Uwezekano wa kuenea kwa salafi jihadi nchini Tanzania

Mimi ni gaidi wa kiislam na ninafata quran na hadith za mtume sasa sijui wewe unaongelea uislam upi ambao siujui
Ugaidi
ni mfumo wa kulenga mabadiliko ya kisiasa kwa kutisha watu kwa njia ya vurugu au mauaji. Matendo ya kigaidi yanatisha kwa sababu watu wanajeruhiwa au kuuawa. Watendaji wa ugaidi kwa kawaida ni vikundi au watu wasio na cheo au nafasi rasmi.

Mara nyingi si rahisi kutofautisha kati ya magaidi, wapinzani wa uhuru au watu wanaoendesha vita ya msituni. Hata jeshi rasmi za serikali zinaweza kutumia mbinu za kigaidi lakini kwa kawaida hawahesabiwi kati ya magaidi.
 
Kwenye uislamu hakuna Ugaidi.
Ukiwa gaidi ,uslamu wako umeshanajisika
Muislamu hawezi kuwa gaidi kwa hali yoyote ile.
Hakuna Gaidi wa Kiislamu.
Kwenye uislam ugaidi nauita jihad..hivyo mimi ni mujaheed na "nimeamriwa na Allah kupigana na makafiri mpaka dunia yote ikiri kuwa La illah ila Allah na wasipokiri hivyo mali zao na uhai wao ni haki ya upanga wangu."
 
Athari za Salafi -Jihad kuenea katika nchi yetu ya Tanzania, Kwanza ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru MwenyeziMungu mwingi wa Rehma na mwenye Kurehemu, Kabla ya hili janga la Corona tunalopitia hivi sasa mwanzoni mwa mwaka 2019 kulikua kuna matukio mbalimbali ya Ugaidi yaliyokua yanajitokeza katika pande mbalimbali za Africa. Ukiachana na nchi kama Mali, Burkina Faso na Libya ambazo zipo mbali kidogo na ukanda huu wa Africa Mashariki , kuna nchi katika upande wa Afrika Mashariki ambazo zina chembechembe za Ugaidi.

Inajulikana kua Tanzania ilikua moja ya nchi ambazo zilitoa au “kurecruit” wanamgambo wa Al Shabab kule Somalia. Mikoa iliyoongoza kutoa wanamgambo wengi ni Tanga, Mwanza na Dar es Salaam. Katika kipindi kile tulishuhudia kijana wa Kitanzania akihusishwa na mashambulizi ya Garissa. Kijana mstaarab alieyetoka katika familia ya kitajiri ya MBERESERO. Naam nipende kushukuru jeshi la Polisi kipindi kile wakishirikiana na Intelligency kupambana na janga lile sanasana ningependa kumshukuru DCI wa kipindi kile CP Diwani Athumani.

Ukiachana na hayo, mwanzoni mwa mwaka 2020 kuna matukio mengi ya Kigaidi yalikua yanatokea saana katika ukanda wa Afrika ya mashariki pamoja na Kusini , specifically nchini Msumbiji (Mozambique) pamoja na Kenya. Hii inatokana na uwepo wa makundi ya Waislam wenye Itikadi kali za Salafi.

Hii inaleta picha mpaka kule Africa ya Kati ambapo mpaka saiv bado kuna kavuguvugu ka udini kanatawala baina ya “Seleka” na “Anti Balaqa”. Makundi ya Salafi yaliyopo Mozambique yanafanya harakat zake karibia na mpaka wa nch iyetu ya Tanzania na hivo bas kuhatarisha usalama wa Raia kwa ujumla. Hofu yangu kubwa ni kuona baadhi ya Vijana wa Kiislamu kushawishika kuingia katika makundi hayo ya kigaidi kama ilivyotokea miaka iliyopita kule Somalia.

Hivyo bas vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama vinapaswa kuzingatia hayo mambo yasijurudie tena. Bado tunahitaj nguvu kazi katika Taifa letu na hivyo bas VIjana wakiiIslam tusishwawishike katika kuyaendea hayo mambo. Mikoa iliyo hatarini zaidi ni ile iliyopo kusini ikiwemo LIndi na Mtwara na ni mikoa ambayo Idadi ya wakazi wengi wao ni waislam .

Na kwa jinsi Serikali ilivyofocus kwenye suala la Corona unawapa muda zaidi kujipanga na kuandaa mikakati madhubuti. Sitoshangaa baada ya kuisha kwa Janga la Corona, janga la Ugaidi kuchkua nafas kama vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama havitatilia mkazo dalili hizi.

ABDULKARIM MZEE

Mwanadiplomasia na Mchambuzi wa Masuala ya Ugaidi katika bara la Afrika


rucotz98@gmail.com
Naaam nimekuja kidogo na taarifa ya wiki iliyopita kutoka BBC swahili
 

Attachments

  • Screenshot_20200603-122223_Twitter.jpg
    Screenshot_20200603-122223_Twitter.jpg
    94.6 KB · Views: 2
Ugaidi = Uislamu kwa sababu quran inaruhusu kuua ukitetea uislamu
Kwaio unasema kuwa ukiua kwa kujitetea ni sawa na UGAIDI? mhhh Tanzania nayo ni gaidi, maana waliua kipindi cha vita ya kagera. USA ni gaidi, UK ni gaidi, in fact kuna taifa lisilo la kigaidi?

Hebu tutizame ukristo unaruhusu kuua?

Kutoka 21:23 SRUV
Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai

1 Samuel 15: 18 Kisha BWANA akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia.

Ngoja niishie hapa upate kunywa maji!
 
Halafu wewe unaonekana hata hujui nini maana ya jihadi,si semi salafi tuu
Labda ulikaririshwa?
Habari ya somalia ni ya kisiasa zaidi,ule uislamu umeingia kwa sababu ni sehemu tu ya imani yao.
Kule libya Ni bada ya kuondoshwa Ghadafi ndio zikaanza hizo nyimbo za IS kitu ambacho kimepangwa na waliomuondosha Ghadafi ili kuwatungia wimbo wa kuimba wajinga wakati wao wanfanya uharamia wa kidola.
Hivyo hivyo Iraq, Syria na kwenginekop.
Ukisikia Ugaidi ujue kuna Mmarekani anafanya vitu vyake,au Mashoga zake,kwa maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi.
wanatengeneza mazingira ya kuzikalia hizo nchi.
What about bhokoharam , Nigeria, Niger, mali , central africa republic ni agent wa USA ndio wanataka kuzikalia hizo nchi
 
Asante sana binafsi nakubaliana na wewe kabisa mtazamo wangu ni kama naiona Tanzania ikiwa kama Nigeria sio mtabiri kwamba ni lini but at least not later than 2050, kama msisitizo wa serikali kutokuwa na dini ukiendelea kudhoofika hivi. Mungu atupe nguvu na uzima, ambaye hajui kwa taarifa population ya Tanzania ina double after every 20 years.
Kwa hiyo unataka serikali ifanye nini ili kuepusha sisi kuwa kama Nigeria
 
Kwenye uislam ugaidi nauita jihad..hivyo mimi ni mujaheed na "nimeamriwa na Allah kupigana na makafiri mpaka dunia yote ikiri kuwa La illah ila Allah na wasipokiri hivyo mali zao na uhai wao ni haki ya upanga wangu."
Lakini Mbona Mtume aliweza kuishi na Makafiri na Mayahudi, na kuna mchangiaji moja kasema Maneno ya Mwisho ya Mtume alisema Jihad iwe ni Mapambano ya kunusuru nafsi yako, ya mtu moja moja, kwani vita kama hiyo ya jihad haina mwisho , bali kupanda chuki isiyo iisha
 
Kwaio unasema kuwa ukiua kwa kujitetea ni sawa na UGAIDI? mhhh Tanzania nayo ni gaidi, maana waliua kipindi cha vita ya kagera. USA ni gaidi, UK ni gaidi, in fact kuna taifa lisilo la kigaidi?

Hebu tutizame ukristo unaruhusu kuua?

Kutoka 21:23 SRUV
Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai

1 Samuel 15: 18 Kisha BWANA akakutuma safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata watakapoangamia.

Ngoja niishie hapa upate kunywa maji!
Unachanganya hbr.....bokoharamu, isis, alkaeda, etc wanajitetea na nn? Mbona wote hao wanadoma Quran kabla ya kufanya mauaji? Kwasababu ndivyo ilivyo andikwa
 
Mimi ni gaidi wa kiislam na ninafata quran na hadith za mtume sasa sijui wewe unaongelea uislam upi ambao siujui
Hakuna Ugaidi katika uislamu, kwa hiyo wewe unahitaji kupatiwa nasaha,
Katika uislamu kuna jihadi tuu, hii ina masharti na kanuni zake, sio kupita na kufanya mauwaji masokoni na kwenye maeneo ya kiraia wasio na hatia.
 
Kwenye uislam ugaidi nauita jihad..hivyo mimi ni mujaheed na "nimeamriwa na Allah kupigana na makafiri mpaka dunia yote ikiri kuwa La illah ila Allah na wasipokiri hivyo mali zao na uhai wao ni haki ya upanga wangu."
Kakusomesha nanii hivyo?
Au ulijitafsiria mwenyewe?
Tahadhari, na Qur-an, kuna aya zinaitwa Mansukh na Nasikh,
tafuta Mwalimu akufafanulie hiyo aya uliyoitumia,usikurupuke tuu,utajiumiza ,na mwisho utaingizwa Motoni kwa ujinga wako.
Umeifahamu vibaya hiyo aya.
 
Unachanganya hbr.....bokoharamu, isis, alkaeda, etc wanajitetea na nn? Mbona wote hao wanadoma Quran kabla ya kufanya mauaji? Kwasababu ndivyo ilivyo andikwa
Mbona kuna waislam Bilioni wanasoma Quran na hawafanyi wanachofanya Boko harama na wengine?
 
Tanzania ina watu wambea sana na wanafatilia maisha ya watu,unaweza ukanya sehemu usiku wa manane hakuna anayekuona,lakini asubuh utashangaa habari zimesambaa mtaani umekunya.

Usiri hamna so hayo makundi yatajifichia wapi,watamshirikisha nani kama hazijavuja.Ugaidi Tz sahau.

Hao wakina January malamba tu habar zao za siri dhidi ya serikali zilivujaje.
 
Back
Top Bottom