Uzalendo na moyo wa kuchapa kazi ndio sifa kubwa ya vijana wa China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111255268459.jpg


Wakati wachina wanaadhimisha siku ya taifa ya vijana, vijana kutoka nchi za Afrika ambao wamekuwa wakiishi China na kufanya kazi pamoja nao, wamekuwa wakitoa maoni mbalimbali kuhusu wanavyowaona wenzao wachina. Maoni ya vijana wengi kutoka Afrika kuhusu vijana wa China yanafanana, na karibu kila mmoja anataja uzalendo kwa taifa lao na moyo wa kuchapa kazi.

Bw. Abdul Maisala kutoka Tanzania yeye anavutiwa zaidi na umakini kwenye kazi, unyenyekevu na ufanisi kwenye kazi. Anasema mwanzoni alipoanza kufanya kazi hapa China, alihisi kama anaonewa kwani alikuwa anaona kuwa anabanwa sana na kazi, lakini baada ya kuona anavyotendewa na bosi wake ndivyo kila kijana mchina anavyotendewa akaanza kuzoea hali hiyo. Lakini baada ya kuongeza umakini na ufanisi kwenye kazi yake, alianza kushangaa baada ya kuanza kupokea ujumbe wa malalamiko kwa njia ya WhatsApp kutoka kwa rafiki zake, wakiuliza kwanini hauonekani “online” na kwanini hajibu ujumbe na pia hawasiliani nao mara kwa mara. Bw. Maisala anasema hilo lilimfanya atambue tofauti iliyopo kwenye mtazamo wa kazi kati ya vijana wa China na Tanzania.

Bw. Bakari Masasi kutoka Tanzania ameishi na kufanya kazi nchini China kwa zaidi ya miaka mitatu sasa. Anasema anakumbuka kabla ya kuja kufanya kazi nchini China alijua kuwa wachina ni wachapa kazi, lakini hakujua wanachapa kazi kivipi. Baada ya kuishi na kufanya kazi na vijana wachina, ametambua kuwa kwa vijana wachina, kazi ni sehemu muhimu ya maisha yao. Bw. Masasi anaona kuwa tofauti na vijana wa Tanzania, vijana wa China licha ya kuwa kazi ni jukumu la kila siku, pia ni wajibu na vilevile ni kama sehemu ya burudani.

Kutokana na maendeleo ya kiuchumi kwa sasa miji ya China ina maeneo mengi ya burudani, lakini kupata muda wa kutosha kwa ajili ya burudani ni jambo gumu. Vijana wengi wa China wanapenda kugawa muda wa wikiendi kupumzika na burudani kiasi. Hii ni tofauti na mazingira ya alikotoka, ambako kuna uwekezano wa kuwa na muda wa kupumzika na burudani kila siku.

Bw. Richard Sejungo kutoka Uganda, anaona moja ya sifa kubwa ya vijana wa China ni uzalendo kwa nchi yao. Yeye anawaweka vijana wa China katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni la wale ambao wanaelekea kuwa watu wazima, ambao anaona ni wenye moyo wa uti kwa mamlaka, wachapa kazi, na wenye uzalendo kwa taifa lao. Hii ni hali tofauti kidogo na vijana wa Afrika, ambao licha ya kuwa wanafanya hivyo, wao kwanza wanataka kushawishiwa, kuhimizwa na sio wote wanaofanya hivyo kwa hiari. Anasema hii inatokana na kuwa wana mifano ya kuiga kutoka kwa wakubwa wao kuhusu utamaduni wa jadi wa utii, kuchapa kazi na kuheshimu muda.

Bw. Richard anaona changamoto iko kwa kundi la pili la vijana, wale wanaotoka kwenye utoto na kuingia kwenye ujana. Anasema kama ilivyo kwa vijana wengine duniani, mawazo yao pia yanaathiriwa na utandawazi. Kutokana habari wanazopata kupitia televisheni na internet, mawazo na mitazamo yao inaathiriwa kiasi na hali ya umagharibi. Lakini uzuri ni kuwa vijana hawa wamekuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa taifa, kwani wao pia ni wachapa kazi, ni wavumbuzi wa mambo mbalimbali yanayosaidia kuhimiza ongezeko la uchumi na pia wao ni soko jipya muhimu.

Kutokana na China kufungua milango yake kwa vijana kutoka Afrika kuja kusoma na hata kuwapa fursa ya kufanya kazi nchini China, polepole moyo wa kuchapa kazi na kuthamini muda vinakuwa ni mambo muhimu ambayo vijana wengi wa Afrika wanajifunza. Lakini pia vijana wa China ni wepesi kutii maelekezo na kuonyesha uzalendo kwa nchi yao iwe ni kwenye mazingira ya kazi au nje ya hapo.
 
Umeongea kitu muhimu sana ila mfano tu nikupe mimi ninapofanyia kazi ubinafsi umejaa sana viongozi wapo bize na matumbo yao wanajijali wenyewe tu seminar kila siku wanajipa plus safar isitoshe inakuja safar ya officer anaenda meneja wewe unabung' aa mimacho tu embu nambie kwa staili hii nawezaje kuwa mzalendo uzalendo unaendana na uhalisia wa kazi pamoja na kupata staiki zako za mzingi embu tusubili wengine tuone wanasemaje
 
Back
Top Bottom