Mikopo ya China ni bora kuliko ya Ulaya

Se Busca

Member
Dec 11, 2023
41
72
Christopher Mutsvangwa Balozi wa zamani wa Zimbabwe nchini China anasema kuwa mikopo ambayo China inatoa kwa nchi zinazoendelea hususani Afrika haijawahi kuwa ya kiunyonyaji kutokana na riba zake nafuu ukilinganisha na tasisi za kifedha kutoka nchi za magharibi kama Benki ya Dunia (WB) na shirika la fedha la kimataifa (IMF).

Anasema "Hakuna nchi yoyote ya Kiafrika inayolemewa na deni la China. Mzigo wa madeni barani Afrika unasabishwa na Benki ya Dunia, taasisi za Bretton Woods za nchini Marekani na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lakini, wanataka kuishutumu China." "Nchi za magharibi zina wivu kwa sababu mikopo kutoka China inaifanya Afrika kuwa ya kisasa

Inaifikisha Afrika kwenye hatua ya uchumi wa dunia. Wale wanaoishutumu China kwa kusababisha mtego wa madeni kwa nchi za Afrika wana wivu. Tunahitaji mikopo mingi zaidi kutoka China."Christopher Mutsvangwa.
Kwa miongoni mingi nchi za Afrika zimekuwa njiapanda huku zikijaribu kutafuta washirika sahihi kutoka nchi
zilizoendelea kama China.

Marekani na Urusi ili kukuza Uchumi wao hali ambayo imepelekea kubadilisha wakoloni kila asubuhi na jioni.
Thomas Sankara aliwahi kusema kuwa " Kuikimbia Ufaransa na kwenda China sio njia sahihi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Afrika bali ni mchezo usio wa akili unaobadilisha mkoloni mmoja kwenda kwa mkoloni mwingine atakaye endelea kukutawala, hakuna nchi ambayo inahuruma kwaajili ya nchi nyingine.

Hakuna mkopo ambao ni bora kuliko mkopo mwingine.

Je, unakubali kuwa mkopo unaotolewa na China kwa nchi za Afrika una riba nafuu kuliko taasisi zingine za kifedha za magharibi kama Benki ya Dunia na IMF?

IMG_9329.jpg
 
hiyo ZAMBIA yenyewe,,,kuna polisi wa kichina
 
China walikubali kugharamia reli ya standard gauge kutoka Dsm, Mwanza, Kigoma, Burundi, Congo, Mpanda yootee, yule chizi akiwa anasaka asilimia kumi akagoma, na wachina hawatoi asilimia kumi, kule kwao wakikujua ni kifo.

Akaanza kukopa hovyohovyo mara Standard Chartered, mara CRDB, NBC, mikopo ya kibiashara, baadae akakata moto, kaiachia nchi janga kubwa sana la mikopo.

Aliendesha nchi kama mchepuko wake.
 
Back
Top Bottom