Jile79
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 17,668
- 13,237
Mengine mengi wanafanya sirini huku yalihodhahiri ni macheche snMbona kuna waislam Bilioni wanasoma Quran na hawafanyi wanachofanya Boko harama na wengine?
Mengine mengi wanafanya sirini huku yalihodhahiri ni macheche snMbona kuna waislam Bilioni wanasoma Quran na hawafanyi wanachofanya Boko harama na wengine?
Katika imani, kutenda dhambi manake kwenda kinyume na dini yako. Na nafikiri hakuna dini/kundi lilosalimika na wale wanaotenda dhambi.Mengine mengi wanafanya sirini huku yalihodhahiri ni macheche sn
Moja ya tabia ya Mtume Muhammad rehma na amani iwe juu yake ni kuwa hakuwa mwenye kulaani watu. Ikiwa ni mwenye makosa mleta Uzi ni vizuri kumsahihisha.Adui wa muislam ni muislam mwenyewe.Mwenyezi mungu akulaani kuuhusisha uislam na ugaidi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kusoma Quran ni habari nyengine na kuifanyia kazi habari nyengine. Lililo haswa ni kuifanyia kazi kwani utaishi nayo. Quran inatutaka tujadiliane na watu kwa wema.Unachanganya hbr.....bokoharamu, isis, alkaeda, etc wanajitetea na nn? Mbona wote hao wanadoma Quran kabla ya kufanya mauaji? Kwasababu ndivyo ilivyo andikwa
Athari za Salafi -Jihad kuenea katika nchi yetu ya Tanzania, Kwanza ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru MwenyeziMungu mwingi wa Rehma na mwenye Kurehemu, Kabla ya hili janga la Corona tunalopitia hivi sasa mwanzoni mwa mwaka 2019 kulikua kuna matukio mbalimbali ya Ugaidi yaliyokua yanajitokeza katika pande mbalimbali za Africa. Ukiachana na nchi kama Mali, Burkina Faso na Libya ambazo zipo mbali kidogo na ukanda huu wa Africa Mashariki , kuna nchi katika upande wa Afrika Mashariki ambazo zina chembechembe za Ugaidi.
Inajulikana kua Tanzania ilikua moja ya nchi ambazo zilitoa au “kurecruit” wanamgambo wa Al Shabab kule Somalia. Mikoa iliyoongoza kutoa wanamgambo wengi ni Tanga, Mwanza na Dar es Salaam. Katika kipindi kile tulishuhudia kijana wa Kitanzania akihusishwa na mashambulizi ya Garissa. Kijana mstaarab alieyetoka katika familia ya kitajiri ya MBERESERO. Naam nipende kushukuru jeshi la Polisi kipindi kile wakishirikiana na Intelligency kupambana na janga lile sanasana ningependa kumshukuru DCI wa kipindi kile CP Diwani Athumani.
Ukiachana na hayo, mwanzoni mwa mwaka 2020 kuna matukio mengi ya Kigaidi yalikua yanatokea saana katika ukanda wa Afrika ya mashariki pamoja na Kusini , specifically nchini Msumbiji (Mozambique) pamoja na Kenya. Hii inatokana na uwepo wa makundi ya Waislam wenye Itikadi kali za Salafi.
Hii inaleta picha mpaka kule Africa ya Kati ambapo mpaka saiv bado kuna kavuguvugu ka udini kanatawala baina ya “Seleka” na “Anti Balaqa”. Makundi ya Salafi yaliyopo Mozambique yanafanya harakat zake karibia na mpaka wa nch iyetu ya Tanzania na hivo bas kuhatarisha usalama wa Raia kwa ujumla. Hofu yangu kubwa ni kuona baadhi ya Vijana wa Kiislamu kushawishika kuingia katika makundi hayo ya kigaidi kama ilivyotokea miaka iliyopita kule Somalia.
Hivyo bas vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama vinapaswa kuzingatia hayo mambo yasijurudie tena. Bado tunahitaj nguvu kazi katika Taifa letu na hivyo bas VIjana wakiiIslam tusishwawishike katika kuyaendea hayo mambo. Mikoa iliyo hatarini zaidi ni ile iliyopo kusini ikiwemo LIndi na Mtwara na ni mikoa ambayo Idadi ya wakazi wengi wao ni waislam .
Na kwa jinsi Serikali ilivyofocus kwenye suala la Corona unawapa muda zaidi kujipanga na kuandaa mikakati madhubuti. Sitoshangaa baada ya kuisha kwa Janga la Corona, janga la Ugaidi kuchkua nafas kama vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama havitatilia mkazo dalili hizi.
ABDULKARIM MZEE
Mwanadiplomasia na Mchambuzi wa Masuala ya Ugaidi katika bara la Afrika
rucotz98@gmail.com
Jihadi ipo, na Mtume hakusema kuwa imekwisha. Isipokuwa Mtume aliita hii ni jihadi ndogo. Mfano wa jihadi hiyo ni aliyopigana Mtume na waliyopigana maswahaba. Au mfano wa vita aliyopigana mwana wa zuoni aliyeitwa Abuu Qudamah. Jihadi hii ni jihadi ambayo lengo si kuleta vurugu, uhasama, chuki na ubaguzi na umwagaji wa damu kwenye jamii. Bali hii ni kuletaamani,utulivu umoja na haki kwenye jamii. Ni jihadi ambayo haibagui.Kuna hadithi siikumbuki vizuri nadhani ni wakati mtume anaelekea ukingoni alisema “jihadi ya vita vita imeisha, jihadi iliyobaki pekee ni baina ya mtu na nafsi yake tu”
Sasa ndugu zangu hawa wanaoenda pigana hovyo huwa sijui wanawaza nini, nadhani haya ni madhara ya kusoma dini pekee bila kusoma vingine(kujua dunia inaendeshwaje) mtu anakuwa ni rahisi saana kuwa brainwashed hasa kama uwezo wake wa kufikiria na kupambanua mambo ni mdogo.
Asilimia kubwa ya wanaopigana jihadi wanaenda kuwatumikia makafiri(marekani bila kujijua) wanaenda kuwa sehemu ya kukamilisha mipango ya watu bila kujijua.
Atleast kidoooogo jihadi wapigane wapalestina maana imeandikwa
Aya ya kwanza ya Jihadi ndogo, mapambano ya silaha, ambayo ilishuka kwa wakati huo, imo kwenye Sura ya 22 ya Qur’an Tukufu, aya ya 39-40. inaelezea wazi kabisa lengo la hii Jihadi ndogo:
“Imeruhusiwa (kupigana) kwa wale ambao wanapigwa, kwa sababu wamedhulumiwa, na kwa hakika Mwenyezi Mungu anao uwezo wa kuwasaidia, wale ambao wametolewa majumbani mwao bila sababu ya haki………”
Halafu tena ikizungumzia kuhusu wale makafiri wa Makkah ambao walipigana vita baada ya vita dhidi ya Mtume na wafuasi wake huko Madina, Qur’ani Tukufu katika sura ya 2, aya ya 190 inasema:
“Na wapigeni vita katika njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanakupigeni vita, wala msiruke mipaka, hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaoruka mipaka.”
Reasoning kubwa saana inahitajika katika mambo haya.
MkuuJihadi ipo, na Mtume hakusema kuwa imekwisha. Isipokuwa Mtume aliita hii ni jihadi ndogo. Mfano wa jihadi hiyo ni aliyopigana Mtume na waliyopigana maswahaba. Au mfano wa vita aliyopigana mwana wa zuoni aliyeitwa Abuu Qudamah. Jihadi hii ni jihadi ambayo lengo si kuleta vurugu, uhasama, chuki na ubaguzi na umwagaji wa damu kwenye jamii. Bali hii ni kuletaamani,utulivu umoja na haki kwenye jamii. Ni jihadi ambayo haibagui.
Masikitiko ni kuwa jihadi hii wapo miongoni mwa madhehebu ndani ya Uislam wanaielewa vibaya mno!
Mfano mzuri wa usahihi wa hii jihad ni Khalifa Umar Ibn Al Khatwaab aliombwa msaada na wakristo wa Syria dhidi ya ufisadi na umwagaji wa damu wanaofanyiwa na Dola ya wa-Roma. Amani haipo! Utulivu wa nafsi haupo! Uislam ukaenda kuwasaidia Wakristo wa Syria na Dola ya Kirumi ikashindwa. Huu ni sehemu ya mfano wa historia ili kuonyesha jihadi ya kugharimu uhai wa mtu ipoje. Hii jihadi Mtume ameiita jihadi ndogo.
Hii ni pindi Mtume na Maswhaba waliporejea kutoka katika vita vya Tabuk, vita vilivyoitwa “Vita vigumu” kutokana na
asili yake magumu yaliyopatikana ndani yake, Mtume- rehema na amaniziwe juu yake- aliwageukiwa maswahaba zake na kuwaambia, “Sasa hivitumetoka kwenye jihad ndogo na tunaelekea kwenye jihad kubwa”. Maswahaba walistaajabishwa na hivyo wakamuuliza Mtume- rehema na amani ziwe juu yake, “Je jihad ipi kubwa zaidi ya hii?”, Mtume- rehema na amani ziwe juu yake- akajibu, “Kwa hakika kwa sasa tumetoka kwenye jihad ndogo na tunaelekea kwenye jihad kubwa...jihad dhidi ya nafsi”
Jihadi kubwa ni jihadi ambayo wengi wa Waislam wameiacha, ndiyo jihadi ambayoitakayo mpeleka kwa Mungu salama. Kwa sababu ni jihadi ambayo mtu anapambana na nafsi yake. Ni usafi wa moyo mbele ya Mola wako. Ni usafi wa kuulinda moyo dhidi ya matamanio yote dhidi ya dunia. Usafi huu ndiyo umebeba msingi mkubwa wa imani! Kushindwa kutekeleza matendo ya ibada kwa moyo safi na kuruhusu nafsi kukuendesha kutaleta madhara makubwa.
Jihadi hii ni kuusafisha moyo, moyo ukitakasika nafsi nayo inatakasika. Nafsi ikitakasika mtu anakuwa na maadili. Mwenye maadili anakuwa na moyo wa huruma, huyo mtu anakuwa muadilifu, ni mwenye tabia njema.
Asili ya moyo ni kwamba umefunikwa na utukufu wa Mwenyezi Mungu; kwa maneno mengine, ni sehemu ambayo Mola wetu anapatazama wakati wote, na hivyo moyo uko wazi kupokea maamrisho matakatifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sharti kuwa uwe umesafishwa dhidi ya matamanio ya kidunia na ubinafsi. Moyo ambao umegubikwa na matamanio haya unakuwa hauko safi kiimani na hivyo hauwezi kupokea ufunuo kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Binafsi mimi nilichagua kuchukua hii njia miaka 2 iliyopita. Masheikh wenye elimu ya kulea nafsi wanapewa majina mabaya kabisa na Waislam wenyewe. Nilivyoamua kwenda kwao sikuenda kwa fikra ya kuwa wao ni wakosefu bali nilikwenda na fikra ya kutaka kuujua ukweli. Hawa Masheikh ni Masheikh wa Kisufi! Wa ki-Twariqah! Allah ni shahidi juu hili; Hawa Masheikh ndiyo wameibeba dini ya Uislam. Kukaa nao kote hawajanifundisha kumchukia mtu! Hata aliyenitendea ubaya wanasema nisimchukie?!
Binafsi ni Sunnih! Madhehebu ya Shafii ninayefuata Twariqah ya Imamul Auliyaa Sheikh Abdul Qadir Al Jaylaan.
Imenifunza nisiishi na hate au kujiona ni bora, kudharau mtu wa aina yoyote, hekima itangulie zaidi. Nisiwe na roho ya kwa nini, imenifunza mwenzangu akipata chema nifurahi, niishi na watu kwa wema. Kufanya bila kutizamia watu watakufikiriaje! Kuwa mnyenyekevu na kufanya kwa ajili ya Mungu,ukiangalia mema yote tuliyoamrishwa ni kuleta mahaba ndani ya jamii yasiyobagua. Ustadhi huwa anasema "Kabla ya dini yatangulie mahaba". Huwezi kumfuata Mtume kabla haujampenda.
Indonesia walikwenda Waislam 9 tu ambao hata kiindonesia hawakijui. Walizungumza nao kwa lugha ipi? Kwa lugha ya mahaba(Upendo)! Ndivyo Mtume na Maswahaba walivyoishi! Mtume alikuwa ni mpole sana. Upole ambao maswahaba wanasema ulikuwa ni wenye kutisha! Kwa maana alikuwa ni mpole mpaka mtu kufanya jambo baya kwake unaogopa!
Hii ndiyo jihadi kubwa ambayo Waislam wanapaswa kupambana nayo. Jihadi ya nafsi! Ni jihadi baina yako wewe na nafsi yako na sheytwaani.
Weka mfano hai katika hili. Kupomoka kwao ni kwa vipi!Kosa lako lipo sehemu moja tu Mkuu
Uliposema kuhusu Masheikh wa Kisufi
Masheikh wengi wa Kisufi,wamepomoka mno katika Itikadi(wameharibu sana)
Na hili ni kosa kuu
Weka mfano hai katika hili. Kupomoka kwao ni kwa vipi!
Karibu.
Mfano ni wa ibada zipi?mfano 1
kuelekeza Ibada kwa Mawalii au Masharifu katika Makaburi yao(Ibada ya Makaburi)
Nafikiri itakuwa ni vizuri ukielezea kwa uwazi. Yaani isiwe kiujumla.mfano 1
kuelekeza Ibada kwa Mawalii au Masharifu katika Makaburi yao(Ibada ya Makaburi)
Nafikiri itakuwa ni vizuri ukielezea kwa uwazi. Yaani isiwe kiujumla.
Acha porojo, futeni vifungu vinavyohamasisha na kuhalalisha mauaji kwa waliotofauti na uislamu....Katika imani, kutenda dhambi manake kwenda kinyume na dini yako. Na nafikiri hakuna dini/kundi lilosalimika na wale wanaotenda dhambi.
Sasa kama wanatenda dhambi zao kisiri siri ni wao na Mungu wao.
Kwaio kama wewe unauhukumu uislam kwa watu laki 2 wakati kuna watu bilioni hawafanyi wanachokifanya hao laki mbili, basi ni vyema ungesoma ukajua nini kinaendelea.
Akili tumepewa tuzitumie na sio tuendeshwe na Medias. Hivi wewe hujiulizi, kwanini Muuaji akiwa jina la kiislam basi media wanamwita gaidi? Kwanini muuaji wa kizungu haitwi gaidi? utasikia alikuwa ana mental issues, au depression. Au huoni yakitokea hata kwa watu weusi?
By the way, kama lipi hufanywa kwa siri ambalo lingekuwa dhahiri basi lingeashiria kitu kibaya?
Acha porojo, futeni vifungu vinavyohamasisha na kuhalalisha mauaji kwa waliotofauti na uislamu....
Unachonisihi nimelifuatilia kwa miaka ila nilichogundua ni kuwa kuna baadhi ya Waislam na Masheikh wenye kuitakidi hivyo pia wana wazungumzia Sufi pasipo kuwajua.Akhuy
Allah akubaarik sana,wengine sisi,hatuna uweledi wa kuandika saana
Nakuomba hili ulifuatilie kwa ukaribu sana,nataraji utapata majibu sahihi
Namuomba Allah atujaalie ni wenye kusikia haki na kuweza kuifuata
Unachonisihi nimelifuatilia kwa miaka ila nilichogundua ni kuwa kuna baadhi ya Waislam na Masheikh wenye kuitakidi hivyo pia wana wazungumzia Sufi pasipo kuwajua.
Hii inatokana na wao wenyewe kuwazungumzia kwenye baadhi ya vitabu vyao kisha wanajihitimishia kuwa Sufi wapo hivi: Kuwa Sufi ni grave worshippers (Waabudu Makaburi), Sufi ni washirikina n.k. Inafika pahala wana watuhumu na kuwatukana Sufi mpaka wanawatukana na Maimam ambao Sufi wanafuata mienenendo yao. Usimpe sikio pekee anayelalamikia kadhia fulani, mpe sikio na anayelalamikiwa kisha utajua uhakika wa mambo jinsi ulivyo.
Imam Ibn Hajar Al Asqalani kwenye Fat'h Al Baari 2nd volume na Sahihi chain kutoka kwa Imam Al Bayhaqi na Al Haakim na Ibn Khuzayma imepokewa kwamba: Bilal Ibn Al Haarith alikwenda kwenye kaburi la Mtume kipindi cha Aamu rramada Ukhalifa wa Umar na akisimama kwenye kaburi la Mtume akasema; " Yaa rasuulallah! Ardhi na mimea imenyauka, tafadhali tuombee kwa Mungu atunyeshelezee mvua kwa ummah wako"
Unaielewaje hii?
Imam Malik anasema: " Whoever studies tafaqaha and didn't study Sufism will be corrupted, and whoever studied Sufism and didn't study tafaqaha will became a heretic, and whoever combined both will be reach the truth. [The Scholar Ali Al Adawi volume.2 p 195]
Imam Ahmad Ibn Hambal: O My son, you have to sit with people of Sufism, because they are like a fountain of knowledge and they keep the remembrance of Allah in their hearts. They are the ascetics and have the most spiritual power [ Tanwir Al Quluub p. 405]
Imam Shafii kawazungumzia pia kwa wema mzuri watu wa Sufi na akasema amekaa kwao na amepata kujifunza dini kwao. ImamAbuu Hanifa kadhalika naye ni vivyo hivyo kuwa ni watu wema kwenye Ad Dur Al Mukhtar vol. 1 p. 43.
Unawazungumzia vipi hao Maimam kwa walichokisema ama kuwazungumzia Sufi?
Nimesoma Tawhiid ndugu, itikadi sahihi naijua. Kadri nilivyozidi kusoma ndivyo kadri nilivyozidi kujua na naandika kwa wema na siyo chuki. Wanaowapinga sufi wengi wao ni Salafi! Na salafi kielimu wamejifunga! Hawaamini wala hawamfuati Imam yoyote wa Sunnih wal Jamaa bali wanawafuata Maimam wenye Itikadi ya kwao. Ikiwa kama wakimfuata Imam wa Sunnih wal Jamaa basi wanachukua kipande kinachoendana na kile kinachokwenda sambamba na kile wanachokipigania wao. Ni watu waliyoivishwa itikadi ni watu wenye uchache wa elimu.
Kadri nilivyozid kutafuta ukweli nikakuta wana wa zuoni wakubwa wote wa Madhehebu ya Hambali walikuwa ni Sufi. Hambal Saudi Arabia wanajinasibu ni dhehebu lao lakini wanakataza Tasawwuf,Kutembelea makaburi n.k. Sikutanguliza itikadi. Nilitanguliza kuujua ukweli.
Ninasoma kwa Sheikh wa kisufi na nahudhuria hafla mbalimbali na hata siku moja sijawahi kushuhudia Sufi wakimuabudu mwengine zaidi ya Allah! Watu wanasema wanamuabudu Mtume sijawahi kuona hill! Watuwanasema wanawaabudu Mawalii sijawahi kuona hili! Watu wanasema wanaabudu makaburi sijawahi kuona hili! Na kuna mengine yanazungumzwa hata sijawahi kuyasikia zaidi ya kutoka kwa hao wanaowatuhumu.
Mimi ni Sunni, madhehebu ya Imam Shafii na nimeridhia kufuata twariqah ya Sheikh Abdul Qaadir Al Jaylaan.