kiongozi mwenye mpango wa kuishi Tanzania, usishangae wewe unayeishi Boston au Toronto au Tokyo, ukarudi ukaambiwa Tanzania ni private property ya watu na huruhusiwi kuingia. Ni ndoto lakini kwa kasi hii tunavyouzwa na "Moses" ukweli wana wa Israel hatuna kimbilio.

Kipi kifanyike jamani? mimi naona ambayo tumeyafichua kupitia hata JF pekee yake yanatosha kufanyia kazi. Uchaguzi ujao ni miaka miwili na ushee, jamani tuwe ACTIVISTS wote humu tuangalie namna ya kuibadilisha hii serikali kupitia sanduku la kura. Tuanze kujadili namna kila mmoja wetu anaweza kuchangia KUIBADILISHA HII serikali, kwa sababu maovu yake yote tunayajua na wala hatuhitaji tena research au machapisho! Michango ya wote humu ina manufaa sana, lakini haitakuwa na impact endapo hatutaenda on the ground tufanye kile ambacho kitatuondolea hii dhuruma. Mtu aliyeko ughaibuni ni vema ajiulize kwa undani na atafakari nini mchango wake katika kuinusuru Tanzania? Au wajibu wako ni kutuma shekeli tuu nyumbani kwa wadogo zako? Jamani waungwana, hili swala tuliangalie kwa makini sana na tulipe uzito unaostahili.

JF, hata hapa Tanzania imefungua macho walio wengi, sasa basi hata kama watu mnaingia humu kujadili hizi scandals za hawa viongozi wetu, tufike mahali tuanze kucheza ngoma na sio kushangilia tuu. Tujiulize watu kama akina Mwanakijiji, wamejitahidi saaana kuwaambia watawala wetu ukianzia na swala la Ukraine, mikopo nk, lakini watu sasa wanajua hawa wabeba mabox ni wapayukaji tuu! After hawapigi kura! Hata kama una kazi nzuri US, ULAYA, UN nk, at the end of the day Tanzania is your home whenever you think home, ulipokulia, ulikochota maji kisimani, uliposomea primary bila viatu, its Tanzania. We ought to do something practically to salvage what is still Tanzania.

Vitabu vimeandikwa, utafiti umefanywa, lakini bila ya wewe na mimi kuamka, hata kama tungekuwa tunashinda JF hapa, tunaexpose ubadhirifu wa hawa jamaa, hatutabadilisha hali za ndugu zetu, uhuru wa kweli utapatikana pale wenye nacho watakapo kubali kujitoa kafara kwa ajiri ya maskini walio wengi. Najua ni kitu kigumu, lakini bila huo ugumu, Tanzania yenye neema itabakia ndoto kwetu Sengerema na reality kwa wachache pale Oysterbay na Masaki.

Hapa mjini gharama za maisha zinapanda mno day after day, wakubwa hawayajui, wachache wanaojaribu ndo hawa wanakuwa kafara, watanzania wenzangu, tuache porojo, we should all be united against the common enemy and that enemy is known to us all. Hatuwezi kuendelea kwa mtaji huu, we need each other. Najua wengi mnaongea humu kwa nostalgia na wala hamna mpango wa kurudi nyumbani, lakini kumbuka, TZ ndo nchi yetu sote, hata kama leo unakula "good time" huko, bado utakuwa second class citizen tuu na ndugu zako walioko huku ndo wanaonja machungu wanayotubebesha akina Lowassa na JK.

Sina la zaidi watanzania wenzangu, nawatakia Noel njema, na kipindi cha tafakuri mchango wa kila mmoja wetu katika Tanzania ya leo. Tuanze kupeana mawazo ni namna gani tunaweza kujikomboa (kama ulishakombolewa, basi kuwakomboa ndugu zako) kwenye hii minyororo ya umaskini wa kutupwa! Madini yanauzwa tukiwa tunafurahia peremende na shanga tunazopewa, na kodi wanazolipa hawa wazungu ndo tunapewa kama mikopo kwa masharti! Yaani inasikitisha yanayofanyika hapa kwetu TZ, yaani kiongozi anakuwa mwizi mchana kweupeee! Tanzania tunaenda wapi jamani?

Najua tuna mawazo tofauti, lakini, tukipeana mawazo hapa KIPI KIFANYIKE NA SIO KULAUMU TUU, hakika tutasonga mbele. Hakuna mchango mdogo, kila wazo lina umuhimu wake. Lets think big my brothers and sisters after all ya dunia yote ni chumvi, tuliyakuta tutayaacha.

Ngoja niwahi dala dala, giza linaingia.
 
Kwa maoni yangu inabidi tuendelee kulaumu ili kuonyesha kutoridhika kwetu kwa maamuzi mbali mbali ambayo hayana maslahi kwa Watanzania. Pamoja na kulaumu pia kuna umuhimu mkubwa wa kuwafumbua macho Watanzania wenzetu ambao asilimia kubwa wanaishi vijijini kuhusiana na ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi wa CCM na serikali kuhusiana na rasilimali zetu na pia kutumia nyadhifa zao kujitajirisha.

Lingine tunaloweza kulifanya ni kuingia msituni, lakini mimi hili siliafiki hata kidogo. Sababu kubwa ya kutoliafiki ni kwamba bunduki haichagui, inaua aliyekuwemo na asiyekuwemo. Pia kuamua kuingia msituni ni kuuana wenyewe kwa wenyewe, maana ndugu, jamaa na marafiki wa wengi wetu ni wanachama ama washabiki wa chama kimojawapo cha siasa Tanzania. Na tukishaamua kuchukua short cut ya kuingia msituni basi kurudi kwenye 'amani' tuliyokuwa nayo leo hii itakuwa vigumu sana. Tumepata fundisho kubwa la vita za majirani zetu wa Rwanda na hata Burundi wenye makabila mawili tu wahutu na watusi walivyouana kwa maelfu kama siyo mamilioni.

Mchango wangu wa senti mbili.
 
Kwa maoni yangu inabidi tuendelee kulaumu ili kuonyesha kutoridhika kwetu kwa maamuzi mbali mbali ambayo hayana maslahi kwa Watanzania. Pamoja na kulaumu pia kuna umuhimu mkubwa wa kuwafumbua macho Watanzania wenzetu ambao asilimia kubwa wanaishi vijijini kuhusiana na ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi wa CCM na serikali kuhusiana na rasilimali zetu na pia kutumia nyadhifa zao kujitajirisha.

Lingine tunaloweza kulifanya ni kuingia msituni, lakini mimi hili siliafiki hata kidogo. Sababu kubwa ya kutoliafiki ni kwamba bunduki haichagui, inaua aliyekuwemo na asiyekuwemo. Pia kuamua kuingia msituni ni kuuana wenyewe kwa wenyewe, maana ndugu, jamaa na marafiki wa wengi wetu ni wanachama ama washabiki wa chama kimojawapo cha siasa Tanzania. Na tukishaamua kuchukua short cut ya kuingia msituni basi kurudi kwenye 'amani' tuliyokuwa nayo leo hii itakuwa vigumu sana. Tumepata fundisho kubwa la vita za majirani zetu wa Rwanda na hata Burundi wenye makabila mawili tu wahutu na watusi walivyouana kwa maelfu kama siyo mamilioni.

Mchango wangu wa senti mbili.
pamoja na kulaumu ,lakini nadhani pia ni vyema tukasifu pale linapotendwa jema na serikali ,kufanya hivi tutakuwa tunaiencourage serikali.tukiwa tunalaumu panapo lawama lakini hatupongezi pale panapohitajika kupongezwa basi hiyo itakuwa ni siasa ya chuki na sio ya maendeleo.
 
Mimi nimesifia maamuzi mengi na ushahidi wa kutosha umo humu JF. Kwa mfano Muungwana alipoamua kuunda kamati ya madini nilisifia bila woga wala kificho, lakini siku hizi ya kusifia yanakuwa ni machache mno au hakuna kabisa.
 
Wengine hatutungi sera, inabidi angalau tunune ili wale walioshika mpini wajue hatupendi wanayoyafanya. Tukiwachekelea watafikiri wanafanya mazuri. So, we are on the right course.
 
Diaspora wapo na hamu na nia sana ya kutusaidia, ila kuna maswala ya kuwapa moyo nawo, URAIA PACHA, hili hasa likirekebishwa naamini TZ tutanufaika sana, swala tu viongozi wasiwe na woga na ushindani...
 
Back
Top Bottom